Kwanini Magufuli hawezi kuwa na mafanikio

Kwanini Magufuli hawezi kuwa na mafanikio

Mbona hamkwisi kutapatapa!!! Unapewa supu unataka na pera!!Tulia maana huna hata moja ulilolieleza hapo.. na tatizo lako kubwa unaruka ndani ya elevator...Tulieni njooni na mawazo ya kujenga na hata kukosoa basi ukosoe ya msingi..Utajazaje maji kwenye ndoo iliyotoboka?

Huyo mkuu wenu wa maono mbona yeye aliendesha kwa ujanja ujanja mpaka yakamkuta japo mnasema Mkwere alimponza.. mwnye maono haponzi kamweeee...!!
 
..OK.

..tusubiri kwa muda gani?

..when do you think itakuwa wakati muwafaka/sahihi kuanza kumpima Raisi wetu kama anafanikiwa au anaboronga?

Soma kwanza historia za nchi zilizo endelea ambao walikua maskini hapo awali ndio utapata majibu. Tatizo la watanzania ni wavivu wa kusoma na kutafuta njia badala ni mahodari wa kuandika na kulalamika.
Ebu jiulize katika historia yako ndogo uliokuanayo je ilisha wahi kutokea kazi na mwendo kama huu hapa tanzania? Hata afrika nzima ukiacha afrika kusini? Leo hii mnawekewa kila kitu wazi, hadi mapato na matumizi ya kodi lakini bado tunalalamina. Au bora basi Magufuli nae angejilia zake tu kwa mrija ndio mgefurahi. Uwazi upo kwamba serikali zilizopita ziliadhiri nchi sana
 
Sikiliza ndugu Rais yeyote anapoingia madarakani anakuwa na strategies ambazo anatakiwa kuanza kuzitekeleza immediately baada ya kuingia madarakani.

Kimsingi masuala ya mabadiliko ya 'kimfumo', 'kikatiba' na kufuta unnecessary posts ni mambo ya kufanyika mapema sana sio kusubiri mwezi wa 39 katika 60.
Sawa, kila rais anakuwa na strategies zake kufuatana na mazingira ya nchi yake. Kamwe strategies za nchi tofauti haziwezi kuwa sawa. Hapa kwetu JPM ameona aanze na stratetigies zake nasi wananchi tunamfurahia. Hizo za kwako zisubiri rais atakayetoka ukawa.
 
Hakuna sehemu nimetaja ukawa wala ccm ila wewe unaleta akili premature
 
muda upi?wakati muda ndio unazidi kuyoyoma?
Watanzania ni wepesi kudanganyika, tujiulize mda alipokuwa mbunge wa Chato, jimbo lake limepata maendeleo gani zaidi ya kulazimisha barabara ya kuu ipite nyumbani kwake? Maendeleo katika jamii yeyote hayajawahi kuletwa na mtu au kikundi cha watu, bali ni muafaka wa kijamii unakubaliwa na wote na kushirikisha wote. Katiba ya wananchi ingekuwa muarobainina sio katiba ya Chenge
 
Mimi nilifikiri utakuja na hayo maono kwamba nini kifanyike, badala ya hiki anachofanya RAIS, ungesema maono yako kwamba afanyeje? Kipi kianze kipi aache lakini hamna kitu ni kulalamika tu, kama huna mchango wa nini ungetaka RAIS afanye ni bora umwache afanye kwa utaratibu anaoona yeye unafaa na sio kuwa mtabiri wa kumwombea asifanikiwe.
 
Namuunga Magufuli kwa vitu vingi ila ana kauli kadhaa ambazo zinaweza leta matatizo kwa wananchi ambao ni innocent.

Mfano yeye kuwapa ruhusa viongozi wengine ati watupe watu jela anytime kama kuna mistake wataifix baadaye, this is plain stupid and very dangerous. Watu innocent wengi tu wataumia kwa hili, baadaye uchunguzi unafanyika wanarudishwa huku wameishasota ndani muda mrefu shughuli zimesimama, hakuna compensation hakuna nini.
Hii ina tofauti gani na dictatorship?

Rais ameonyesha kua ana moyo wa kuibadilsha nchi lakini inabidi akubali kua sheria zipo ili zifatwe na ndio hizo sheria zilizotupa amani hadi leo hii, akianza kuwapa watu nguvu wabend hizi sheria ndipo tunapoanza kufa kifo cha polepole bila kujua, ni kama cancer.

