Kwanini Mahujaji walipendelewa na Kikwete?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,392
39,495
SIDHANI kama upendelo wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa mahujaji waliokwama wakati wa kujiandaa kwenda Hijja umetokana na udini.

Naamini kabisa kuwa kulikuwa na sababu nyingine iliyomfanya Rais Kikwete na watendaji wenzake kukosa usingizi na kuhakikisha kuwa mahujaji wetu wanawahi ibada ya Hijja na mambo yote ambayo yanatakiwa kufanywa wakati wa Hijja tukufu. Miongoni mwa sababu naweza kusema kwa uhakika kuwa haihusiani na dini ya Kikwete.

Ninaandika hili kwa sababu kulifumbia macho ni kuwapa kibali watawala wetu kuendelea kuwatendea Watanzania kwa ubaguzi na upendeleo usio na sababu yoyote ya msingi.

Nimefuatilia sakata hili tangu mwanzo na kwa karibu nimejaribu kuangalia mwitikio wa serikali. Jambo moja ambalo ni dhahiri ni kuwa serikali imewatendea mahujaji hawa kinyume kabisa na jinsi ambavyo wamekuwa wakiwatendea Watanzania wengine wanaojikuta katika adha ya kukwama kutokana na matatizo ya chombo cha usafiri.

Kama watu wanavyoweza kukumbuka, mahujaji zaidi ya 300 walitakiwa kuondoka nchini kuelekea Saudi Arabia mapema Disemba, ili kushiriki katika ibada hiyo wakiunganika na mamilioni ya Waislamu wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani. Hijja ni mojawapo ya Nguzo Tano za dini ya Kiislamu ambako muumini wa Kiislamu mwenye uwezo wa kwenda Hijja anatakiwa kufanya hivyo angalau mara moja katika maisha yake.

Hivyo utaona kuwa Waislamu wengi kati ya mambo mengi ya imani ambayo wanayafanya katika maisha yao, Hijja huwa kama kilele cha kutimiza yale yaliyoamriwa na Mwenyezi Mungu.

Nguzo nyingine Nne za Uislamu ni Shahda (kushuhudia kuwa Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake), Sala, Zaka, na Saumu. Kwa Mwislamu yeyote kuishi na kutimiza nguzo hizo ni sehemu ya msingi wa imani yake. Kwenye suala la Zaka hata hivyo, Waislamu wa Tanzania wamekuwa wakienda Hijja kila mwaka wakipanga na kujipangia safari zao kama kawaida na wanarudi salama salimini.

Mwaka huu hata hivyo kuna uzembe mkubwa uliofanyika kati ya wale walioaminiwa kusimamia mipango ya safari hii na hasa vikundi vile ambavyo havikutaka kuingia katika mpango wa Bakwata na hivyo kujitafutia usafiri wao wenyewe. Hivyo tunapozungumzia mahujaji waliopendelewa tunawazungumzia wale ambao tu waliamua safari yao kufanywa na taasisi mbalimbali za kidini ambazo si Bakwata.

Taasisi hizo kwa sababu wanazozijua wao waliamua kutumia Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya kuwasafirisha mahujaji wao. Shirika ambalo limetoka kwenye hali mbaya ya kiuchumi, lenye kidege kimoja, shirika ambalo halifanya shughuli ya kusafirisha mahujaji kwa miaka zaidi ya kumi sasa.

Kidokezo cha sababu hizo kipo kwenye majibu ya ATCL kwa Wizara ya Miundombinu kwenye barua yake ya Desemba 12, 2007. Katika majibu yao kampuni hiyo ya ndege ilieleza wazi kuwa tangu mwanzo haikuwa tayari kuhudumia mahujaji mwaka huu na ya kuwa hakukuwa na mkataba wowote kati yao na kampuni ya RAK Leasing katika kusarifisha mahujaji. Suala la ‘safeguard’ ya maslahi ya mahujaji halikuwapo.

Sababu pekee ni ushawishi wa Mwenyekiti wa Bodi, Mustapha Nyang'anyi, kwa ATCL ndiyo kampuni ikaingia mkenge wa kujaribu kusafirisha mahujaji bila ndege yoyote! Katika majibu hayo yao kwa Waziri wa Miundombinu, kulikuwa na barua iliyokuwa imeandaliwa kupelekwa kwa taasisi za Hijja, lakini barua hiyo ilizuiwa baada ya mwenyekiti huyo wa bodi kuingilia kati.

Majibu ya Bodi yanasema kuwa “Barua ya ATCL yenye Kumb. Na DZ/C.1/99 ya Julai 26, 2007 ilikuwa na lengo la kutoa taarifa hiyo lakini haikufikia walengwa kwa maagizo ya mwenyekiti wa bodi.”

Ni hadi pale mahujaji walipojikuta wamekwama pale Kipawa ndipo siri ikafichuka na ndipo jitihada za kweli za kutafuta utatuzi zilipotokea. Ndipo watu wakamuona Mama Salma Kikwete akienda airport ‘kuwapa moyo’ mahujaji, na baadaye viongozi wa kisiasa n.k wakajitokeza kujaribu kutatua tatizo hilo.

Matokeo yake ni serikali kuingilia kati kwa ahadi ya kuhakikisha mahujaji wanaondoka na ndipo kwa jitihada kubwa mkataba ukaingiwa wa kuwasafirisha mahujaji hao, mkataba ambao na wenyewe ulikuwa na mapungufu yake.

Serikali ikatoa na ahadi kuwa mahujaji watapewa “kifuta jasho” baada ya usumbufu mkubwa walioupata na Rais wakati anazungumza na waandishi wa habari akaahidi kabisa kuwa atahakikisha kuwa mahujaji hawapati matatizo yoyote wakati wa kurudi nyumbani.

Kwa jinsi serikali ilivyoingilia kati sakata hili la kukwama mahujaji na jinsi viongozi wakuu wa nchi hii walivyojishughulisha, bila ya shaka kuna maswali ambayo watu wanayo na mimi ni mmoja wao. Maswali ambayo yameulizwa pembeni lakini miye nayauliza hadharani. Kwa nini?

Ili kuelewa uzito wa maswali haya naomba niwakumbushe kisa kingine cha mapema mwaka jana ambacho leo hii kwa wengi kimeshasahauliwa na hakina maana yoyote. Kwa wengine kisa hiki imekuwa ni ‘mavi ya kale’ ambayo hayanuki. Lakini kwa sisi wengine ambao tunafuatilia utendaji kazi wa serikali, kitendo cha serikali kuingilia kati safari za mahujaji na kutumia fedha zake nyingi (wasizokuwa nazo) kuwasafirisha, kuwalisha na hatimaye kuwarudisha Tanzania. Labda niliweke hili katika mwanga wa kile kisa kingine cha Watanzania waliojikuta wamekwama mahali fulani.

Pale wanafunzi 29 wa Kitanzania walipojikuta wanakatishwa masomo yao na kwa mabavu serikali ikaamua kuwarudisha nyumbani huku ikidai “walienda kule kwa maamuzi yao, na serikali haikuhusika kuwapelekeka” na baadaye kutuma barua za mkataba wa mikopo ili warudi nyumbani, mkataba ambao una miezi sita ambapo vijana wale watadaiwa, na hivyo kukatishiwa masomo yao huku wakiwa hawana uhakika wa kuendelea na masomo nyumbani. Watanzania tulikubali maelezo hayo ya serikali na tukawapa kibali cha uonevu.

Wanafunzi wale wakaomba kila aina ya msaada kutoka kwa viongozi wao na kutoa ushahidi wote waliokuwa nao kuwa hawakwenda kwa kujitakia na ya kuwa walikuwa wamekubaliwa mikopo ya kwenda kusoma; hakuna aliyesikia hata kuamua kulizungumzia isipokuwa kutupiana mpira.

Si Kikwete aliyesema Msolla keshalizungumzia na si Msolla ambaye naye akasema Rais ameshalitolea maelezo. Si Lowassa kiongozi mahiri, shujaa, aliyetamba bungeni aliyejitokeza na kukutana na wazazi wa watoto hawa! Serikali ikanawa mikono kabisa na kwa kumtumia Gesimba akazungumza na kuwakana watoto hawa hadharani huku mapovu yanamtoka kwa jazba! Wananchi tukakubali.

