Kwanini Maghufuli asiwe waziri wa nishati? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Maghufuli asiwe waziri wa nishati?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kandambilimbili, Mar 19, 2009.

 1. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #1
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia utendaji wa Mh POMBE Maghufuli kutoka kujua idadi ya miradi ya baraba na kila mradi alikuwa anakutajia garama na urefu wake.

  Kwenye Ardhi kafanya mambo makubwa sana.

  Kwenye Kitoweo anaweza kukutajia mpaka idadi ya mayai ya samaki yaliyotajwa leo, HIVI MTU KAMA HUYU AKIWEKWA KWENYE WIZARA YA NISHATI NA MADINI SI ITAKUWA BALAA? Tutakuwa na takwimu ya tani ngapi zinavunwa na ngapi tuaibiwa na huo utakuwa mwisho wa mikataba FEKI ya madini inayotutafuna. HONGERA KWA KUIKAMATA MIJIZI YA SAMAKI SIJUI KIASI GANI WATANZANIA TUMEIBIWA MPAKA MIDA HII.

  NOTE: POsting hii haina uhusiano na 2010.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nadhani tusiwe too autistic. Tuangalie beyond hawa waliotufikisha hapa tulipo. Kwa kuanzia hakufurahisha wengi jinsi alivyouza nyumba za serikali na kuna mengine pia.
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pessimist, All in all jamaa anathubutu na ana msimamo, kila utakapomuweka yuko fit, mazuri na mabaya yake kipi kina outweigh n dio tucapitalize suala la nyumba sitachangia sana sijui kama alilikuta, lilimkuta au alipewa maagizo.
   
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwenye uuzaji wa nyumba kulikuwa na mkono wa mheshimiwa kwahiyo asingeweza kuzuia.
   
 5. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Uuzaji wa nyumba haukuwa mpango wa Magufuli bali ulikuwa ni wa Mkaapa na Sumayo. Tunamuonea Magufuli bure!
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwa nini usiseme Magufuli awe PM?
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwanini asiwe raisi? Maana nchi inakosa mwelekeo kila siku!
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  We wasema.
   
 9. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dr. Mwakyembe ndiye angefaa kuwa Waziri wa nishati au mkurugenzi wa Tanesco. I wish it was possible. Angeweza kuishughulikia mikataba yote mibovu inayoiletea shida nchi hivi sasa, kuanzia IPTL hadi Dowans. Ila tu itabidi ajiuzulu kwenye PowerPool.
   
 10. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutoa hilo wazo. John Pombe Magufuli angefaa awe Waziri wa nishati na Madini badala ya Bill Ngeleja ili angalau kwa mwaka mmoja na miezi 7 uliobaki kabla ya uchaguzi 2010 asadie hii wizara ambayo kwa sasa inaongozwa na Rostam Aziz. Kama sio upuuzi wa wanamtandao alipaswa ndiye agombee Urais kama angekosa mno mno angekuwa Waziri Mkuu. Huyu bwana ana msimamo na ni kati ya wanasiasa wachache Duniani wanaofanya wanachosema/kuamini. Tatizo ni kwamba huwezi kuwa na RAIS asiye na msimamo ukawa na Waziri Mkuu shapu hayo tuliyaona wakati wa Mwinyi, Mkapa na juzi Teddy Lowasa alivyotaka kumpiku JK ndio maana akamchagua Pinda awe rahisi kupinda. Magufuli usikate tamaa iko siku tutakupatia Urais hata kama kwa kutumia Peoples power staili ya Madagascar hata kama CCM hawataki tunaye Spika atakuapisha tu. Kwa sasa tupatie vibua kwa kwenda mbele usiogope zile nyumba alitaka Mkapa kwa Ubabe laikini ungejua ungejiuzulu tu mbona hata Ruksa alijilipua lakini akarudi na ruksa zake mbovu?
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawezi kuwa kwa sababu si mwanamtandao na hayuko karibu na rais.
   
 12. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #12
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi naona hapa Tanzania labda Mwakyembe, Maghufuli na Seleli katika CCM ndio walio na unafuu, pengine ndo tungetaka wagombee nafasi hizo kwa sasa; waliobaki wote uozo mtupu kwa mtazamo wangu
   
 13. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwenye uthubutu angekataa kukamilisha zoezi au angejiuzulu kama kulikuwa na mkono mzito kwenye zoezi lile.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama Mh Magufuli ndiye aliyetoa wazo la kuuza nyumba za Serikali, naamini yeye alikuwa antekeleza tu uamuzi wa baraza la Mawaziri na Serikali kwa jumla.

  Magufuli bado ni mchapa kazi ambaye kama angekuwa Kiranja wa Mawaziri naamini Serikali ingefikia viwangi vya juu vya utendaji, jamaa yuko fiti sana haijalishi Wizara aliyopewa haina umaarufu kiasi gani akipewa Magufuli, Wizara hiyo itaonekana umuhimu wake na viwango vyake vya utendaji kazi vitakuwa juu.
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  JK chukua ushauri huo ili umteue Magufuri Waziri wa nishati na Madini siku za usoni utakapovunja baraza la Mawaziri ili uwaondoe Masha,Ngeleja na Nchimbi.
   
 16. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  PM ataishia kutoa maelekezo tu na atadanganywa awepo KUNAKOPIKWA MCHUZI


  HILO NALO WAZO ZURI SANA, lakini wacha asafishe huku chini kwanza na apate experiense zaidi.


  HUYU JAMAA ATATAKA KUIMARISHA MRADI WAKE KWA FAIDA YAKE, hawa PHDs na Maproffessor wafanye tafiti na watupe matokeo sisi watendaji tuzifanyie kazi (JOKE)
   
 17. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Akiwaondoa hao ni kina nani watamsaidia kurudi madarakani 2010?
   
 18. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Uamuzi wa kuuza nyumba haukuwa wa magufuli ila lake lilikuwa tu ni utekelezaji. Mkuu wako anapohitaji chochote bwana inabidi umtengenezee mazingira au ukiona huwezi basi upotelee mbali. Ukweli wa nyumba upo kwa BM, kwani ni jambo rahisi kujiuliza yeye BM alichukuwa nyumba ipi. Ingewezekana angajiuzia ikulu. Sasa kwa kuwa wafrika tumezoea kuweka vikao na kubadilisha taratibu na sheria ili zikidhi mahitaji yetu binafsi ya sasa, usishangae.
   
 19. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ila kweli Magufuli kupewa Wizara ya vitoweo ni kumwonea tu!

  Yaani misuse of his capacity!

  Yaani waziri wa Kuku, ng'ombe, kondoo wote na samaki Tanzania??

  Kama uko mahali unapata mchemsho wa kuku, samaki jua dingi wanke ni Mzee Magufuli!
   
  Last edited: Mar 23, 2009
 20. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Taratibu mzee
   
Loading...