Kwanini makampuni yana bei tofauti ya Maji yaliyo katika ujazo sawa?

SEASON 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
481
Reaction score
1,015
Katika kuwaza waza leo nilikua nakunywa maji yangu ya Kilimanjaro madogo ya 500ml wakati nimekaa zangu ofisini hapa sina kazi nikawa nimeishika hii chupa naisoma naipembua sioni utofauti wa material ya ziada na wengine lakini maji ya 500ml nimenunua 1000Tsh.

Nikinunua 1.5ltr ya k.njaro bei yake ni 1500
Nikinunua 1.5ltr ya Masafi bei yake ni 700
Nikinunua 1.5ltr ya Uhai bei yake ni 700

Nikishika kopo la maji huwa nasoma composition nakuta vipimo chlorine,mg,nitrate,Ph hivi vipimo vimetofautiana kwa makampuni lakini mimi swali langu leo ni kwenye bei,hivi hili swala la bei kwann k.njaro ana maji gharama kuliko wengine?

Maji si nguo,si tv si radio useme material yaliyotumika ni ghali maji kila mtu anaweza yafanyia treatment yakawa bora yakanyweka,sasa hii bei ya k.njaro inasababishwa na nini kwenye maji yao ya kunywa?

Bei ya Kilimanjaro ni ile ile hata dukani kwa mangi sasa hii kampuni ndio tuseme maji yao ni ORIJINO SANAAAA au tusemeje sasa wakuuu? maji yale yale, chupa zile zile huu utofauti wa bei unatokaga wapi,na hizi bei ni kwa ajili ya maji tunayoyanywa au ni bei za package za maji yanapohifadhiwa? maana sielewi inakuaje maji lita 1 huyu auze 500 yule auze 1200 yule auze 700 huyu auze 600 hizi bei nani anazipanga kwanza?

Wataalamu wa maji naomba mnisaidie hasa hasa haya maji orijino ya kilimanjaro yana tengenezwa na nini? au chem chem ya haya maji ipo huko mbinguni maana huwa sielewi kwanza tofauti kati ya K njaro na Hill, uhai atleast yana taste ya uchungu uchungu ila hawa ambao taste zinalingana nini sababu ya bei zao kuwa tofauti?

Na swali la mwisho,Je kuna maji orijino na feki?
 
Unajua kinacho uzwa sio maji ila ni mechanism ya mteja hadi kuyapata
Nielekeze vizuri mkuu bado sijaelewa lakini usisahau kunipa jibu la kwanini bei ya maji ni tofauti wakati ujazo nii sawa.
 
Katika kuwaza waza leo nilikua nakunywa maji yangu ya Kilimanjaro madogo ya 500ml wakati nimekaa zangu ofisini hapa sina kazi nikawa nimeishika hii chupa naisoma naipembua sioni utofauti wa material ya ziada na wengine lakini maji ya 500ml nimenunua 1000Tsh.

Nikinunua 1.5ltr ya k.njaro bei yake ni 1500
Nikinunua 1.5ltr ya Masafi bei yake ni 700
Nikinunua 1.5ltr ya Uhai bei yake ni 700

Nikishika kopo la maji huwa nasoma composition nakuta vipimo chlorine,mg,nitrate,Ph hivi vipimo vimetofautiana kwa makampuni lakini mimi swali langu leo ni kwenye bei,hivi hili swala la bei kwann k.njaro ana maji gharama kuliko wengine?

Maji si nguo,si tv si radio useme material yaliyotumika ni ghali maji kila mtu anaweza yafanyia treatment yakawa bora yakanyweka,sasa hii bei ya k.njaro inasababishwa na nini kwenye maji yao ya kunywa?

Bei ya Kilimanjaro ni ile ile hata dukani kwa mangi sasa hii kampuni ndio tuseme maji yao ni ORIJINO SANAAAA au tusemeje sasa wakuuu? maji yale yale, chupa zile zile huu utofauti wa bei unatokaga wapi,na hizi bei ni kwa ajili ya maji tunayoyanywa au ni bei za package za maji yanapohifadhiwa? maana sielewi inakuaje maji lita 1 huyu auze 500 yule auze 1200 yule auze 700 huyu auze 600 hizi bei nani anazipanga kwanza?