Cha kushangaza ni jinsi gani tumeshindwa kuoanisha na kulinganisha mambo haya mawili na kuona upendeleo mkubwa wa serikali kwa mahujaji. Sakata la wanafunzi Ukraine lilikuwa na sababu kubwa zaidi ya kuingiliwa kati na serikali kuliko suala la mahujaji. Hebu tulinganishe matukio haya na kuona upendeleo mkubwa uliokuwa na chembe za kibaguzi wa serikali kwa mahujaji.

Serikali ilisema wanafunzi walienda kule “kibinafsi” na ya kuwa serikali haikuhusika hata kidogo na walijaribu kuwazuia wasiende lakini “hawakusikia”. Msingi mzima wa serikali kujitoa ni kuwa “haikuhusika” na suala la vijana hawa.

Hebu turudi kwenye mahujaji. Mahujaji walikuwa wanaenda Saudi Arabia kwa sababu binafsi au la? Jibu ni ndiyo. Walikuwa wanaenda kwa sababu binafsi. Ni nani aliwaandalia mipango ya safari ya kwenda huko kwa Hijja? Jibu ni taasisi mbalimbali zenye kujishughulisha na mambo hayo. Kimsingi mahujaji walikuwa wanaenda kwa sababu zao za kidini na serikali haikuhusika hata kidogo katika kutoa mwaliko, kupanga, na kuandaa safari zao!

Kwa upande wa wanafunzi kule Ukraine waliamini ahadi ya serikali kuwa watatumiwa fedha zao za masomo na hivyo watangulie fedha zikifuata. Wakatumia fedha zao kukata tiketi na kuondoka. Mahujaji wakapewa ahadi na mwenyekiti wa ATCL kuwa ndege itapatikana na kutokana na ahadi hiyo waliamini kuwa mambo yatakwenda yanavyopaswa. Wanafunzi 29 wakaenda Ukraine, mahujaji wakaenda airport. Wote wakasubiri ahadi zitimizwe.

Ahadi zikachelewa. Wanafunzi waliokuwa Ukraine wakaanza kuulizia fedha zao na ahadi yao. Wakajaribu kila njia kutaka serikali iwakumbuke na kuwatambua, matokeo yake Profesa Msolla akaongoza shambulio la ukanaji na kuwang'aka vijana hawa. Vijana wakaenda hadi Ubalozi wa Uingereza mjini Kiev na kwa wiki nzima wakapigwa na mvua na baridi. Serikali ya Rais Kikwete akawalia ngumu!

Mahujaji wakapiga kambi airport na wakajaribu kutafuta kila aina ya msaada ili waondoke. Msaada kwa vijana Ukraine wakanyimwa, mahujaji si tu walitembelewa na mke wa Rais bali msururu wa vigogo ukawatembelea na ahadi lukuki!

Matokeo yake, vijana Ukraine wakaambiwa na serikali yao kuwa wakitaka hata kurudi nyumbani lazima watie saini barua za kuomba mkopo wa nauli na fedha hiyo lazima irudishwe baada ya miezi sita. Vijana hawakuwa na ujanja isipokuwa kukatisha masomo, kusaini barua za ‘kujichinjia’ na hatimaye kurudishwa nyumbani bila ahadi ya kuendelea na masomo wala nini. Waliporudi nyumbani wachache walioweza kuendelea na masomo waliweza lakini wengine wakaachwa solemba na kuhangaika mitaani!

Mahujaji hata hivyo, wakapewa ahadi na Rais wa nchi, kuwa “watakwenda Hijja” na jitihada zote zitafanywa. Ikaundwa ‘taskforce’ ya kushughulikia hilo na hatimaye mahujaji si tu walisafirishwa bali pia kugharimiwa. Serikali ikawalipia tikezi bila kutaka mkopo na kumwaga mamilioni ya shilingi huko walikokwenda na kuwahudumia kwa kila namna.

Wenyewe (kama alivyosema Naibu Katibu Mkuu Omari Chambo) walikiita hicho ndicho “kifuta jasho”. Hata wakati wa kurudi, serikali si tu ilituma watu Saudi Arabia bali ilihakikisha hata matatizo ya ukosefu wa ‘slots’ au ndege usingezuia hivyo, wakashirikiana na serikali ya Saudia na hatimaye kuwarudisha mahujaji nyumbani. Rais Kikwete akatimiza ahadi yake kuwa mahujaji hawatapa matatizo yoyote yale wakati wa kurudi. Tukashukuru Mungu.

Hata hivyo katika mambo hayo mawili kuna kitu kimoja ni dhahiri. Serikali iliwabagua vijana wetu Ukraine na kuwapendelea mahujaji. Ni kwa nini basi? Kwanza jibu liko kwenye namba; vijana 29 si namba ya kumkosesha waziri mkuu au Rais usingizi ila mahujaji zaidi ya 300 kwa hakika waliwaumiza kichwa. Hivyo serikali haikutaka kusababisha manung'uniko makubwa kwenye jamii hii hasa ukizingatia familia zaidi ya mia tatu zilizokuwa na wasiwasi ukilinganisha na familia kama 30 tu. Hivyo serikali haikujali wanafunzi.

Pili ni suala la unyeti wa sakata lenyewe. Suala la mahujaji ni suala la imani wakati wanafunzi ni suala la elimu. Kwa wale waliopata nafasi ya kumsikiliza Sheikh Ponda Issa Ponda na baadhi ya viongozi wa dini walivyokuwa wanazungumza kuhusu “kufanya maandamano” serikali haikuwa tayari kukabili ghadhabu ya Waislamu hasa ukiwa na watu kama “mtafutwa” Ponda Issa Ponda.

Manung'uniko ya baadhi ya jumuiya za Waislamu yakaanza kuenea ambapo tetesi za “njama” zikaanza tena. Tayari kulikuwa na suala la Mahakama ya Kadhi na sasa sakata la Hijja kuibuka hakukuwa na mtu serikalini aliyetaka hilo litokee. La wanafunzi Ukraine halikuwasumbua sana kwani lilihusu “elimu tu” na siyo imani ya watu.

Jambo la tatu hata hivyo ni madai ya “undugunaizeshen” uliofanyika. Mitaani ikaanza kusikika kuwa kati ya watu waliokuwapo kwenye msafara wa hija ni baba mkwe wa Rais Kikwete pamoja na ndugu kadhaa wa viongozi wengine. Hadi hivi sasa serikali haikukana hilo na mimi ninaamini kwa ukimya wao wamelithibitisha.

Kama Rais Kikwete alitaka amani nyumbani hakuwa na ujanja isipokuwa kuingilia kati ama sivyo “kula hakuliki na kulala hakulaliki” pale Ikulu. Rais ilimbidi aingilie kati kumwepushia aibu na adha baba mkwe.

Kimsingi tulichoshuhudia ni kitendo cha ubaguzi wa wazi na upendeleo usio na sababu kwa mahujaji kuliko Watanzania wengine wanaopatwa matatizo wakati wa usafiri. Mbona wakati treni imekwama kutoka Kigoma kuja Dar kwa karibu wiki nzima hatukusikia waziri mkuu kenda kuwaangalia au mpango wa kifuta jasho au hata kununuliwa “kuku” wa Itigi na minofu ya Saranda? Ni lini sera ya “kifuta jasho” imeingizwa serikali wananchi wanapopata matatizo ya usafiri na kwanini ianzie kwa mahujaji? Je, kuanzia leo hii wananchi wanaotaka kusafiri na vyombo vya serikali na wakajikuta wanakwama kutokana na makosa ya vyombo hivyo watarajie kulipiwa hoteli, msosi, na kujikimu kwingine, kama sivyo kwa nini?

Kama serikali imeona kuwa ni lazima ijihusishe katika masuala ya namna hii na ya kuwa hata kama mtu akijipangia mambo yake ya binafsi ambayo yanahusisha kwa namna moja au nyingine “ahadi” ya serikali kuwa anastahili msaada basi serikali itangaze kuwasamehe mkopo wa tiketi vijana wetu waliorudi nyumbani toka Ukraine na kuwaomba radhi kwa kuwatelekeza, kuwasusa na kuwakatishia masomo yao kimabavu.

Fedha iliyotumika kuwagharimia mahujaji kwa karibu wiki tatu ingeweza kuwasomesha vijana wote 29 kwa karibu miaka yote iliyobakia! Kama serikali yetu inajali wananchi wake basi ikiri kutowatendea haki na ya kuwa hata wale ambao walikatishwa masomo na sasa wameshindwa kurudi shuleni basi wasamehewe na waahidiwe kuendelea na masomo mwaka huu bila kuumizwa na masharti mapya ya mikopo kama walivyofanyiwa sasa.

Vinginevyo, tulichoshuhudia kwenye sakata la wanafunzi Ukraine na mahujaji pale Kipawa ni matumizi mabaya ya madaraka na uonevu mkubwa kwa watu wasio na sauti. Sisi sote hatuwezi kuwa katika kundi moja na ndugu wa vigogo ili na sisi tupate neema!

Nisieleweke vibaya, tatizo langu si mahujaji kusaidiwa kwani mwenye njaa hana mwiko. Tatizo langu ni msingi wa kuamua kuwasaidia wao na kuwakatilia watu wengine kwenye matatizo kama hayo. Kwa nini serikali ilibagua hivyo? Kama nilivyosema hapo juu siamini msingi ni dini kwani katika kundi la wale wanafunzi asilimia kubwa walikuwa ni waislamu na si wote toka bara. Mmoja ni mtoto wa Shehe!

Serikali ya Rais Kikwete kwa kufanya kitendo hiki cha kibaguzi na upendeleo wa wazi imeonyesha udhaifu mkubwa wa kuongoza na matokeo yake ni kutengeneza kiwango kipya kabisa.

Kuanzia hivi sasa Watanzania wa madhehebu yoyote wakikwama Kipawa serikali lazima iingilie kati! Si kukwama Kipawa tu bali piwa wakikwama pale Relwe au kwenye vituo vingine vya kusafiria ambako chombo cha serikali kilitakiwa kuwasafirisha.

Si kuwasaidia usafiri tu, kuanzia sasa Watanzania wote wanayo haki ya kudai kulipiwa gharama ya chakula na malazi wanapokwamishwa na vyombo vya serikali! Vinginevyo, serikali itueleze kwanini mahujaji walipewa upendeleo?
 
Hiyo makala ilitoka jana kwenye Tanzania Daima. Nimepata email kadhaa kuhusiana na makala hiyo. Mojawapo ni hii ambayo bila ya shaka ilitakiwa iwe public kwani ilitumwa pia kwa Tanzania Daima.

Forwarded Conversation
Subject: KWA NINI WAKRISTO WANAPENDELEWA?
------------------------

From: Tanzania Journalists <tanzaniajournalists@yahoo.co.uk>
To: mwanakijiji@klhnews.com, mpayukaji@yahoo.com, tzdaima@freemedia.co.tz
Date: Thu, Jan 17, 2008 at 9:51 AM
Kwa nini serikali inawapendelea Makafiri kuliko Waislamu nchini Tanzania?

Nimeisoma makala yako iliyo chapishwa ndani ya gazeti la Tanzania Daima, toleo na. 1139 la tarehe 16 Januari, 2008 yenye kichwa cha habari: "KWA NINI SERIKALI IMEWAPENDELEA MAHUJAJI ( WAISLAMU)? ukurasa wa 10.

Niseme kwamba makala hiyo was highly offensive not only to President Kikwete, but to Muslims in Tanzania in particular and Muslims all over the world at large and should be dealt in the manner appropriately.

Huu ni udini, chuki na chokochoko ambazo makafiri wamekuwa wakizionesha dhahiri kwa Waislamu na Uislamu hapa nchini kwa muda mrefu.

Mahujaji walistahiki na wataendelea kupewa kila namna ya msaada unaohitajika ili waende Mecca na Medinah kutekeleza nguzo hii muhimu kwa dini yao.

Chuki za Wakristo na Mapagani haziwezi kufua dafu kwa Waislamu na kama mnataka mapambano, Waislamu tuko tayari kwa hilo, fanyeni fyoko muone cha mtema kuni.

Kwa muda mrefu gazeti hili limekuwa likiandika mambo ya kuwaudhi Waislamu.

Mbona hamuandiki yale serikali hii hii inavyowanyongesha Waislamu?

Nafasi nyeti zote serikalini zimechukuliwa na Makafiri wenye magovi, mbona Waislamu hawasemi kitu, ila suala la Mahujaji mnalivalia njuga, vipi nyie, mmetumwa na mabwana zenu nini?

Wakristo mmekuja juu kuhusu masuala yanayo wagusa Waislamu, km. Mahakama ya Kadhi, OIC, mabucha ya nguruwe, vilabu vya pombe na madanguro ya uzinzi na wanawake kwenda uchi; nk.

Hivi Waislamu wa Tanzania hawawezi kuendesha mambo yao hadi hapo Wakristo watakapo penda, siyo?

Eleweni kuwa Uislamu ni dini yenye mfumo kamili unaojitegemea, hautaki kuingiliwa na makafiri au watawala.

Angalieni chokochoko hizi zitatupeleka pabaya kusiko takiwa.

Angalieni mfano wa huko Iraq , Afghanistan, Kosovo, Chechnea na kwingine kwingi.

Tusipojenga ufa sasa tutajenga ukuta.

Acheni Waislamu wakafanya ibada zao bila kuingiliwa na washenzi kama ninyi.

Mbona Ubalozi wa Vatican upo hapa, ni kwa maslahi ya nani?

Mashule na mahospitali ya Wakristo yanafadhiliwa na pesa za serikali, Waislamu wanafaidika na nini?

Mkiendelea na mwendo wenu kuandika vibaya mambo ya Waislamu mtajuta, acheni ushenzi wenu.
 
SIDHANI kama upendelo wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa mahujaji waliokwama wakati wa kujiandaa kwenda Hijja umetokana na udini.

Naamini kabisa kuwa kulikuwa na sababu nyingine iliyomfanya Rais Kikwete na watendaji wenzake kukosa usingizi na kuhakikisha kuwa mahujaji wetu wanawahi ibada ya Hijja na mambo yote ambayo yanatakiwa kufanywa wakati wa Hijja tukufu. Miongoni mwa sababu naweza kusema kwa uhakika kuwa haihusiani na dini ya Kikwete.

Ninaandika hili kwa sababu kulifumbia macho ni kuwapa kibali watawala wetu kuendelea kuwatendea Watanzania kwa ubaguzi na upendeleo usio na sababu yoyote ya msingi.

Nimefuatilia sakata hili tangu mwanzo na kwa karibu nimejaribu kuangalia mwitikio wa serikali. Jambo moja ambalo ni dhahiri ni kuwa serikali imewatendea mahujaji hawa kinyume kabisa na jinsi ambavyo wamekuwa wakiwatendea Watanzania wengine wanaojikuta katika adha ya kukwama kutokana na matatizo ya chombo cha usafiri.

Kama watu wanavyoweza kukumbuka, mahujaji zaidi ya 300 walitakiwa kuondoka nchini kuelekea Saudi Arabia mapema Disemba, ili kushiriki katika ibada hiyo wakiunganika na mamilioni ya Waislamu wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani. Hijja ni mojawapo ya Nguzo Tano za dini ya Kiislamu ambako muumini wa Kiislamu mwenye uwezo wa kwenda Hijja anatakiwa kufanya hivyo angalau mara moja katika maisha yake.

Hivyo utaona kuwa Waislamu wengi kati ya mambo mengi ya imani ambayo wanayafanya katika maisha yao, Hijja huwa kama kilele cha kutimiza yale yaliyoamriwa na Mwenyezi Mungu.

Nguzo nyingine Nne za Uislamu ni Shahda (kushuhudia kuwa Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake), Sala, Zaka, na Saumu. Kwa Mwislamu yeyote kuishi na kutimiza nguzo hizo ni sehemu ya msingi wa imani yake. Kwenye suala la Zaka hata hivyo, Waislamu wa Tanzania wamekuwa wakienda Hijja kila mwaka wakipanga na kujipangia safari zao kama kawaida na wanarudi salama salimini.

