Kwanini Maghufuli asiwe waziri wa nishati?

PhD anafanya wapi mkuu?asije naye akawa kama wale wasomi wa internet aliyowasema Mwakyembe kwenye press conference,teh tehe

Ni kweli mkuu, magufuli anafanya PhD sasa na haita kuwa feki anafanyia UDSM na kama sikosei anaangalia mbolea fulani katika ganda la korosho you can prove it.
 
magufuli ni kichwa ambacho kinafanya mambo kwa ujasiri.kutokana na mchango muhimu aliotoa kwa siri-kali yetu anafaa sana kuwa waziri wa nishati na madini.kwani tumewekeza badala ya kulinda nishati zetu.tumekua tukinufaisha watu wachache badala ya umma kwa ujumla.ndugu magufuli anaweza fanya kazi yake kwa ufansi kabisa kwani amekua mwaminifu kwa kila anapowekwa na siri-kali
 
Sidhani kama Mh Magufuli ndiye aliyetoa wazo la kuuza nyumba za Serikali, naamini yeye alikuwa antekeleza tu uamuzi wa baraza la Mawaziri na Serikali kwa jumla.

Magufuli bado ni mchapa kazi ambaye kama angekuwa Kiranja wa Mawaziri naamini Serikali ingefikia viwangi vya juu vya utendaji, jamaa yuko fiti sana haijalishi Wizara aliyopewa haina umaarufu kiasi gani akipewa Magufuli, Wizara hiyo itaonekana umuhimu wake na viwango vyake vya utendaji kazi vitakuwa juu.

Jamaa anafaa na kuonesha anakubali kwa utendaji na hapendi majungu ila HANA MAKUNDI/MWANAMTANDAO ndio maana wenye WANAMTANDAO wana taka "kumuuwa" kwa kumpa WIZARA ambazo hazina sauti/hazi mfanyi kusikika.LAKINI JAMAA KILA AKIPEWA ANAJIONESHA KWA UTENDAJI WAKE MZURI
 
Magufuli

Wanamchafuwa tu kama walivyomchafuwa Salm ili kumnyima nafasi ,mambo wanayoandika ni uzushi .

Naanza na barabara wanayosema kupindishwa kijijini kwake hata kama ningekuwa mimi ningefanya kama alivyofanya.

Eti tuseme kama upo pale feli na kati ya feli na kigamboni ni kapoli kenye barabara ya ng'ombe na kutoka feli->Mbagala rangi 3->kongowe->changanyikeni ->kigamboni kuna barabara ya vumbi wamekupa pesa ujenge barabara utafuata njia ipi? jamani huo ndio uzuri wa kumpa Waziri maeneo yake ya elimu huwezi mzuga ili ujenge parefu upate fedha za kufisadi.

Barabara iliyojengwa kutoka BWANGA kupitia CHATO ,Mganza hatimaye MLEBA ni safari ya masaa mawili.
Na barabara wanayoshabikia wengi ni BWANGA-> BIHARAMULO->KATOKE-> BUKOBA kwa gari ni zaidi ya masaa KUMI na mawili.

Na kutoka KAMANGA Feli upande wa Sengerema hadi BWANGA ni masaa manne hadi sita.

Na kutoka bandari ya mwanza hadi kemondo na hatimaye bukoba ni zaidi ya masaa tisa hadi kumi na mawili kwa meli wewe ungefanya nini? Engineer mzima ukubali kudaganywa wakati unafahamu ukweli??

Hata hizo meli nani ameshasafiri hiyo barabara ya kati ?? MAGUFULI alipiga mahesabu si ya kisiasa bali ya ki ENGINEER na kukuonyesha asilimia kubwa lazima meli hizo zitaanguka SEKENKE maana pale kila mmoja anapafahamu.
Na akawaelezeni kabisa barabara zetu ni finyu hivyo kusafirishwa meli nzimanzima lazima barabara ifungwe kama wewe msafiri ungekubali barabara kufungwa kwa siku kadhaa ama masaa?


sounds like unadhani magufuli is an engineer graduate.wengi wanadhani hivyo.jamaa ni Bsc.education nadhani hata masters alinyuka hiyohiyo.
 
Ni kweli mkuu, magufuli anafanya PhD sasa na haita kuwa feki anafanyia UDSM na kama sikosei anaangalia mbolea fulani katika ganda la korosho you can prove it.

Nakumbuka sakata lake na jamaa wa Tanroads walipodai kuwa jamaa(Magufuli)anawaonea wivu wasomi(wao).
Magufuli akawaambia-yeye mwenyewe ni msomi hivyo hana sababu ya kuwaonea wivu.
Naona sasa anataka u PhD holder ili awamalize kabisa!
 
Jamani semeni mlivyosema,pondeni mlivyoponda lakini Magufuli is a hero.Ujasiri wa kina Sokoine na Mrema siwezi kuushabikia sana kwa sababu enzi hizo sikuwepo au nilikuwa mdogo hivyo sikuweza kufuatilia mambo ya siasa za tanzania.Magufuli alifanya kazi nzuri sana wakati wa Mkapa na nilikuwa nafuatilia sana utendaji wake.
Mpaka leo hii nafuatilia viongozi wa bongo sijaona mtendaji kama Magufuli.Jamaa ana msimamo,vision na mfuatiliaji mzuri sana wa mambo kitu ambacho viongozi wetu wengi hawana na ndiyo mana wanampiga vita sana na kumfitini na kusambaza uzushi wa kumchafua.Magufuli muweke kokote kule ata perform tu.
Bahati mbaya watu wachapakazi,wasiopenda uswahiliswahili,unafiki na majungu hawana nafasi katika uongozi wa nchi yetu.
Lakini naamini Magufuli angepewa uwaziri mkuu au hata hiyo wizara ya nishati au hata angebaki kulekule ujenzi nchi yetu ingekuwa katika hali nzuri zaidi ya ilivyo sasa.
Naomba kutoa hoja!
 
Aliyeleta mada hii ashukuriwe, Tungekuwa na mawaziri hata watano kama magufuli basi watu wangekuwa na adabu.Nakumbuka JKaliokuwa ansoma baraza jipya,watu walikuwa wanasubiri kujua jamaa atapelekwa wapi,na nakwambia cku hiyo watu wa hiyo wizara walisikitika saana,wakasema jmaa hafai. Hii ni kwa sababu jamaa pamoja na fani yake ya uhandisi kweli anawakilisha,hataki mijadala ya muda mrefu isiyokuwa na maana yoyote,kazi kazi.


Hongera saana magufuli,tunaamini sisi vijana tumejifunza mengi kutoka kwako,cha kwanza ikiwa ni uchapakazi kwa kila wizara unayoifanyia kazi.Hata jamaa akikaa miezi michache,anaonyesha kazi aliyoifanya. Umekuwa ni jasiri pale unapoamua kufuatilia kile unachokiamini bila kumwogopa mtu yeyote.

Kuna mawaziri toka wateuliwe hawajawahi kufanya kazi yoyote ya maendeleo katika wizara husika,japo kila awamu hawakosekani.Na hawa ndo wanturudisha nyuma kimaendeleo,bali ni maneno bila vitendo vyovyote vile!!

Mungu akujalie maisha marefu magufuli.
 
magufuli hata u PM anafaa.

ukiacha hapo wizara ambayo inafaa magufuli kuwekwa ni ile ambayo ikidhibitiwa na kuendeshwa vizur pato letu litaongezeka na ufisad dhid yetu utapungua.

ni kweli madin na nishat ndo kwenyewe

lakin nashangaa. kwanini hatufikirii awe ndo rais ajaye?
 
magufuli hata u PM anafaa.

ukiacha hapo wizara ambayo inafaa magufuli kuwekwa ni ile ambayo ikidhibitiwa na kuendeshwa vizur pato letu litaongezeka na ufisad dhid yetu utapungua.

ni kweli madin na nishat ndo kwenyewe

lakin nashangaa. kwanini hatufikirii awe ndo rais ajaye?
Watu chichim wapo lakini basi tu!
 
sounds like unadhani magufuli is an engineer graduate.wengi wanadhani hivyo.jamaa ni Bsc.education nadhani hata masters alinyuka hiyohiyo.

GENERAL
Salutation Honourable Member picture

First Name: John
Middle Name: Pombe Joseph
Last Name: Magufuli
Member Type: Constituency Member
Constituent: Biharamulo Mashariki
Political Party: CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location: P.O. Box 9132, Dar es Salaam
Office Phone: +255 713 322272/+255 754 292580
Ext.:
Office Fax: + 255 22 2124505
Office E-mail: jmagufuli@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date: 28 December 2005
End Date: 30 August 2010
Date of Birth 29 October 1959
EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam B.Sc Ed. (Hons) Chem.&Maths 1985 1988 GRADUATE
Universities of Dar es Salaam, TZ &Salford -U.K. MSc. (Chem) 1991 1994 MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam. PhD (Chem) 2006 NOT COMPLETED
Mkwawa College of Education Diploma in Education (Sc.) Chem., Maths&Edu. 1981 1982 DIPLOMA
Mkwawa High School A-Level Education 1979 1981 HIGH SCHOOL
Lake Secondary School ? Mwanza O-Level Education 1977 1978 SECONDARY
Katoke Seminary Biharamulo, Kagera O-Level Education 1975 1977 SECONDARY
Chato Primary School Primary Education 1967 1984 PRIMARY

Hii master ni ya chemistry ama chemical engineeing.Mzee asante kwa kuhabarishana
 
kama aliweza kuyumbishwa kwenye nyumba za serikali na yeye akatrumia advantage kumbapa ndugu/girl friend sasa itakuwaje kwenye madini? si atatoa mgodi mzima? na Umeme atawapa Girfriend au ndugu?
Na sasa hivi katoa rushwa ya Kanisa huko Biharamulo, litumike na madhehebu yote? what about Wauslamu? au Biharamulo hakuna waislamu? Hafai uongozi .., mwambie akatambike upya
 
Ibrah, wewe inaonekana unamfagilia sana jamaa, sasa tukianza kubenchmark waovu na kusema huyu ni bora zaid itakuwa sio sahihi. Kama ulinpata vizuri nilisema ukweli jamaa ni mchapa kazi but is not such clean kama mnavyo mnadi

No one is 100% clean!
 
GENERAL
Salutation Honourable Member picture

First Name: John
Middle Name: Pombe Joseph
Last Name: Magufuli
Member Type: Constituency Member
Constituent: Biharamulo Mashariki
Political Party: CHAMA CHA MAPINDUZI
Office Location: P.O. Box 9132, Dar es Salaam
Office Phone: +255 713 322272/+255 754 292580
Ext.:
Office Fax: + 255 22 2124505
Office E-mail: jmagufuli@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Start Date: 28 December 2005
End Date: 30 August 2010
Date of Birth 29 October 1959
EDUCATIONS
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam B.Sc Ed. (Hons) Chem.&Maths 1985 1988 GRADUATE
Universities of Dar es Salaam, TZ &Salford -U.K. MSc. (Chem) 1991 1994 MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam. PhD (Chem) 2006 NOT COMPLETED
Mkwawa College of Education Diploma in Education (Sc.) Chem., Maths&Edu. 1981 1982 DIPLOMA
Mkwawa High School A-Level Education 1979 1981 HIGH SCHOOL
Lake Secondary School ? Mwanza O-Level Education 1977 1978 SECONDARY
Katoke Seminary Biharamulo, Kagera O-Level Education 1975 1977 SECONDARY
Chato Primary School Primary Education 1967 1984 PRIMARY

Hii master ni ya chemistry ama chemical engineeing.Mzee asante kwa kuhabarishana

Mkuu thanks for the infor!
 
ni kwasababu alikuwa rafiki wa mkapa, mtu ambaye kikwete amekuwa akimuwinda na kumwonea wivu tangu awali, Mkapa kwanza hakupenda kabisa kikwete achukue huu urais, kikwete mwenyewe analijua hilo, pia kina sumaye na kampeni zake kama magufuli alichangia kidogi, aliliwa. wote waliomsapoti sumaye au marafiki wa mkapa kama kina Dr.kigoda na wengine, walipigwa chini kimtindo hivi. magufuli alikuwa rafiki sana wa mkapa, na hata zile nyumba alilazimishwa tu na mkapa na selikali yake, asingeweza kufaiti peke yake jamani.

kipindi cha nyerere, ikumbukwe watz walimpenda sana kikwete awe rais, lakini kwa kupitia nyerere, kikwete alinyang'anywa donge mdomoni, miaka yote kumi akavumilia na maumivu monyoni. watz walimpenda sana kikwete tangu miaka kumi na nne iliyopita. hivyo mkapa kumnyang'anya tonge mdomoni kwa miaka kumi vile, hata hivyo amemstahi tu, ilikuwa akiingia kwenye madaraka arudishe visasi. mkapa alipenda kigoda au sumaye awe rais hata baaya ya kikwete kuvumilia kwa miaka yake yote kumi hiyo. na katiba tu inamlinda mkapa, kikwete angemmaliza kama alivyommaliza sumaye. hivyo ana kinyongo na magufuri vilevile kwasababu magufuri watu walimpenda hata awe rais na wengi tulijua atakuwa waziri mkuu wakati wa kikwete.
 
Hili swali la marehemu Kandambili bado ni sahihi hata leo hii.

Watu waadilifu wanapopungua ndani ya nchi, wale wenye uaminifu wachache hutamaniwa kila kona kulinda maslahi ya umma. Kweli naona kuna kafundisho fulani ndani ya swali hili.
 
..watu wanaiba halafu wanajibanza nyuma ya mgongo wa Mkapa.

..Mkapa hakuwa na shida ya nyumba kwasababu maraisi wastaafu wote hujengewa nyumba.

..sasa kama Magufuli anadai alilazimishwa na Mkapa, basi wakati ni huu kwa yeye kurudisha serikalini nyumba aliyojitwalia.

..angekuwa waziri wa madini na nishati angekwapua mgodi wa madini halafu asingizie kwamba ni Mkapa ndiyo kamlazimisha.
 
Maslahi ya wakubwa yamejikita huko kwenye nishati ndio maana hata miundombinu kanyimwa kusimamia bandarini maana nako kuna maslahi ya wakubwa na uozo mwingi sana.
 
Hivi hii thread ni ya lini? Uchaguzi wa 2010 umeshapita na Masha siyo waziri tena sasa mbona tunarudishwa nyuma?
 
Ukizingatia umuhimu wa wizara hii nyeti na usimamizi unaohitajika,itabidi rais amteue waziri mwingine shupavu kuongoza hii wizara.

Ni wakati sasa wa rais kumkabidhi John P.Magufuli usukani wa nishati na madini ili kuendeleza pale atakapo achia Mhongo kama atabwaga au kubwagiwa manyanga kutokana na uhusika kwenye wizi wa Tegete Escrow.

Magufuli amefanya vizuri kwenye wizara zote alizoenda(ukiacha uuzaji ovyo wa nyumba za umma)
 
Back
Top Bottom