aminiusiamini
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,577
- 2,221
Habari wanaJamii,
Mafanikio katika kazi na maisha mara nyingi hayaji kwa kusema tu,bali kuingia kazini na kufanya kazi kwa akili na nguvu zote.Mafanikio baina ya watu au kitu hayawezi kulinganishwa,bali tunaweza kuangalia hatua na mwelekeo wa jambo hilo kutokana na kuwa tumetofautiana katika mafikiri,maono,resources na hata wale wanaokuzunguka.
Katika uongozi wa nchi,mafanikio hayaji kwa maamuzi ya raisi mwneye bali ushawishi wake kwa kile anachoamini akishirikiana na washauri na wataalumu katika ujuzi wa jambo.
Kwanini nasema Magufuli hawezi kufanikiwa?Awali,ikumbukwe mimi napenda kazi anazofanya raisi katika kupunguza matumizi,rushwa nk.Lakini je akimaliza awamu yake yeye,Tanzania haiwezi kurudi kwenyewe pale alipokuta?
Lazima tukubaliane kuwa sasa ni wakati wa kwenda mbele.Vietnam,south korea na nchi nyingi zilizotuacha, hazjafika hapo kwa maneno na siasa.Wamefika hapo kwa kujituma na kufanya kazi lakini kubwa Zaidi ni mfumo thabiti na sheria zilizotungwa kunufaisha nchi.
Hii leo,wako wanaopinga katiba ya warioba ambayo imeelezea na wananchi wameafiki.Tumekuwa tukitunga sheria za kuwanufaisha wakubwa na wale wanaofanya kazi serikalini;huu ni wakati wa wananchi watanzania kufaidika na kuwa na fahari na nchi yao.
Namshauri raisi kwanza aangalie mzigo na utitiri wa viongozi wandamizi kwenye serikali yake.Ukuu wa wilaya,mkoa na vyeo vingi wasomaji mnavijua.
Rais Magufuli bado anaamini kuwa anaweza kuongoza nchi kwa njia zile zile watanguliz wake walipopita na tukafanikiwa,hili naliona ni usingizi wa mchana.
Namshari raisi Magufuli awe kama maraisi waliotokea na kuunda mifumo, mfano,raisi wa marekani Raisi Roosevelt,Reagan na weingine ambao ndio walioweka misingi mikuu ya taifa la marekani na kuwafikisha hapo waliopo.Magufuli,anahitaji kuwa na maono hata kama uraisi ni wakupewa.
Lazima ifike wakati tuwe na maono na ndoto ni wapi tunataka kwenda,huku tukikumbuka wapi tunatoka.Raisi usiwe mwoga kufanya maamuzi na mapinduzi ya uchumi.Kwa mwendo huu na yale unayoaamini,na kasi hii uliyoipa jina "Hapa Kazi tu" ni sawa na usingizi wa mchana wa maskini aliyeshiba ugali na maharagwe.