Lifahamu kanisa halisi Kigoma na hija zake mkoani Kigoma

Phamarcist

JF-Expert Member
Apr 18, 2021
211
449
Habari za wakati?

Siku ya jana na leo yaani tarehe 30 na 31, mkoa wa kigoma umefurika wageni wengi kiasi cha kujaza karibia 90% ya nyumba za kulala wageni.

Baada ya kufuatilia ndipo nilipogundua kuwa wageni hao ni mahujaji wa kanisa HALISI, kanisa pekee lililoasisiwa nchini Tanzania huku likiwa na waumini kutoka pande zote duniani ikiwemo mataifa kama Marekani, Congo, Malawi msumbiji nk.

Mkuu wa kanisa hili anajulikana kama BABA HALISI huku Mrs akiitwa MAMA HALISI.

Kwanini hija za kanisa hili hufanyikia mkoani kigoma?

Kwa mujibu wa watu Wachache niliofanikiwa kuwauliza swali hili, walidai kwamba, tumekuja kushukuru Utimilifu wa Matahayo 21:43 katika ule mstari Bwana Yesu zaidi ya miaka 2000 baada ya Wayahudi kumkataa alisema Ufalme utahama kutoka Mashariki ya Kati kwenda Taifa lingine ambalo kwa wakati ule hakulitaja. Sasa baada ya Sauti kusikika mara nne hapa Kigoma, tumejua kumbe Taifa lenyewe ni Tanzania.

Kwa mujibu wa KANISA HALISI mungu huitwa chanzo halisi na Salam yao kuu ni "Heri Heri"

Hayo ni machache niliyong'amua siku ya jana kuhusu kanisa halisi, Kama yupo muumini au yeyote anayejua zaidi namkaribisha kwa kutuhabarisha zaidi asanteni.
 
Chuma ya BABA HALISI
IMG_0305.JPG
 
Nikipata nafasi ya kuwa kama Baba na Mama Halisi..ni mwendo huo huo.Duniani kwenyewe tunakaa miaka 70
 
Nyakati za mwisho
Nyakati za mwisho Bado mkuu, hiki kipindi kinaitwa enlightenment ambacho wenzetu Europe walipata toka 1680's na sisi ndio tunakipitia sahivi. Hii inaonyesha ni kwa namna gani bado tupo nyuma ya muda.
 
Back
Top Bottom