Mwaka huu hata hivyo kuna uzembe mkubwa uliofanyika kati ya wale walioaminiwa kusimamia mipango ya safari hii na hasa vikundi vile ambavyo havikutaka kuingia katika mpango wa Bakwata na hivyo kujitafutia usafiri wao wenyewe. Hivyo tunapozungumzia mahujaji waliopendelewa tunawazungumzia wale ambao tu waliamua safari yao kufanywa na taasisi mbalimbali za kidini ambazo si Bakwata.

Taasisi hizo kwa sababu wanazozijua wao waliamua kutumia Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya kuwasafirisha mahujaji wao. Shirika ambalo limetoka kwenye hali mbaya ya kiuchumi, lenye kidege kimoja, shirika ambalo halifanya shughuli ya kusafirisha mahujaji kwa miaka zaidi ya kumi sasa.

Kidokezo cha sababu hizo kipo kwenye majibu ya ATCL kwa Wizara ya Miundombinu kwenye barua yake ya Desemba 12, 2007. Katika majibu yao kampuni hiyo ya ndege ilieleza wazi kuwa tangu mwanzo haikuwa tayari kuhudumia mahujaji mwaka huu na ya kuwa hakukuwa na mkataba wowote kati yao na kampuni ya RAK Leasing katika kusarifisha mahujaji. Suala la ‘safeguard’ ya maslahi ya mahujaji halikuwapo.

Sababu pekee ni ushawishi wa Mwenyekiti wa Bodi, Mustapha Nyang'anyi, kwa ATCL ndiyo kampuni ikaingia mkenge wa kujaribu kusafirisha mahujaji bila ndege yoyote! Katika majibu hayo yao kwa Waziri wa Miundombinu, kulikuwa na barua iliyokuwa imeandaliwa kupelekwa kwa taasisi za Hijja, lakini barua hiyo ilizuiwa baada ya mwenyekiti huyo wa bodi kuingilia kati.

Majibu ya Bodi yanasema kuwa “Barua ya ATCL yenye Kumb. Na DZ/C.1/99 ya Julai 26, 2007 ilikuwa na lengo la kutoa taarifa hiyo lakini haikufikia walengwa kwa maagizo ya mwenyekiti wa bodi.”

Ni hadi pale mahujaji walipojikuta wamekwama pale Kipawa ndipo siri ikafichuka na ndipo jitihada za kweli za kutafuta utatuzi zilipotokea. Ndipo watu wakamuona Mama Salma Kikwete akienda airport ‘kuwapa moyo’ mahujaji, na baadaye viongozi wa kisiasa n.k wakajitokeza kujaribu kutatua tatizo hilo.

Matokeo yake ni serikali kuingilia kati kwa ahadi ya kuhakikisha mahujaji wanaondoka na ndipo kwa jitihada kubwa mkataba ukaingiwa wa kuwasafirisha mahujaji hao, mkataba ambao na wenyewe ulikuwa na mapungufu yake.

Serikali ikatoa na ahadi kuwa mahujaji watapewa “kifuta jasho” baada ya usumbufu mkubwa walioupata na Rais wakati anazungumza na waandishi wa habari akaahidi kabisa kuwa atahakikisha kuwa mahujaji hawapati matatizo yoyote wakati wa kurudi nyumbani.

Kwa jinsi serikali ilivyoingilia kati sakata hili la kukwama mahujaji na jinsi viongozi wakuu wa nchi hii walivyojishughulisha, bila ya shaka kuna maswali ambayo watu wanayo na mimi ni mmoja wao. Maswali ambayo yameulizwa pembeni lakini miye nayauliza hadharani. Kwa nini?

Ili kuelewa uzito wa maswali haya naomba niwakumbushe kisa kingine cha mapema mwaka jana ambacho leo hii kwa wengi kimeshasahauliwa na hakina maana yoyote. Kwa wengine kisa hiki imekuwa ni ‘mavi ya kale’ ambayo hayanuki. Lakini kwa sisi wengine ambao tunafuatilia utendaji kazi wa serikali, kitendo cha serikali kuingilia kati safari za mahujaji na kutumia fedha zake nyingi (wasizokuwa nazo) kuwasafirisha, kuwalisha na hatimaye kuwarudisha Tanzania. Labda niliweke hili katika mwanga wa kile kisa kingine cha Watanzania waliojikuta wamekwama mahali fulani.

Pale wanafunzi 29 wa Kitanzania walipojikuta wanakatishwa masomo yao na kwa mabavu serikali ikaamua kuwarudisha nyumbani huku ikidai “walienda kule kwa maamuzi yao, na serikali haikuhusika kuwapelekeka” na baadaye kutuma barua za mkataba wa mikopo ili warudi nyumbani, mkataba ambao una miezi sita ambapo vijana wale watadaiwa, na hivyo kukatishiwa masomo yao huku wakiwa hawana uhakika wa kuendelea na masomo nyumbani. Watanzania tulikubali maelezo hayo ya serikali na tukawapa kibali cha uonevu.

Wanafunzi wale wakaomba kila aina ya msaada kutoka kwa viongozi wao na kutoa ushahidi wote waliokuwa nao kuwa hawakwenda kwa kujitakia na ya kuwa walikuwa wamekubaliwa mikopo ya kwenda kusoma; hakuna aliyesikia hata kuamua kulizungumzia isipokuwa kutupiana mpira.

Si Kikwete aliyesema Msolla keshalizungumzia na si Msolla ambaye naye akasema Rais ameshalitolea maelezo. Si Lowassa kiongozi mahiri, shujaa, aliyetamba bungeni aliyejitokeza na kukutana na wazazi wa watoto hawa! Serikali ikanawa mikono kabisa na kwa kumtumia Gesimba akazungumza na kuwakana watoto hawa hadharani huku mapovu yanamtoka kwa jazba! Wananchi tukakubali.

Cha kushangaza ni jinsi gani tumeshindwa kuoanisha na kulinganisha mambo haya mawili na kuona upendeleo mkubwa wa serikali kwa mahujaji. Sakata la wanafunzi Ukraine lilikuwa na sababu kubwa zaidi ya kuingiliwa kati na serikali kuliko suala la mahujaji. Hebu tulinganishe matukio haya na kuona upendeleo mkubwa uliokuwa na chembe za kibaguzi wa serikali kwa mahujaji.

Serikali ilisema wanafunzi walienda kule “kibinafsi” na ya kuwa serikali haikuhusika hata kidogo na walijaribu kuwazuia wasiende lakini “hawakusikia”. Msingi mzima wa serikali kujitoa ni kuwa “haikuhusika” na suala la vijana hawa.

Hebu turudi kwenye mahujaji. Mahujaji walikuwa wanaenda Saudi Arabia kwa sababu binafsi au la? Jibu ni ndiyo. Walikuwa wanaenda kwa sababu binafsi. Ni nani aliwaandalia mipango ya safari ya kwenda huko kwa Hijja? Jibu ni taasisi mbalimbali zenye kujishughulisha na mambo hayo. Kimsingi mahujaji walikuwa wanaenda kwa sababu zao za kidini na serikali haikuhusika hata kidogo katika kutoa mwaliko, kupanga, na kuandaa safari zao!

Kwa upande wa wanafunzi kule Ukraine waliamini ahadi ya serikali kuwa watatumiwa fedha zao za masomo na hivyo watangulie fedha zikifuata. Wakatumia fedha zao kukata tiketi na kuondoka. Mahujaji wakapewa ahadi na mwenyekiti wa ATCL kuwa ndege itapatikana na kutokana na ahadi hiyo waliamini kuwa mambo yatakwenda yanavyopaswa. Wanafunzi 29 wakaenda Ukraine, mahujaji wakaenda airport. Wote wakasubiri ahadi zitimizwe.

Ahadi zikachelewa. Wanafunzi waliokuwa Ukraine wakaanza kuulizia fedha zao na ahadi yao. Wakajaribu kila njia kutaka serikali iwakumbuke na kuwatambua, matokeo yake Profesa Msolla akaongoza shambulio la ukanaji na kuwang'aka vijana hawa. Vijana wakaenda hadi Ubalozi wa Uingereza mjini Kiev na kwa wiki nzima wakapigwa na mvua na baridi. Serikali ya Rais Kikwete akawalia ngumu!

Mahujaji wakapiga kambi airport na wakajaribu kutafuta kila aina ya msaada ili waondoke. Msaada kwa vijana Ukraine wakanyimwa, mahujaji si tu walitembelewa na mke wa Rais bali msururu wa vigogo ukawatembelea na ahadi lukuki!

Matokeo yake, vijana Ukraine wakaambiwa na serikali yao kuwa wakitaka hata kurudi nyumbani lazima watie saini barua za kuomba mkopo wa nauli na fedha hiyo lazima irudishwe baada ya miezi sita. Vijana hawakuwa na ujanja isipokuwa kukatisha masomo, kusaini barua za ‘kujichinjia’ na hatimaye kurudishwa nyumbani bila ahadi ya kuendelea na masomo wala nini. Waliporudi nyumbani wachache walioweza kuendelea na masomo waliweza lakini wengine wakaachwa solemba na kuhangaika mitaani!

Mahujaji hata hivyo, wakapewa ahadi na Rais wa nchi, kuwa “watakwenda Hijja” na jitihada zote zitafanywa. Ikaundwa ‘taskforce’ ya kushughulikia hilo na hatimaye mahujaji si tu walisafirishwa bali pia kugharimiwa. Serikali ikawalipia tikezi bila kutaka mkopo na kumwaga mamilioni ya shilingi huko walikokwenda na kuwahudumia kwa kila namna.

Wenyewe (kama alivyosema Naibu Katibu Mkuu Omari Chambo) walikiita hicho ndicho “kifuta jasho”. Hata wakati wa kurudi, serikali si tu ilituma watu Saudi Arabia bali ilihakikisha hata matatizo ya ukosefu wa ‘slots’ au ndege usingezuia hivyo, wakashirikiana na serikali ya Saudia na hatimaye kuwarudisha mahujaji nyumbani. Rais Kikwete akatimiza ahadi yake kuwa mahujaji hawatapa matatizo yoyote yale wakati wa kurudi. Tukashukuru Mungu.

Hata hivyo katika mambo hayo mawili kuna kitu kimoja ni dhahiri. Serikali iliwabagua vijana wetu Ukraine na kuwapendelea mahujaji. Ni kwa nini basi? Kwanza jibu liko kwenye namba; vijana 29 si namba ya kumkosesha waziri mkuu au Rais usingizi ila mahujaji zaidi ya 300 kwa hakika waliwaumiza kichwa. Hivyo serikali haikutaka kusababisha manung'uniko makubwa kwenye jamii hii hasa ukizingatia familia zaidi ya mia tatu zilizokuwa na wasiwasi ukilinganisha na familia kama 30 tu. Hivyo serikali haikujali wanafunzi.

Pili ni suala la unyeti wa sakata lenyewe. Suala la mahujaji ni suala la imani wakati wanafunzi ni suala la elimu. Kwa wale waliopata nafasi ya kumsikiliza Sheikh Ponda Issa Ponda na baadhi ya viongozi wa dini walivyokuwa wanazungumza kuhusu “kufanya maandamano” serikali haikuwa tayari kukabili ghadhabu ya Waislamu hasa ukiwa na watu kama “mtafutwa” Ponda Issa Ponda.

Manung'uniko ya baadhi ya jumuiya za Waislamu yakaanza kuenea ambapo tetesi za “njama” zikaanza tena. Tayari kulikuwa na suala la Mahakama ya Kadhi na sasa sakata la Hijja kuibuka hakukuwa na mtu serikalini aliyetaka hilo litokee. La wanafunzi Ukraine halikuwasumbua sana kwani lilihusu “elimu tu” na siyo imani ya watu.

Jambo la tatu hata hivyo ni madai ya “undugunaizeshen” uliofanyika. Mitaani ikaanza kusikika kuwa kati ya watu waliokuwapo kwenye msafara wa hija ni baba mkwe wa Rais Kikwete pamoja na ndugu kadhaa wa viongozi wengine. Hadi hivi sasa serikali haikukana hilo na mimi ninaamini kwa ukimya wao wamelithibitisha.

Kama Rais Kikwete alitaka amani nyumbani hakuwa na ujanja isipokuwa kuingilia kati ama sivyo “kula hakuliki na kulala hakulaliki” pale Ikulu. Rais ilimbidi aingilie kati kumwepushia aibu na adha baba mkwe.

Kimsingi tulichoshuhudia ni kitendo cha ubaguzi wa wazi na upendeleo usio na sababu kwa mahujaji kuliko Watanzania wengine wanaopatwa matatizo wakati wa usafiri. Mbona wakati treni imekwama kutoka Kigoma kuja Dar kwa karibu wiki nzima hatukusikia waziri mkuu kenda kuwaangalia au mpango wa kifuta jasho au hata kununuliwa “kuku” wa Itigi na minofu ya Saranda? Ni lini sera ya “kifuta jasho” imeingizwa serikali wananchi wanapopata matatizo ya usafiri na kwanini ianzie kwa mahujaji? Je, kuanzia leo hii wananchi wanaotaka kusafiri na vyombo vya serikali na wakajikuta wanakwama kutokana na makosa ya vyombo hivyo watarajie kulipiwa hoteli, msosi, na kujikimu kwingine, kama sivyo kwa nini?

Kama serikali imeona kuwa ni lazima ijihusishe katika masuala ya namna hii na ya kuwa hata kama mtu akijipangia mambo yake ya binafsi ambayo yanahusisha kwa namna moja au nyingine “ahadi” ya serikali kuwa anastahili msaada basi serikali itangaze kuwasamehe mkopo wa tiketi vijana wetu waliorudi nyumbani toka Ukraine na kuwaomba radhi kwa kuwatelekeza, kuwasusa na kuwakatishia masomo yao kimabavu.

Fedha iliyotumika kuwagharimia mahujaji kwa karibu wiki tatu ingeweza kuwasomesha vijana wote 29 kwa karibu miaka yote iliyobakia! Kama serikali yetu inajali wananchi wake basi ikiri kutowatendea haki na ya kuwa hata wale ambao walikatishwa masomo na sasa wameshindwa kurudi shuleni basi wasamehewe na waahidiwe kuendelea na masomo mwaka huu bila kuumizwa na masharti mapya ya mikopo kama walivyofanyiwa sasa.

Vinginevyo, tulichoshuhudia kwenye sakata la wanafunzi Ukraine na mahujaji pale Kipawa ni matumizi mabaya ya madaraka na uonevu mkubwa kwa watu wasio na sauti. Sisi sote hatuwezi kuwa katika kundi moja na ndugu wa vigogo ili na sisi tupate neema!

Nisieleweke vibaya, tatizo langu si mahujaji kusaidiwa kwani mwenye njaa hana mwiko. Tatizo langu ni msingi wa kuamua kuwasaidia wao na kuwakatilia watu wengine kwenye matatizo kama hayo. Kwa nini serikali ilibagua hivyo? Kama nilivyosema hapo juu siamini msingi ni dini kwani katika kundi la wale wanafunzi asilimia kubwa walikuwa ni waislamu na si wote toka bara. Mmoja ni mtoto wa Shehe!

Serikali ya Rais Kikwete kwa kufanya kitendo hiki cha kibaguzi na upendeleo wa wazi imeonyesha udhaifu mkubwa wa kuongoza na matokeo yake ni kutengeneza kiwango kipya kabisa.

Kuanzia hivi sasa Watanzania wa madhehebu yoyote wakikwama Kipawa serikali lazima iingilie kati! Si kukwama Kipawa tu bali piwa wakikwama pale Relwe au kwenye vituo vingine vya kusafiria ambako chombo cha serikali kilitakiwa kuwasafirisha.

Si kuwasaidia usafiri tu, kuanzia sasa Watanzania wote wanayo haki ya kudai kulipiwa gharama ya chakula na malazi wanapokwamishwa na vyombo vya serikali! Vinginevyo, serikali itueleze kwanini mahujaji walipewa upendeleo?

Mwanakijiji:

Kuna posti ilikuwepo kwenye ukumbi wa biashara ukiimiza watanzania waanze kuthamini Made In Tanzania.