Inabidi asimame aangalie ajue kua wapo wataalamu wengi kwenye nchi hii, asifanye neno lake kua final, anaongoza watu 50M inabidi atumie vichwa vingi kufikiria na sio kimoja tu na watu wanne watano walio karibu yake. Any wrong decision inaweza ikaturudishwa mwanzo au hata kwenye a much worse situation.

Mi nafikiria viongozi wengi walio chini yake wanafata kasi yake kwa kijinga, wapo ignorants wengi ambao wanafanya kazi tu ovyo bila hata kufikiria mara mbili au kufanya research, yaani mtu kasikia rumors fasta anaita waandishi wa habari waende kufukuza watu kazi, na watanzania dunia nzima wanashangilia, tuna madaktari wachache sana tanzania, tukipunguza hata 100 hapo ni wagonjwa zaidi ya 10,000 hawana pa kwenda.

Watanzania wengi naona bado hatujui tunachotaka,mimi nafikiri tulihitaji RAIS dikteta zaidi kuliko hata anavyofanya huyu tulienae sasa lakini mwenye nia ya kuipeleka nchi mbele.
Sheria zimefatwa sana huko nyuma lakini matokeo yake yako wazi,walioiba kuku wengi wapo ndani walioifisadi nchi hii ndio wanaitwa mashujaa na tunawaamini kiasi cha kutaka kuwapa nchi kweli?
kama kuwasikiliza wataalam wamesikilizwa sana lakini wametufikisha wapi na michakato isiyokwisha na 10% kwenye miradi mbalimbali?
kuhusu kufukuzwa watu kazi inasaidia kuwafanya watu wajue kazi ni dhamana kwamba sio zao na familia zao,watu walifanya utumishi serikalini kama zao hawakuwa na uoga wala mtu wa kuwafanya chochote.
kuhusu madaktari,wafanyakazi wote wana haki sawa huwezi kusema madaktari ndio bora sana kwavile wako wachache kwahiyo wawe na mahitaji mahsusi maana kuna askari pia wanaolinda raia na mali zao,kuna walimu kuna wanajeshi nk,
RAIS lazima awe mwenye kuthubutu hata kama anakosea ingawa anaweza kuwa na mapungufu yake lakini ni mara mia mwendo huu,kuisafisha hii nchi lazima kuje na uchungu,hakuwezi kuwa smooth yani mageuzi yafanyike kama kuwasha taa HAIWEZEKANI KAMWE.
 
kukosea kwa wengine uko nyuma,hakumpi ruhusa huyu wa leo,nae akosee...two wrongs don't a right!
 
We ndiye uliyehitaji dictator sio wengine. Unajua leo hii haijakutokea wewe au mzazi wako au ndugu yako yeyote ukaona anawekwa ndani na biashara zake kufungwa bila kosa na kiongozi flani kisa tu kahisiwa vibaya bila evidence, alafu anakuja kutolewa halipwi anaambiwa tu sorry utadhani sorry itamfidia kipato alichokosa akiwa ndani. Haijanitokea ila siwezi nikakaa nikashangilia vitu kama hivi hata siku moja, ana vitu yuko right ila kwenye hili yuko very wrong.

Siku ikikutokea wewe ndio utajua kama kauli "waweke ndani kama kuna errors mfix baadaye" ni statement sahihi au stupid. Tanzania mtu anafungwa kwanza alafu uchunguzi baadaye, hehehe hilo hata China hakuna, labda North Korea. Uliona kilichowatokea six, walifunga business na kuwekwa ndani alafu jamaa wanasema ati "tupe miezi mitatu tutafute evidence" Hehehe hata chizi anaona kabisa kua thats stupid.
 
Kwanza umesema haijawahi kukutokea sasa sijui mfano unautoa wapi?kwa ndugu labda?au kwa kusikia tu kwa watu wanaongea?
nchi hii ina cancer na imefikia level ya mwisho kinachofanyika ni kupiga mionzi tu ambayo pia sio mizuri kwa afya lakini hakuna namna inabidi iwe hivyo.
Ndio maana kuna kiapo cha uadilifu wafanyakazi wote wa serikali wametakiwa kuapa na moja ya kifungu cha kiapo hicho kinasema hutatumia mamlaka uliyonayo kumpendelea mtu au kumwonea mtu,kwahiyo mtu akifanya tofauti kiapo kita muhukumu.
Tuache kulialia,tujiandae tu kisaikolojia kwamba inawezekana ikafika mahali kinachoendelea sasa kikagusa maslahi yetu,ndugu na jamaa lakini kwa faida ya wengi,
mimi mwenyewe ni muhanga wa kinachoendelea ingawa sina makosa lakini sijalialia kwasababu naamini ndio kinachotakiwa kufanyika kwa maslahi ya wengi as long as RAIS ana nia njema na nchi hii.
 
