Kwanini mamba hamfanyii fujo Kiboko?

Kwanini mamba hamfanyii fujo Kiboko?

Kwenye mto uliojaa mamba na viboko,ilitokea attempt ya mamba kumla mtoto wa kiboko akaishia kumjeruhi vibaya.Walichofanya viboko kulipiza kisasi maji ya mto yaligeuka damu.Mamba mmoja alipigwa jino la maana akawa vipande.Jino la kiboko ni refu kama mpini wa jembe
Umenikumbusha uongo wa zamani kabla ya TV😂😂😂jini la kiboko ni refu kama mpini😂😂😂 tembo halali anajiegemeza kwenye mti mkubwa
 
Nambie Google ,mjuaji wa kila comment ,unae fit kila mada . happy your own year 2021
Ala! Hivi kumbe kuna mada zingine haifai kabisa kucomment, eti!??? Shame on your short-sightedness. Halafu, kwani mtu anatakiwa atume how many comments, kimfano, kwa kila uzi!??? Ule wimbo wa ^Huo ni Ushamba^ hakutungiwa mwingineyo, ila. Do you even pay for my air-time!???
 
Ala! Hivi kumbe kuna mada zingine haifai kabisa kucomment, eti!??? Shame on your short-sightedness. Halafu, kwani mtu anatakiwa atume how many comments, kimfano, kwa kila uzi!??? Ule wimbo wa ^Huo ni Ushamba^ hakutungiwa mwingineyo, ila. Do you even pay for my air-time!???
Fuatilia Tz safari channel,au fanya utalii wa ndani,tour guide akupe maelezo kidogo kuhusu relation ya hao viumbe ,utakuja kunishkuru.lakini Kama unatafuta umaalufu na like ,si tunakupa shekhe .There is no limitation on comments but it seemed you know everything in this universe.Thus why l like to get you know ,your a winner.

Bravo! Bravo!!!
 
Huwa najiuliza sana, Mamba anakula nyama na Kiboko anakula nyasi, lakini wanaishi sehemu moja. Kwa tabia ya Mamba anakula mnyama yoyote anayekatiza mbele yake. Sasa mbona hamtafuni Kiboko na yuko nae muda mwingi?
Mamba anakula kiboko akiwa mtoto lakini ugomvi wao unakuwa ni mkubwa sana.ila kiboko nae akiwa na mtoto dimbwi aliloko mamba anatimuliwa kabisa tena maeneo hayo haruhisiwi kabisa ni sawa na kikao cha halmashauri kuu ya chama cha ccm eti aende hapo mtu wa cdm na uniform yake
 
SIMBa wanamkimbia honeybadger just for fun simba aliyekuwa stressed anakafinya
THUBUTUUU!!

Simba ni wanyama wasiopenda windo lenye usumbufu kama nyegere.

Ni ngumu sana simba kumuua nyegere!

Kale kajamaa ni kakali na kana ujasiri wa kupambana bila kurudi nyuma. Simba wengi huwa wanakaacha. (labda huenda pia kwa sababu wanakaona ni kaduchu hakana minofu ya kushibisha)

Mnyama pekee mwenye uwezo wa kumuua nyegere ni chui maana chui ana kasi sana na anajua kukamata wanyama haraka bila kusita sita. He is sharp.
 
Kifaru sio sana mkuu> Kiboko ndio hatari na ukikutana nae jua umekwisha kwanza ana mbio kali ndani ya umbali mfupi.
Kinachochangia kiboko kuwa ndio anaeongoza kwa kuua watu kwanza anaua kote kote iwe majini au nchi kavu. Kwa majini anaweza pindua mtumbwi na kwa nchi kavu nyakati za usiku huwa anatoka kwenda kujitafutia chakula na anaweza tembea hata 10 km. Sasa ukutane nae kwenye njia yake ndio utaelewa mziki wake. ANakimbia sana ndani ya short distance.
 
Mamba anakula kiboko akiwa mtoto lakini ugomvi wao unakuwa ni mkubwa sana.ila kiboko nae akiwa na mtoto dimbwi aliloko mamba anatimuliwa kabisa tena maeneo hayo haruhisiwi kabisa ni sawa na kikao cha halmashauri kuu ya chama cha ccm eti aende hapo mtu wa cdm na uniform yake
Wengi wamechangia lakini jibu hasa wameshindwa kulitoa. Jibu ni kuwa mamba huua windo lake kwa kulizamisha majini na kufa kwa kukosa hewa. Pamoja na kuwa mamba ana meno makali na yanayojeruhi sana lakini kinachofanya aue windo lake kwa urahisi ni kwa sababu analizamisha kwenye maji na kufa kwa kukosa hewa. Na kiboko ni mkubwa na ana uwezo wa kukaa majini kwa muda mrefu bila kutoka kuvuta hewa. Hivyo kama mamba atajaribu kumshambulia mapigano yataendelea mpaka ndani ya maji na kwa ukubwa wa kiboko uwezekeno wa kushinda ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom