MAGOMENI KOTA- Hapa ni pale karibu na makao makuu ya manispaa ya kinondoni na pameitwa hivyo kutokana na vile vinyumba vya serikari vilivypo hapo (Quartes)
MAGOMENI mAPIPA- H aya ni maeneo yanayoanzia pale KKKT mpaka Deluxe kule na hilo jina lilitokana na nyumba nyingi za eneo hili kuwa zimeezekwa na mifuniko ya mapipa enzi hizo
MAGOMENI MAKUTI- kwa wakati huo nyumba nyingi za eneo hilo zilikuwa zimeezekwa na makuti
HANANASIF- Hli ni jina la mjerumani aliyekuwa anamiliki hilo eneo alikuwa anaitwa HANNA NASIF
OYSTERBAY- huo ni muunganiko wa maneno mawili OYSTER na BAY, OYSTER kwa maana ya makonokono yaliyokuwa yanapatikana kwa winggi eneo hilo la bahari na BAY kwa maana ya ufukwe (upwa)
MSASANI- hilo lilikuwa jina la mtu maarufu sana eneo hilo akiitwa MUSA HASSANI, na eneo hilo lilikuwa limejaa wamakonde wengi sana (nadhani mpaka leo), na kwa wao ilikuwa ni vigumu sana kuita MUSA HASSANI na badala yake wakawa wanatamka MUCHA HACHANI, NA MWISHO NDIO IKAWA JINA.
MIKOCHENI- hilo lilikuwa jina la mzungu mmoja alikuwa akikaa maeneo hayo akiitwa MICHAEL CHAIN (MAIKO CHEINI)
MABIBO- hilo eneo lilikuwa maarufu sana kwa kupika gongo (nadhani mpaka leo), na gongo nyingi iliyokuwa ikipendwa ilikuwa ikipikwa kwa mabibo, sasa wale wanunuzi walikuwa wanauliz ahiyo ya nini? na muuzaji hujibu MABIBO, na mwisho ikawa jina
MWANANYAMALA- hilo ni neno la kizaramo likiwa na maana ya MWANA NYAMAZA