Mkuu naona amepoteza na anaongoza dola bila kuzingatia vipaombele , kila kitu anataka kufanya katika mda mmoja
 
Mkuu naona amepoteza na anaongoza dola bila kuzingatia vipaombele , kila kitu anataka kufanya katika mda mmoja
Unaweza kumsaidia au kutusaidia na sisi kwamba vipaumbele vipi angeanza navyo?,yani nini angefanya kwanza na nini kingesubiri?.kwasababu imefika mahali kilakitu ni tatizo nchi hii haijulikani uanzie wapi umalizie wapi.
 
Soma kwanza historia za nchi zilizo endelea ambao walikua maskini hapo awali ndio utapata majibu. Tatizo la watanzania ni wavivu wa kusoma na kutafuta njia badala ni mahodari wa kuandika na kulalamika.
Ebu jiulize katika historia yako ndogo uliokuanayo je ilisha wahi kutokea kazi na mwendo kama huu hapa tanzania? Hata afrika nzima ukiacha afrika kusini? Leo hii mnawekewa kila kitu wazi, hadi mapato na matumizi ya kodi lakini bado tunalalamina. Au bora basi Magufuli nae angejilia zake tu kwa mrija ndio mgefurahi. Uwazi upo kwamba serikali zilizopita ziliadhiri nchi sana

..hata wewe naona unalaumu pia.

..swali langu ni dogo tu, and I want to be fair to this administration.

..je, ni muda gani utakuwa muafaka kuanza kupima mafanikio na mapungufu ya utawala wa Raisi Magufuli?
 
Kupima mafanikio na mapungufu yanaweza kufanyika wakati wowote, na inatakiwa ifanye wa watalaam wasio na upendeleo lakini sisi wananchi wa kawaida ndio tunaishia kulalamika kila siku kwamba mbona hatuoni hayo maisha mazuri tulioahidiwa.
Mimi binafsi nikiangalia maendeleo ya miaka iliopita na ya leo ni tofauti.
Leo hii unawekewa wazi mapato ya serikali na matumizi yake. Kwa sasa hivi serikali lazima ijitahidi kukusanya kipato chakutosha ili itimize angalau baadhi ya ahadi. Kwanza ufahamu mwana siasa hata siku mmoja hatimizi ahadi zake kwa asilimia mia. Hata huku ulaya pia wanatoa ahadi nyingi tu
 
Tangu awe rais ana miezi minne na nusu hivi kati ya miezi sitini anayotakiwa awe rais. Kama uonavyo bado hata teuzi za wasaidizi wake zinaendelea. Ikiwa teuzi zitakamilika ndanh ya miezi sita, binafsi naona tumpe mwaka mmoja mpaka mmoja na nusu ndipo tuanze kumpima. Urais si kigodoro.

..asante kwa majibu yako.

..now, at what point utasema Raisi amekamilisha zoezi la kuunda timu yake?

..tayari ameshateua Mawaziri, Makatibu Wakuu, na juzi wakuu wa mikoa. what is next?

..Je, unataka tusubiri mpaka ateuwe wakuu wa wilaya, halafu ndiyo tuhesabu mwaka mmoja kutoka hapo?

NB:

..kuna wachangiaji wenzetu wanakuwa wakali kweli kila wazo la kupima utendaji wa Raisi wetu linapoletwa.
 
Habari wanaJamii,

Mafanikio katika kazi na maisha mara nyingi hayaji kwa kusema tu,bali kuingia kazini na kufanya kazi kwa akili na nguvu zote.Mafanikio baina ya watu au kitu hayawezi kulinganishwa,bali tunaweza kuangalia hatua na mwelekeo wa jambo hilo kutokana na kuwa tumetofautiana katika mafikiri,maono,resources na hata wale wanaokuzunguka.

Katika uongozi wa nchi,mafanikio hayaji kwa maamuzi ya raisi mwneye bali ushawishi wake kwa kile anachoamini akishirikiana na washauri na wataalumu katika ujuzi wa jambo.

Kwanini nasema Magufuli hawezi kufanikiwa?Awali,ikumbukwe mimi napenda kazi anazofanya raisi katika kupunguza matumizi,rushwa nk.Lakini je akimaliza awamu yake yeye,Tanzania haiwezi kurudi kwenyewe pale alipokuta?

Lazima tukubaliane kuwa sasa ni wakati wa kwenda mbele.Vietnam,south korea na nchi nyingi zilizotuacha, hazjafika hapo kwa maneno na siasa.Wamefika hapo kwa kujituma na kufanya kazi lakini kubwa Zaidi ni mfumo thabiti na sheria zilizotungwa kunufaisha nchi.

Hii leo,wako wanaopinga katiba ya warioba ambayo imeelezea na wananchi wameafiki.Tumekuwa tukitunga sheria za kuwanufaisha wakubwa na wale wanaofanya kazi serikalini;huu ni wakati wa wananchi watanzania kufaidika na kuwa na fahari na nchi yao.

Namshauri raisi kwanza aangalie mzigo na utitiri wa viongozi wandamizi kwenye serikali yake.Ukuu wa wilaya,mkoa na vyeo vingi wasomaji mnavijua.

Rais Magufuli bado anaamini kuwa anaweza kuongoza nchi kwa njia zile zile watanguliz wake walipopita na tukafanikiwa,hili naliona ni usingizi wa mchana.

Namshari raisi Magufuli awe kama maraisi waliotokea na kuunda mifumo, mfano,raisi wa marekani Raisi Roosevelt,Reagan na weingine ambao ndio walioweka misingi mikuu ya taifa la marekani na kuwafikisha hapo waliopo.Magufuli,anahitaji kuwa na maono hata kama uraisi ni wakupewa.

Lazima ifike wakati tuwe na maono na ndoto ni wapi tunataka kwenda,huku tukikumbuka wapi tunatoka.Raisi usiwe mwoga kufanya maamuzi na mapinduzi ya uchumi.Kwa mwendo huu na yale unayoaamini,na kasi hii uliyoipa jina "Hapa Kazi tu" ni sawa na usingizi wa mchana wa maskini aliyeshiba ugali na maharagwe.

Hakuna unalolijua Dunia hii, hizo nchi zote ulizozitaja kama Korea Kusini, na nyingine kama Singapore, Taiwan, hata Ujapani yenyewe zilijengwa na mfumo kama huu wetu, kwanza unaweza kusema nchi karibia zote Dunia hii zilijengwa na mfumo kama huu wetu ambapo unakuwa na strong man ambaye ana madaraka makubwa na hivyo kuweza kuharakisha maendeleo!

Tatizo lako umeanza kuzisikia Korea Kusini jana bila kuelewa Korea Kusini imetoka wapi na ijengwa na vipi na nani? Rudia tena kusoma historia, hata nchi za Ulaya pia zilijengwa na Katiba inayompa kiongozi madaraka makubwa kama hii yetu hivyo wacha kupotosha hapa!

Sheria zote zipo Tanzania kilichokuwa kinakosekana na utii na ufwatliaji wa hizo sheria, hivyo hakuna haja ya Katiba ya Warioba wala ya kwako isipokuwa Katiba hii hii tuliyo nayo inatosha kabisa kama tukiwa na Uongozi makini kutoka hapa!
 
Mkuu usitake kujifanya unajua kuliko watu wote.
Hakuna aliyemkosoa magufuli hapa bali kumpa changa moto na kumwaminisha asije kuvaa viatu vya wenzake.
Mfumo wetu ni mbovu. Utake usitake. Sisi waafrica hatujui kutawala,wala kujitawala. Hatujui tunataka nini ila tunachojua ni kuhodhi madaraka makubwa kwa manufaa yetu.

Kwa staili hii ni wazi kwamba tunahitaji katiba tofauti na hapa sijaongelea structure ya katiba nzjma bali utendaji,effectiveness ya serikali katika kuwatumikia wananchi na katika hilo nimeona ni blea tuanze na sheria na utawala bora.
 
Sjasoma hoja yako, ila aise wakati unaandika na mimi nilitaka kuja na hoja kama hiyo, ila kwa ufupi Rais wetu, hana vission, he is not a visionary leader.ili ni kosa kubwa ndio maana anataka wakuu wa mikoa wafanye kazi, kira kona watui wafanye kazi paspokujua kuwa watu hawna kazi je wanafanya nini? je kuiba ni kazi watu wote waibe? ndio maana yeye kama yeye ukimuuliza vision yake inamtaka atoe ajira kiasi gani jawezi kutajia? viwanda vingapi unataka kuvijenga ? utavijengaje? lakini anakwambia atavijenga, bnafsi nilipenda Lowasa awe raisi wa nchi hii, alafu Magufuli awe Wazir mkuu, nakwakbieni nchi hii ndani nya miaka mitano ingeitwa dependent Bajet country. ni hayo tu
 
Back
Top Bottom