Matatizo yaliowatokea mahujaji yangeweza kutoa kundi lolote lile. Kwa mfano kombe la mataifa ya Africa limeanza na kama taifa star ingekuwepo kwenye mashindano hayo, je shirika la hili lingeweza kuchukua mashabiki wa soka wa Tanzania kwenda Ghana. Au ingebidi watanzania watumie Ethiopia Airline kwenda kwenye mashindano hayo?

Vilevile mwandishi wa hiyo makala anashindwa ku-connect dots. Kwa maoni yangu atakuwa wale old school ya Nyerere ya kuunganisha kila hasara na matumizi ya shule au Afya.

Upande mwingine unaonyesha kama ATC wangetumia msimu wa watu kwenda kuhiji wangeweza kupata faida. Na faida hiyo ingeweza kuliongezea taifa pato la kusomesha watu Ukraine na vile vile kuliendesha shirika lenyewe.

Mtu yoyote mwenye mawazo ya kibepari kama yangu angetumia nafasi hiyo kujipatia faida na mambo ya dini yangekaa pembeni. Na kwa mujibu wa mashirika ya ndege, ndege inapokwama, mmiliki inabidi aingie gharama za kuwasaidia wasafiri. Kwa kuwa serikali imeamua kuwa na udau wa 100% basi ni lazima gharama iingie. Na hayo sio mambo ya kidini bali ni ya biashara.

Katika kila nchi kuna makundi ya waislamu tofauti na yanakwenda kuhiji bila kupitia chombo kimoja. Kwanini waislamu wa Tanzania wapitie BAKWATA?

Kwa upande wangu naona tuna matatizo ya kiakili katika mambo ya biashara. Hata mashirika makubwa ya ndege yana msimu wa kupata faida. Na kwa shirika dogo kama la ATC kipindi cha watu kwenda kuhiji ni kizuri kwao kujipatia faida na sio kuangalia udini. Na kama kuna hasara iliyopatikana mwaka huu, basi ni lazima waendeshaji wa shirika wawajibike kama wafanya biashara na sio waumini wa dini.
 
Nakupa tano..jana nilipost kumjibu mwanakjj...ikatokea bahati mbaya Jamaa alieaminiwa na JF Admin akafanya uterrorism..kwa kufuta everything. so ntamjibu baadae mwanakjj mda huu nshachoka
 
mie sioni kosa lolotw la Makala /ya mwanakijiji,Mzee Mwanakijiji alikuwa najenga hoja,ni kwanini Serikali iliwafidia Waislamu wakati tatizo la Waisalma na /vijana wa Ukraine ni sawasawa.

tuache kujibu hoja kwa vioja.
 
Mimi namuunga mkono M.MK

Maana kama Rais ni rais wa watu wote sio kabila, dini au watu wachache, kama ni viongozi wa serikali ni wa watu wote.

Lakini kwa nini kundi fulani lipate upendeleo/kipaumbele lingine lipuuuziwe? Je huu ndio mwanzo wa udini? au Undugunisation? au Usisi?

Serikali tunaomba majibu
 
Ktk wale mahojaji- Mkwe wake JK alikuwepo! Mke wa JK alitia sana pressure JK to do something- na wote mnajua tena mama akikubana home- hapo home yaani yapakaliki!

JK alizidiwa na chagizo toka kwa Mama Salma- na akayeild down kama wanaume wengine!

This is the main reason!
 
Sasa mnatamani Mahujaji wasipendelewe. Mnataka wadhalilike? Bwana Yesu anasema umpende adui yako. Sijui kama nyinyi ni wafuasi wa Bwana Yesu?
 
Ktk wale mahojaji- Mkwe wake JK alikuwepo! Mke wa JK alitia sana pressure JK to do something- na wote mnajua tena mama akikubana home- hapo home yaani yapakaliki!

JK alizidiwa na chagizo toka kwa Mama Salma- na akayeild down kama wanaume wengine!

This is the main reason!

haya Mambi si hata Mwinyi yalishawahi kumtokea?Je tuwalaumu hawa Vionzoi wawili kwa sababu ya vivuli vyao vya dini yao?

siku na saa ya Maajabu inakuja hivi karibuni,
 
Mimi namuunga mkono M.MK

Maana kama Rais ni rais wa watu wote sio kabila, dini au watu wachache, kama ni viongozi wa serikali ni wa watu wote.

Lakini kwa nini kundi fulani lipate upendeleo/kipaumbele lingine lipuuuziwe? Je huu ndio mwanzo wa udini? au Undugunisation? au Usisi?

Serikali tunaomba majibu

Kuna thread katika ukumbi wa Uchumi ambayo inampa pongezi JK kwa kulianzisha tena ATC.

Katika thread hiyo nimetoa hoja kuwa ni makosa kwa serikali kufanya biashara lakini wachangiaji wengi waliona ni vizuri kwa serikali kuwa na shirika la kibiashara.

Serikali ya Tanzania inamiliki shirika hili kwa 100%. Na inawajibika kibiashara pale matatizo ya kibiashara yanapotokea ndani ya shirika hili.

Na kama mipango mizuri ingekuwepo na mahujaji kwenda bila matatizo, ni nani angepata faida? Ukweli ni kuwa serikali ingepata faida ya 100%.

Elimu ni huduma ya jamii na usafirishaji wa mahujaji ni biashara. Kwa mtu mwenye kutafuta chokochoko za kidini ataunganisha mambo haya katika kapu moja. Katika kusomesha wanafunzi Ukraine, serikali inatoa huduma. Kupeleka mahujaji serikali ilikuwa inafanya biashara tena ya faida lakini kutokana na mipango mibovu imepata hasara.

Katika matukio yote mawili serikali imechemsha. Na ukitaka kujadili matukia haya mawili ni lazima uangalie role gani serikali imecheza.
 
nyinyi msemeeni tu mwanakijiji lakini yeye deep inside anaelewa alikuwa anataka nini(siyo udini),na bila shaka anaelewa wazi kwamba alikosea ,kama anakataa na akanushe haya ninayoyasema.
 
Bahati Mbaya posting niliyojibu jana iliathirika kama zilivyoathirka posting zingine kutokana na mafisadi kufanya UKATILI juu ya JF.

1. Mwanakjj Hongera kwa ushupavu wako wa kutoa dukuduku lako kama ambavyo Wa-TZ wengine walivyo na haki ya kutoa yale yanayoikera jamii yao.

2. Pia Mwenzetu alietoa vitisho ni kumvumilia na ieleweke pia tunatofatiana kufikiri na uwezo wa kuchambua, msingi ni kuelewana na kuvumiliana ktk yale tunayotofautiana.

3. Binafsi mdogo wangu ni mmoja alieathirika na Suala la Ukraine. Suala Ukraine nilipinga na ntaendelea kulipinga kwa namna serikali ilivyo li Handle. Kwa namna ulivyofanya comparison analysis zako za Ukraine na Mahujaji ni vitu 2 tofauti na umekosa maeneo ya kuyaainisha!!! Ukraine ifananishe na 40% issue wa wanafunzi waliopo UDSM. Na vyuo vingine vya Bongo.

4. Mwanakjj umekusudia kuupotosha umma kwa makusudi kwa kusema eti idadi ya Mahujaj walikuwa zaid ya 300, wakati ukijua fika mahujaj walikuwa zaid ya 1000. Ndege ilifanya trip zaid ya Xtatu.Umefanya hivyo makusudi ili hesabu zako za ratio ziingie akilini, ukalazimisha wana Ukraine walikuwa 29, ukakadiria kufikia 30. Hapa si tu inapunguza credits juu ya muonekano wako ktk Jamii ya waTZ.

5. Naomba ieleweke kuwa Viongozi wa Serikali hawakwenda on purpose ya kuwafariji mahujaji, JK alikuwa ziarani kwenda US, so lazima atafungamana na kundi lake. EL Kama ilivyoripotiwa ktk news za tz, alifika kumsindikiza Bosi wake. So kuwaona na kuwafariji mahujaji ilikuwa ni coincidence.

6. Pia Hao viongozi wengine walokwenda kuwafariji mahujaji, pia si kwamba walikwenda eti tu kwakuwa ni mahujaji, bali walikwenda on the other reasons. Ieleweke pia baadhi ya wabunge na viongozi wa mbalimbali wa serikali walikuwa ziarani kwenda Hijja, pia Meya wa Kinondoni Salum Londa nae alikuwepo so kuna watu kama marafiki, majirani au wengine ni bosi wao ilibidi tu waende, in that sense nao wakakutana na mahujaji.ni sawa nawe Mkjj amekuja Ndugu au Jamaa ako US kukuvisit, ikatokea bahati mbaya kakwama usafiri, itabidi kila mara umjulie hali kujua safari ikoje.

