Kwanini maeneo haya yalipewa majina ya hivi?

Kwanini maeneo haya yalipewa majina ya hivi?

Mikocheni kulikuwa na mzungu anaishi maeneo yale anaitwa Michael Shane wamakonde walishindwa kumuita jina lake wakawa wanamuita mikocheni ndio jina likazaliwa.Jogoo kulikua na kiwanda cha unga kinaitwa chapa jogoo na jina jogoo likakua.Kawe ilikuaga ni njia ya ng'ombe(cow way) kwenda kwenye kiwanda cha kusindika nyama cha tanganyika packers,watu wakawa wanapaita kawe.Makongo kulikua kuna mashamba ya mikonge waarabu walishindwa kuita mikonge wa wanaita makongo.
 
Mleta uzi mgeni sana Dar kama anashagaa hat sinza kwa remmu au sgrika sana basi ni mgeni mno
 
Washington Dc ni moja kati ya majimbo mengi yaliyopo marekani ilikuwa maarufu kutokana na Rais wa kwanza wa US kuishi hapa muda mrefu sana ambae ni joji washington
 
Pale mbezi mkono wa kushoto ukienda Tegeta kulikuwapo tanki la maji ambalo kwa siku nyingi lilikaa hapo, sasa limeondolewa. Lilikuwa linaonekana hata ukiwa barabarani na limetoweka mwishoni mwa miaka ya tisini. Watu walilitumia kama reference point ya kukutana na likawa jina na ni kituo maarufu cha mabasi halta kesho.

Samaki wabichi kuna mtu alikuwa anauza samaki fresh pale, wengi walienda kununua kwake na wakapafanya jina Samaki wabichi. Mwanzoni kilikuwa ni kituo cha msaada kwa daladala, kwa sasa ni kituo maarufu tu isipokuwa kwa makonda wabishi ambao hukifanya kituo cha kupakia lakini sio kushushia abiria.
kawe; maana yake pale kulikuwa njia ya kupitisha Ng'ombe kupeleka Tanganyika Packers kiwandani sasa limezaliwa kutoka jina la Cow Way, kwa kuwa watu wengi hasa kutoka bara waliokuwa wanapeleka Ng'ombe pale walishindwa kulitamka
 
Sinza mori

Ni mtu mmoja aliweka baar pale sinza karibu kabisa na barabarani jirani na kituo cha mafuta ,huyu aliweka gesti ya kwanza kabisa maeneo hayo ikaitwa mori geust baadae akaweka baar nayo ikaitwa mori baar ,huyu mori ni mzee wa zamani sana hapo sinza ndio maaana watu wakawa wanauliza sinza ipi ? Maana sinza kubwa wakawanajibu maeneo ya mori mwisho eneo hilo likaitwa sinza mori
 
Mbezi tank bovu


Kulikuwa na tank la mafuta lililoanguka pale mbezi miaka mingi pasipo kuondolewa lilikaaa sana muda mrefu hadi likachakaaa na kuwa bovu jilani kabisa na barabarani ndipo pakazoeleka tank bovu ,maeneo ya tank bovu mwisho pakaitwa tangi bovu
 
Naomba tafsiri ya "kunduchi" maana wazungu wanapata sana shida na hilo neno
 
Kimara stop over palikuwa na baa maarufu sana ikiitwa stop ova miaka ya 90 mwanzon ilikuwa tishio kwa safar resort

Kimara bucha zamani paliitwa kwa lymo Thomas needs ya Lori la ng'ombe kupata ajali hapo miaka ya mwanzon 2000 jina likabadilika
 
pale buguruni nadhani palikua na BUGURU za kutosha enzi za kale
 
pale stop ova palikua na polisi wa kikurya ba radio call yake kila akiongea maneno mawili anatia neno ova
Mfno: akikamata gari anaongea kwenye redio yake "KIMARA STOOOP" OVA
 
shekilango, huyu ni msambaa wa korogwe tanga aliyehudumu ktk awamu ya kwanza ya mwl Nyerere

Alifariki kwa ajali ya ndege wakati akitoka kwenye majukumu yske ya kikazi
 
Kurasini:- "COOL RAS INN" Ilikuwa ni sehemu ya kwenda kustarehe kwa hususan wazungu miaka hiyo kabla na baada tu ya Uhuru wa Tanganyika, kuna sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu. Wakazi wa eneo hili walishindwa kutamka COOL RASS INN na kutamka Kurasini.
 
Back
Top Bottom