Kwanini Makuzi ya Mtoto wa Kiafrika 100% ni Bakora na Adhabu, ila ya Mzungu ni 100% Maelekezo na Ushauri?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,920
Hivi kuna mwana JamiiForums aliyepigwa Bakora za 'Kishalubela' na kupewa Adhabu Kali kuanzia Shuleni na hadi Kitaani kama Mimi?

Ni kwanini Watoto wengi wa Kiafrika (hasa Kitanzania) tunakuzwa zaidi kwa Fimbo (Bakora) na Adhabu Kali ndipo tunanyooka na kuwa na 'Maadili' tofauti na Watoto wa Kizungu?

Leo nitakuwa Msomaji tu zaidi wa 'Comments' zenu hapa huku nikikumbuka Bakora nilizolambwa na Adhabu Kali nilizopewa nikiwa Mtoto ili ninyooke na hakika zimeninyoosha hasa.
 
Change of mindset/attitude = change of action. Ukibadili mtazamo wako juu ya malezi ya mtoto wako, utabidili pia namna utakavyomlea na kumjengea uwezo wa kufikiri bila kutumia nguvu. Actually, mara nyingi matumizi ya nguvu huwa si matumizi ya akili. Kutumia akili kunaendana na kufanya kitu au jambo kwa weledi (the art of persuasion), wakati kutumia nguvu kunaondoa weledi.
 
Wote tumenyooka kutokana na makuzi ya kuchapwa bakora kama wewe, kuchapwa na kunaanzia kwa wazazi wetu hadi shuleni' pia sisi waislamu adhabu ya bakora haina kikomo cha umri, kwahivyo kuchapwa bakora ni adhabu sio kwa watoto, hata kwa watu wazima kwa mujibu wa Quran na Bible tukufu.
 
Waafrika tunatumia Sana nguvu kuliko akili.Thus madikteta wengi wapo afrika.
Madikteta wote ni matokeo ya child abuse.Ukatili wowote atendewayo mtoto utotoni
(kupigwa,viboko,kutukanwa,kunyanyaswa,kuteswa,nk)akiwa kiongozi ni lzm awe dikteta,sabaya jiwe ni kielelezo cha malezi ya ukatili utotoni.
Wenzetu ufanya vetting ulilelewaje utotoni kabla ya kupewa uongozi.
 
Waafrika tunatumia Sana nguvu kuliko akili.Thus madikteta wengi wapo afrika.
Madikteta wote ni matokeo ya child abuse.Ukatili wowote atendewayo mtoto utotoni
(kupigwa,viboko,kutukanwa,kunyanyaswa,kuteswa,nk)akiwa kiongozi ni lzm awe dikteta,sabaya jiwe ni kielelezo cha malezi ya ukatili utotoni.
Na wakoloni wazungu na waarabu waliokuja Africa na kuwachapa babu zetu mijeledi na bakora nao walikua wakitokea kwenye family za kiafrica zenye tabia ya child abuse?
 
Wakoloni walipokuja Afrika walichapa watu wazima kama watoto. Mimi ninaona upeo wa kufikiria uko chini kwa Mwafrika. Anakuambia nawa mikono kwa sabuni kabla ya kula, mzungu akigeuza mgongo hunawi, unafakamia tu msosi!kuchapwa ni halali, ili kumlazimisha mtu kufikiri. Angalia mseminari wa Kikatoliki anaongea kiingereza kizuri baada ya kunyooshwa kwa adhabu shuleni.
 
Viboko vina faida na hasara yake, mimi binafsi mpaka sasa sijaona sababu ya kuchapa watoto, pengine kwasababu sijapata mtoto nunda (unruly child). ila akitokea nunda nitammiminia viboko na nitamfurahisha
 
nikiwa mdogo mama (R.I.P) alininyoosha kwelikweli kiasi kuna muda nilimuona kama adui lkn matunda yake nayaona leo ukubwani kitabia.mwanangu nitakuja kumlea kama mimi nilivyolelewa.
 
Naona umeacha kuwa unajitaja taja as if you are someone special
" Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer " GENTAMYCINE.

Sasa kama tu Rais wako Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Taasisi zake zote Nyeti, Wabunge wa JMT, Watendaji wake Kurugenzi ya Mawasiliano, CDF Mabeyo, Wanafunzi wengi UDSM, SAUT Mwanza na TUMAINI University ( hasa Tawi la Dar es Salaam), Bloggers mbalimbali wakichukua 'Maandiko' yangu hapa na Kuyatumia huko Kuvutia Wasomaji wao na Waandishi wa Habari na Wachambuzi mbalimbali huku 'Boss 'wa Radio One Mtani wangu Deogratius Rweyunga na Watangazaji wa Michezo Azam Tv na East Africa Radio wakinifuatilia na mwisho Wewe Mwenyewe ambaye Unanichukia 'Kunakotukuka' GENTAMYCINE lakini kutwa ukiwa JamiiForums huachi 'Kunikodolea' kwanini unadhani nisijione 'that Special' au 'Galacha' hapa Jamvini?

Nimebarikiwa tu na Mwenyezi Mungu.
 
digba sowey naona 'Natural Charm' yangu kama GENTAMYCINE hapa JamiiForums inakutesa na Kukukera sana. Pole!!

Kikubwa tu nakushauri usinichukie Mimi bali Kamtatie Rufaa Mwenyezi Mungu ni kwanini amenibariki hivi na Wewe hakuona sababu hiyo ya Kukubariki.

" Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer " GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE.
 
Na wakoloni wazungu na waarabu waliokuja Africa na kuwachapa babu zetu mijeledi na bakora nao walikua wakitokea kwenye family za kiafrica zenye tabia ya child abuse?
Mwafrika bila kiboko aendi,mbona lipo wazi.Nani anawajibika pasipo kusukumwa.Sio utamaduni wetu kuwajibika
 
Imeandikwa. Usimnyime mtoto bakora .

Hamna viumbe waloharibikiwa kama Wazungu wenu hao.


Wanachotuzidi ni Maendeleo tu yalotokana na unyonyaji na matumizi ya mwafrika kama Mjenzi .
Ila kumbuka kuwa wakati hao wazungu wanakuja kutuchukua na kuitawala africa tayari walikua na maendeleo kutuzidi. Kwa hiyo utawala wao ulianzia kwenye uchumi
 
Back
Top Bottom