7. Pia ieleweke pia si ATCL wala Serikali iliyogharamia chakula pale airport wala kule Makka/Madina. Mahujaji walipewa chakula na ndugu zao, Jamaa zao, wasamaria wema na wengine walitoa pesa zao mfukoni. Hii kwa mujibu wa taarifa za magazeti na mahujaji. Kama una ripoti ya serikali kuwa imegharamia hilo, please tupe….(Muulize Muhibu Said wa Mwananchi)

8. Kuhusu KIFUTA JASHO. Mwanakjj kama umesafiri na shirika lolote kubwa duniani eg Kenya airways , basi Ndege ikichelewa zaid ya masaa 2-4 basi lazima abiria mpewe chakula, na kama ikichelewa siku nzima basi malazi na chakula lazima mpewe, sometimes na pesa mnapewa kutegemea na situationa na aina ya ndege. Waulize jamaa zako wanaokwenda lagos/Dubai/India wakakwama na Kenya airways watakuambia. La Kifuta jasho lazima lifanyike, na kama halitofanyika Mahujaj watakuwa wameonewa.

9. Pia ieleweka pia Safari za Mahujaji ni kipindi cha kufanya biashara kwa mashirika ya Ndege. ATCL walijuwa seasons hizo ni za kutengeneza pesa. Ni Kanuni za biashara Mwanakjj, wakati kristmas weka Miti ya kristmas utakula pesa. (Soma markerting skills, ujue seasons zinavyofanya kazi ktk business). Kama ilivyo business zingine zinakuwa na Profit n LOSS.(ATCL watajiju ktk Business Forecasting zao kama walipata P/L) Mahujaji walilipia FULL amount as per agreement. Unless ATCL wangesema pesa walopewa haikuwa sahihi. Serikali HAIKUWAPENDELEA Mahujaji, bali walikuwa wakifaciliate shirika lake lisije kufilisiwa. Kumbuka ndo maana wakasema mahujaji wakirudi watawaomba wasiende mahakamani. Kama mahujaji wangeenda mahakamani na waje majaji wa kutoka huko kwako US..jua ATCL ingekuwa ktk financial budden kubwa.

10. Bin Maryam naona kakujibu mengine…please tosheka na hayo…
 
Upande mwingine unaonyesha kama ATC wangetumia msimu wa watu kwenda kuhiji wangeweza kupata faida. Na faida hiyo ingeweza kuliongezea taifa pato la kusomesha watu Ukraine na vile vile kuliendesha shirika lenyewe.

Mtu yoyote mwenye mawazo ya kibepari kama yangu angetumia nafasi hiyo kujipatia faida na mambo ya dini yangekaa pembeni. Na kwa mujibu wa mashirika ya ndege, ndege inapokwama, mmiliki inabidi aingie gharama za kuwasaidia wasafiri. Kwa kuwa serikali imeamua kuwa na udau wa 100&#37; basi ni lazima gharama iingie. Na hayo sio mambo ya kidini bali ni ya biashara.

1. ATC kama shirika waliona kuwa hawana uwezo wa kuhudumia mahujaji isipokuwa mwenyekiti wa bodi ambaye hakupenda kuwaangusha mahujaji kwa vile ni mwenzao ndiye alilazimisha shirika kubeba mzigo huo. Hii imesemwa na wahusika wenyewe. Walisema kwamba walimwamini mwenyekiti kwa sababu hata alipokuwa balozi alikuwa anawasaidia. Huu uamuzi haukufanyika kibiashara bali kwa kufahamiana. Katika biashara yeyote yule anayenunua huduma anawajibika kufanya due diligence kujihakikishia kuwa yule ambaye anayeingia naye mkataba anauwezo wa kumsafirisha kwa bei na wakati muafaka KABLA ya kuingia naye mkataba. Anayetaka pesa yako atakuambia lolote ili aipate, ni wewe unayewajibika kuhakikisha kuwa pesa yako haitapotea na kujiwekea kinga katika mkataba ili pale atakaposhindwa una njia mbadala ya kurudishiwa pesa zako. Katika mikataba ya ujenzi huwa mkandarasi ana submit bond kutoka benki kuhakikisha kuwa pindi atakaposhindwa kutekeleza, mshitiri anakuwa na mahali pa kukata. Kwenye mikataba kama hii, ambako mtu unanua package, mshitiri anaweza akadai mkataba wa pekee au akakta bima ili likitokea lolote asipate hasara jumla. Hamna uzalendo, udini n.k. kwenye biashara.

2. Hapo zamani, pengine kabla haujazaliwa palikuwa na shirika la ndege maarufu sana likiitwa Swiss Air lilokuwa likimilikiwa na serikali moja tajiri sana duniani, nchi ya Uswisi. Shirika lilipoboronga serikali ililiacha likafa. Hakuna cha uzalendo. Ukicheleweshwa na Kenya Airways, British Airways au KLM hautasikia serikali za Kenya, Uingereza au Netherlands zikiingilia kusaidia. Na ukiudhiwa sana unachoweza kufanya ni kushitaki mashirika yenyewe na siyo serikali ambazo ndiyo wadau wakuu wa mashirika haya. Kama nilivyosema awali, ukiilipa tanesco nao wakachelewa kukuunganishia umeme hauendi serikalini kusema ati kwa vile tanesco wameshindwa basi Wizara ya nishati ikuunganishie. La hasha, unakula sahani moja na Tanesco hadi haki yako uipate. Ukiwapeleka mahakamani na ukashinda kesi, kama tanesco hawana uwezo wa kukulipa ni mali ya Tanesco itakayokamatwa na si mali za serikali kuu. Mahujaji walikuwa na kila haki kushitaki ATC na kudai fidia kwa yale yote yaliowatokea. sasa ndugu zangu mnataka kuniambia kwa vile mdau mkubwa wa ATC ni serikali, basi wale mahujaji ambao hawataridhika na hatua zilizochukuliwa waishitaki serikali kudai fidia huku waliingia mkataba na ATC?

3. Serikali ilijiingiza kwenye hili ili kuwanusuru raia wake na sidhani kama itakuwa busara kudai kuwa ulikuwa ni wajibu wake kama mdau wa ATC. Inabidi ishukuriwe kwa kufanya ubinadamu na si kuwabeza ati waliwajibika. Ingekuwa hivyo basi pangekuwa na fungu la kusafirisha mahujaji kwenye bajeti yake!
 
2. Pia Mwenzetu alietoa vitisho ni kumvumilia na ieleweke pia tunatofatiana kufikiri na uwezo wa kuchambua, msingi ni kuelewana na kuvumiliana ktk yale tunayotofautiana.

Hapana Mkuu! Hamna cha kuvumilia matusi na vitisho kama alivyotoa mwandishi. Kibao kingegeuzwa sasa hizi mngeisha mtangazia Fatwa na kumsomea Al badir! Vitendo kama hivi vinabidi vikemewe kwa sauti ya juu kila vinapotokea ili visitufikishe kule waliko jirani zetu. Na inakuwa vyema wale ambao anadhani anawasemea mkimweleza kama alivyofanya Mtoto wa Mkulima in "no uncertain terms" kwamba hawazungumzii. Hastahili kutetewa kwa njia yeyote. Kigugumizi kinatoka wapi?
 