Wataalamu wa maji naomba mnisaidie hasa hasa haya maji orijino ya kilimanjaro yana tengenezwa na nini? au chem chem ya haya maji ipo huko mbinguni maana huwa sielewi kwanza tofauti kati ya K njaro na Hill, uhai atleast yana taste ya uchungu uchungu ila hawa ambao taste zinalingana nini sababu ya bei zao kuwa tofauti?

Na swali la mwisho,Je kuna maji orijino na feki?
Ubora. Mfano Kuna maji ukiyanywa unaskia ladha ya chumvi, kilimanjaro ni matamu, Yana ladha na hayana chumvi

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
sawa lakini napenda kujua kwanni haya yauzwe bei ya juu yale yauzwe bei ya chini wakati ya bei ya juu ni madogo kuliko haya ya be ya chini?
 
Kwanza ongera kwa kuwa na buku la kunywa maji tuu wakati wengine wanatafuta buku kwa UDI na uvumba siku yake ipite.

Tuje kwenye mada yako

Hakuna fair competition kwenye viwanda vya maji.

Vipo vinavyouzia umaarufu wao ( Brand) kama Kilimanjaro na Uhai. Mo yeye anauza kwa unafuu wa bei.

Tukiacha bei na brand MAJI YENYE PH below 7.2 sinywi hata kwa dawa.

( MAJI NI UHAI LAKINI YALE YENYE PH KUANZIA 7.2- 7.3 TUU MENGINE NI KUKATA KIU TU).
 
Tukiacha bei na brand MAJI YENYE PH below 7.2 sinywi hata kwa dawa.
Una maana k.njaro hunywi wala hill hunywi maana hao ph yao haijawahi kuzidi 7.0

tukirudi kwenye mada bado sijaelewa utofaut wa bei n wann kama maji ni yale yale,basi tumtoe k.njaro tuweke kampuni zingine zenye ujazo sawa lakini bei tofauti hao nao wanakua nanini?

kwamaana hiyo maji ni yale yale tofauti ni makampuni tu kujiamulia si ndio?
 
Sisi makondakta wa daladala tunajinwea ya lita moja kwa TZS 500 pale simu 2000 wala hatupati shida yoyote.
 
Kwa sasa gharama kubwa ya maji ipo kwenye chupa yake, zipo kampuni ambazo zinatengeneza zenyewe chupa lakini nyingi zinanunua chupa toka kampuni nyingine..

Kingine kwenye parameters hasa TDS na PH..Zinahitaji process ndefu kwenye treatments.. Kwa kampuni nyingi kwa sasa zinachuku maji ya Dawasco kwa further treatments ila kwa Kilimanjaro bado wana dili na Chemichemi.
 
Sis wa huku buza ndani ndani tunajinywea maji yetu ya kuchemsha tu.
 
Haya kidogo bei yake ni rafiki kwa mlaji wa mwisho

b4d2ecf47867a91c0409875c46209415.jpg
 
Kuna kampuni inauza lita 1 sh 200 hapo mawasiliano na makumbusho ila kopo lako, ni maji safi kabisa. Kuna haya maji ya Pangani yameshika soko kwa baadhi ya maeneo hapa dar, yenyewe lita 1 na nusu ni 500.
 
Katika kuwaza waza leo nilikua nakunywa maji yangu ya Kilimanjaro madogo ya 500ml wakati nimekaa zangu ofisini hapa sina kazi nikawa nimeishika hii chupa naisoma naipembua sioni utofauti wa material ya ziada na wengine lakini maji ya 500ml nimenunua 1000Tsh.

