Kwanini Magufuli hawezi kuwa na mafanikio

Kwanini Magufuli hawezi kuwa na mafanikio

VISIONARY LEADERS,hili neno nimeanza kulisikia kwa muheshimiwa Edward Lowasa.
Niseme wazi tu kwamba kabla ya kuligoogle(mtanisamehe kiswahili nacho kigumu)kwa mawazo yangu yakanipeleka kwa viongozi mfano wa Mwl J.k.Nyerere,wakina Mao Tse-Dong,wakina Kwame Nkrumah,Muammar Gaddafi na wengine wengi.
Lakini baada ya utafiti mdogo,kwanza nimegungua Afrika hatuna viongozi wa Caliber hii kwa sasa na kama wapo ni wachache sana,kwa mawazo yangu hawa ndio walifaa kuitwa VISIONARY LEADERS kwasababu walikuwa na maono mengi ikiwa ni pamoja na sio tu kutaka kuzikwamua nchi zao kiuchumi,kisiasa, bali na nchi nyingine marafiki na walikuwa na OVERPOWER kwa baadhi labda niseme hivyo,kwamba wakisema wamesema.
Wao ndio walikuwa waamuzi wa mwisho kwamba nchi itoke wapi iende wapi?nadhani uendeshaji huo wa nchi ulikuwa unapingana na mambo ya democracy kama tunayoyaona sasa.
Lakini kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kumbe VISIONARY LEADERS ni caliber ya akina Steve Jobs,Albert Einstein,the Wright Brothers na wengine ambao kimsingi mimi nawaweka kwenye kundi la WAVUMBUZI na hizi ni baadhi ya sifa za visionary leaders,Openness,imagination,persistence,and conviction.
Sasa kwasisi wengine tujitafakari kujua kama hapa kwetu Tanzania tunao hao Visionary Leaders kweli?Mtanisaidia nilipokosea.
 
Sjasoma hoja yako, ila aise wakati unaandika na mimi nilitaka kuja na hoja kama hiyo, ila kwa ufupi Rais wetu, hana vission, he is not a visionary leader.ili ni kosa kubwa ndio maana anataka wakuu wa mikoa wafanye kazi, kira kona watui wafanye kazi paspokujua kuwa watu hawna kazi je wanafanya nini? je kuiba ni kazi watu wote waibe? ndio maana yeye kama yeye ukimuuliza vision yake inamtaka atoe ajira kiasi gani jawezi kutajia? viwanda vingapi unataka kuvijenga ? utavijengaje? lakini anakwambia atavijenga, bnafsi nilipenda Lowasa awe raisi wa nchi hii, alafu Magufuli awe Wazir mkuu, nakwakbieni nchi hii ndani nya miaka mitano ingeitwa dependent Bajet country. ni hayo tu
Hoja yangu ni kile ulichoandika hapa kwamba,raisi anatakiwa kuwa na plan na dira kama ulivyosema na pia katiba mpya ambayo itakayotoa dira kwa nchi mpya,sheria na utekelezaji.

Nimejaribu kuandika na kuwa too general huku nikishika kitu kimoja kimoja ila kutotaka kuchosha watu kusoma inabidi kuandika kwa kifupi huku ukiwa na genera idea and the rest can unfold into discussions thats why we having a forum
 
Habari wanaJamii,

Mafanikio katika kazi na maisha mara nyingi hayaji kwa kusema tu,bali kuingia kazini na kufanya kazi kwa akili na nguvu zote.Mafanikio baina ya watu au kitu hayawezi kulinganishwa,bali tunaweza kuangalia hatua na mwelekeo wa jambo hilo kutokana na kuwa tumetofautiana katika mafikiri,maono,resources na hata wale wanaokuzunguka.

Katika uongozi wa nchi,mafanikio hayaji kwa maamuzi ya raisi mwneye bali ushawishi wake kwa kile anachoamini akishirikiana na washauri na wataalumu katika ujuzi wa jambo.

Kwanini nasema Magufuli hawezi kufanikiwa?Awali,ikumbukwe mimi napenda kazi anazofanya raisi katika kupunguza matumizi,rushwa nk.Lakini je akimaliza awamu yake yeye,Tanzania haiwezi kurudi kwenyewe pale alipokuta?

Lazima tukubaliane kuwa sasa ni wakati wa kwenda mbele.Vietnam,south korea na nchi nyingi zilizotuacha, hazjafika hapo kwa maneno na siasa.Wamefika hapo kwa kujituma na kufanya kazi lakini kubwa Zaidi ni mfumo thabiti na sheria zilizotungwa kunufaisha nchi.

Hii leo,wako wanaopinga katiba ya warioba ambayo imeelezea na wananchi wameafiki.Tumekuwa tukitunga sheria za kuwanufaisha wakubwa na wale wanaofanya kazi serikalini;huu ni wakati wa wananchi watanzania kufaidika na kuwa na fahari na nchi yao.

Namshauri raisi kwanza aangalie mzigo na utitiri wa viongozi wandamizi kwenye serikali yake.Ukuu wa wilaya,mkoa na vyeo vingi wasomaji mnavijua.

Rais Magufuli bado anaamini kuwa anaweza kuongoza nchi kwa njia zile zile watanguliz wake walipopita na tukafanikiwa,hili naliona ni usingizi wa mchana.

Namshari raisi Magufuli awe kama maraisi waliotokea na kuunda mifumo, mfano,raisi wa marekani Raisi Roosevelt,Reagan na weingine ambao ndio walioweka misingi mikuu ya taifa la marekani na kuwafikisha hapo waliopo.Magufuli,anahitaji kuwa na maono hata kama uraisi ni wakupewa.

Lazima ifike wakati tuwe na maono na ndoto ni wapi tunataka kwenda,huku tukikumbuka wapi tunatoka.Raisi usiwe mwoga kufanya maamuzi na mapinduzi ya uchumi.Kwa mwendo huu na yale unayoaamini,na kasi hii uliyoipa jina "Hapa Kazi tu" ni sawa na usingizi wa mchana wa maskini aliyeshiba ugali na maharagwe.

Ingesaidia badala ya kulalama, ungewainisha mapendekezo yako. Bado una fursa.
 
Nchi haitajengwa na magamba, kazi yao ni kitafuta mianya ya ufisadi. Apunguze vijembe kwa wapinzani taifa liwe moja.
 
Lucifer ana msimano (consistency)..ninyi hamueleweki.....CCM wote hawafai ni akili ndogo mara mnaazima akili ndogo kuwasaidia kuingia ikulu.....
Ukiweza kuazima akili ndogo ukaingia ikulu, akiliyako siyo ndogo!
 
True day,i support everything....toka magufuli mh aingie madarakani ma critical thinker wamepungua mara 10,000 sioni uwezo tena wa watu kuchambua mambo Kwa kina...but hua nafurahia sana napokutana na post kama hizi komavu
 
Tatizo lako kama ilivyo kwa wapinzani wengiwao ni haraka. Roma haikujengwa kwa siku moja. Amekuta hali mbaya na anatengeneza mazingira rafiki ili aweze kutimiza aliyoahidi. Tulieni kinyozi afanye kazi yake. Tutapendeza tu. Mpeni muda.
 
Tatizo lako kama ilivyo kwa wapinzani wengiwao ni haraka. Roma haikujengwa kwa siku moja. Amekuta hali mbaya na anatengeneza mazingira rafiki ili aweze kutimiza aliyoahidi. Tulieni kinyozi afanye kazi yake. Tutapendeza tu. Mpeni muda.
Kinyozi anayekwambia uokote nywele zako kabla hajaanza kukunyoa? Au kinyozi yupi? Mm nilikua natarajia atawakamata hawa vijana wasio na kazi mtaani kiwapeleka kwenye training za kuendesha viwanda. Maana aliahidi Tanzania ya viwanda Chini ya magufuli
 
Mkuu naona amepoteza na anaongoza dola bila kuzingatia vipaombele , kila kitu anataka kufanya katika mda mmoja
Na bila vipaumbele atakua ana cheza makida nchi haiendeshwi na MTU mmoja inahtaji ushirikiano wa kitaasisi sasa yeye kufanya yote mwenyewe ka kiranja mkuu yatamshinda. Bila kuwa na taasisi imara atapoteza mda wake bure
 
..OK.

..tusubiri kwa muda gani?

..when do you think itakuwa wakati muwafaka/sahihi kuanza kumpima Raisi wetu kama anafanikiwa au anaboronga?
Umeambiwa Roma haikujengwa kwa siku moja. Uwe na subira na uishi kwa matumaini usikate tamaa mapema hivi!
 
Magufuli ana nia ya dhati sana kuhusu Tanzania lakni sio presidential material. Magufuli angefaa kuwa waziri mkuu.
Pendekeza wabadilishane na Majaliwa kama JPM hafai kuwa Rais! Watanzania wengi wamemtaka awe Rais wao ingawaje wewe siyo mmoja wao!
 
Back
Top Bottom