1. ATC kama shirika waliona kuwa hawana uwezo wa kuhudumia mahujaji isipokuwa mwenyekiti wa bodi ambaye hakupenda kuwaangusha mahujaji kwa vile ni mwenzao ndiye alilazimisha shirika kubeba mzigo huo. Hii imesemwa na wahusika wenyewe. Walisema kwamba walimwamini mwenyekiti kwa sababu hata alipokuwa balozi alikuwa anawasaidia. Huu uamuzi haukufanyika kibiashara bali kwa kufahamiana. Katika biashara yeyote yule anayenunua huduma anawajibika kufanya due diligence kujihakikishia kuwa yule ambaye anayeingia naye mkataba anauwezo wa kumsafirisha kwa bei na wakati muafaka KABLA ya kuingia naye mkataba. Anayetaka pesa yako atakuambia lolote ili aipate, ni wewe unayewajibika kuhakikisha kuwa pesa yako haitapotea na kujiwekea kinga katika mkataba ili pale atakaposhindwa una njia mbadala ya kurudishiwa pesa zako. Katika mikataba ya ujenzi huwa mkandarasi ana submit bond kutoka benki kuhakikisha kuwa pindi atakaposhindwa kutekeleza, mshitiri anakuwa na mahali pa kukata. Kwenye mikataba kama hii, ambako mtu unanua package, mshitiri anaweza akadai mkataba wa pekee au akakta bima ili likitokea lolote asipate hasara jumla. Hamna uzalendo, udini n.k. kwenye biashara.

2. Hapo zamani, pengine kabla haujazaliwa palikuwa na shirika la ndege maarufu sana likiitwa Swiss Air lilokuwa likimilikiwa na serikali moja tajiri sana duniani, nchi ya Uswisi. Shirika lilipoboronga serikali ililiacha likafa. Hakuna cha uzalendo. Ukicheleweshwa na Kenya Airways, British Airways au KLM hautasikia serikali za Kenya, Uingereza au Netherlands zikiingilia kusaidia. Na ukiudhiwa sana unachoweza kufanya ni kushitaki mashirika yenyewe na siyo serikali ambazo ndiyo wadau wakuu wa mashirika haya. Kama nilivyosema awali, ukiilipa tanesco nao wakachelewa kukuunganishia umeme hauendi serikalini kusema ati kwa vile tanesco wameshindwa basi Wizara ya nishati ikuunganishie. La hasha, unakula sahani moja na Tanesco hadi haki yako uipate. Ukiwapeleka mahakamani na ukashinda kesi, kama tanesco hawana uwezo wa kukulipa ni mali ya Tanesco itakayokamatwa na si mali za serikali kuu. Mahujaji walikuwa na kila haki kushitaki ATC na kudai fidia kwa yale yote yaliowatokea. sasa ndugu zangu mnataka kuniambia kwa vile mdau mkubwa wa ATC ni serikali, basi wale mahujaji ambao hawataridhika na hatua zilizochukuliwa waishitaki serikali kudai fidia huku waliingia mkataba na ATC?

3. Serikali ilijiingiza kwenye hili ili kuwanusuru raia wake na sidhani kama itakuwa busara kudai kuwa ulikuwa ni wajibu wake kama mdau wa ATC. Inabidi ishukuriwe kwa kufanya ubinadamu na si kuwabeza ati waliwajibika. Ingekuwa hivyo basi pangekuwa na fungu la kusafirisha mahujaji kwenye bajeti yake!

Fundi Mchundo:

Naona mjadala mzima unakuwa kama wa Mama Meghji kudai kuwa alikuwa duped na Balali, wakati yeye ana mamlaka ya kisheria ya kutoa maamuzi.

Sasa wakurugenzi wa ATC walilazimishwa na mwenyekiti wao. Kwa ujumla watanzania hamjui biashara wala kujiongoza. Yanapotokea matatizo mnaanza kuonyeshana vidole vya udini na ukabila.

Ngoja nisikilize zilipendwa.
 
Fundi Mchundo Hawajui Hatujui Biashar????teehteeh Am Ki,,,,
Je Wahusika Wamefanywa Nini Bada Ya Kuliingizia Hasara Kamouni Hili Ndio Tujiulize Zaidi ,,alali Kaanza Mwenyewe Hawa Je ????nasikia Wakaweka Hadi Na Ofisi Zao Atcl..toka Lini Mwenyekiti Wa Bodi Akawa Na Ofisi Kwenye Mlo.....wengine Watakula Wapi Kila Kona Anataka Aone ...ona Sasa Haya Yamemtokea Puani..."""nchachema Chichemi Tena""""
 
3. Serikali ilijiingiza kwenye hili ili kuwanusuru raia wake na sidhani kama itakuwa busara kudai kuwa ulikuwa ni wajibu wake kama mdau wa ATC. Inabidi ishukuriwe kwa kufanya ubinadamu na si kuwabeza ati waliwajibika. Ingekuwa hivyo basi pangekuwa na fungu la kusafirisha mahujaji kwenye bajeti yake![/FONT]

wakati nikiipinga serikali kwa kitendo ilichowafanyia wanafunzi kule Ukraine ninaungana na wewe pale unaposema Serikali ishukuriwe. tofauti na mwandishi wa makala hii ndugu Mwanakijiji anayeilaumu serikali eti kwa nini imesaidia mahujaji!.huku akitoa mifano kedekede ya kwamba KAMA SERIKALI ILIWATELEKEZA WANAFUNZI KWA NINI ISIWATELEKEZE NA MAHUJAJI?, utadhani kwamba yeye mwanakijiji angefurahi kwelikweli kama serikali ingewatelekeza mahujaji pia, au kwa mtazamo wa ndugu mwanakijiji ni kwamba KWA KUWATELEKEZA MAHUJAJI BASI SERIKALI KAMA ILIVYOWATELEKEZA WANAFUNZI UKRAINE BASI SERIKALI INGEKUWA IMETENDA HAKI KWELIKWELI!!.

mimi ninasema Mwanakijiji yupo wrong kwa sababu KUKOSEA MARA MOJA AU MARA KADHAA KWA SERIKALI SI SABABU YA KUKOSEA TENA.kwa hiyo wale wanaotaka serikali ikosee tena katika ishu ya mahujaji eti tu kwa sababu ilikosea na inakoseaga mimi wananishangaza .

Pili Serikali imepatia kwa sababu hii, iwapo mahujaji wangeishitaki ATC ni dhahiri hii kesi ingeigarimu ATC pesa kibao,na ni wazi kwamba ingelazimika kulipa fidia ya mabilioni ya shilingi. sasa kwa shirika linalojikongoja kama ATC ni dhahiri lingeyumba, na lingepoteza credibility kibiashara both internally na internationaly.sasa hebu niambieni SERIKALI yetu ambayo imeingia gharama kulifufua shirika hili ilikuwa tayari kuona haya yanatokea?.kumbuka ATC siyo kama Swiss AIR au hata Ethiopias Airline, hii ni ATC masikini ambayo hata kutembea haijaanza inatambaa halafu mnadhani inaweza kujitegemea bila mkono wa serikali.

Tatu hii ni diplomatic disaster walikuwemo watu wa mataifa mengine mle miongoni mwa mahujaji, ilikuwa ni lazima serikali kuingilia kati,na imeingilia kati kwa hiyo bila shaka serikali IMEPATIA.

nne hii pointi ni ya kutufanya tu tufikiri, iwapo serikali inaitaka serikali ya uingereza iturudishie chetu eti kwa kuwa BAE ni kampuni ya uingereza, kwa nini basi serikali yetu isiwe tayari kwenda kurekebisha mambo pale moja ya mashirika yetu machanga yanapokosea?. thats why NAIUUNGA MKONO SERIKALI KWA HTUA ZOTE ILIZOCHUKUA KUHAKIKISHA MAHUJAJI WANAENDA MAKKA KUHUJI.

tano ninadhani tunapoandika au kusema vitu ni vizuri vikawa ni vya kweli au necessary,kuandika vitu kwa sababu vinasound good bila kuangalia impact ya vitu hivyo nadhani hata waanzilishi wa freedom of speech hawakukusudia hivyo unless otherwise wawe na ajenda ya siri!
 
Nadhani kinacho ibua hoja, ni kuwa serikali haijawahi kukubali kwamba imekosea kwa kutowasaidia wengine?, kwahiyo inapotekea ikaibuka na kusaidia sehemu fulani, lazima maswali kama haya yaibuke!

Ndo maaana nami naona kama serikali imezinduka sasa nakuona wajibu wake wa kusaidia wananchi wake, isiishie hapa, iende mbele na kuwasaidia wengine kwa mfanao kama hao vijana wa ukrane walivo elezewa, isiwadai tiketi, na ihakikishe wanasoma!! Ama la hisia za kwamba huu ni upendeleo zipo na ni za haki!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom