Keko Magurumbasi: Mzee Magurumbasi alikuwa ni mzee mashuhuri mitaa hii, mzee huyu alikuwa anafuga mbuzi wengi tu. Mbuzi hao walikuwa wanafunguliwa asubuhi na kurudi jioni, walikuwa wanazurura hadi mitaa ya zamani KAMATA. Hakuna hata mmoja aliye potea au kuibiwa.