Nikinunua 1.5ltr ya k.njaro bei yake ni 1500
Nikinunua 1.5ltr ya Masafi bei yake ni 700
Nikinunua 1.5ltr ya Uhai bei yake ni 700

Nikishika kopo la maji huwa nasoma composition nakuta vipimo chlorine,mg,nitrate,Ph hivi vipimo vimetofautiana kwa makampuni lakini mimi swali langu leo ni kwenye bei,hivi hili swala la bei kwann k.njaro ana maji gharama kuliko wengine?

Maji si nguo,si tv si radio useme material yaliyotumika ni ghali maji kila mtu anaweza yafanyia treatment yakawa bora yakanyweka,sasa hii bei ya k.njaro inasababishwa na nini kwenye maji yao ya kunywa?

Bei ya Kilimanjaro ni ile ile hata dukani kwa mangi sasa hii kampuni ndio tuseme maji yao ni ORIJINO SANAAAA au tusemeje sasa wakuuu? maji yale yale, chupa zile zile huu utofauti wa bei unatokaga wapi,na hizi bei ni kwa ajili ya maji tunayoyanywa au ni bei za package za maji yanapohifadhiwa? maana sielewi inakuaje maji lita 1 huyu auze 500 yule auze 1200 yule auze 700 huyu auze 600 hizi bei nani anazipanga kwanza?

Wataalamu wa maji naomba mnisaidie hasa hasa haya maji orijino ya kilimanjaro yana tengenezwa na nini? au chem chem ya haya maji ipo huko mbinguni maana huwa sielewi kwanza tofauti kati ya K njaro na Hill, uhai atleast yana taste ya uchungu uchungu ila hawa ambao taste zinalingana nini sababu ya bei zao kuwa tofauti?

Na swali la mwisho,Je kuna maji orijino na feki?
Boss,
Bei ya vitu hutegemea mambo kadhaa,
1) Manufacturing Costs. Maji unaweza kuayona yako sawa labda lita moja yote lakini gharama alizotumia mmoja kuyazalisha haiwezi kua sawa na gharama ya mzalishaji mwengine.

2) Demand ya Bidhaa husika. Hapa manufacturing cost weka costant, kitu kikihitajika Sana kitauzwa bei ghali hata kama kimetengenezwa bei rahis. Mfano Bajaj ya tricycle inauzwa mpaka 7.5mil wakat gharama ya kuiunda haifiki hata 3mil.

3) Supply au upatikanaji wa kitu nao huchangia Bei. Kitu kikiwa ni ngumu kupatikana (adimu) basi bei itapanda regardless of gharama za utengenezaji. Kinyume chake pia ni sahihi.

4) Brand ya kitu, yaani jina ambalo bidhaa imelitengenezea. Hapa ndo labda swala lako la maji linaingia kwa kiwango kikubwa. Kilimanjaro Water wamejitangaza Sana, toka kitambo kias cha kuonekana maji flan hiv classic. Hapa ni juhudi alizofanya mzalishaji au msambazaji kujenga jina la bidhaa anayouza.

5) Mtazamo wa Watumiaji (consumers). Hii inaweza kuendana na ile pale juu ila hii inahusika zaidi Watumiaji. Unaweza ukadhan tu kua maji fulan ni masafi, na flan ni machafu bila hata kua umefanya utafiti wowote. Au kama kati ya Simba vs Yanga ulivoamua kuchagua Simba, na CCM vs Chadema ukachagua CHADEMA basi hata kwenye bidhaa unaweza kua na choices zako. Na muuzaji au msambazaji akapanga Bei kulingana na hizo choices.

Ki msingi viko vingi vinavyoathiri bei ya bidhaa husika.
 
Duh! Mkuu swali lako majibu yake ni mengi tu ila mojawapo no biashara huria, kwani mbona ving'amuzi vinauzwa bei tofauti akati vinafanya kazi moja? Soda kwa Mangi sh 500 ila sehemu nyingne mm hotelin 1000, 1500 n.k
Otherwise pole kwa bei kubwa uliko, hapa chuga hiyo kilimanjaro 1.5L ni buku tu.
 
Back
Top Bottom