Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 3,650
- 9,414
Tujifunze kuweka akiba ya maneno.
Mkuu kama yalifaulu mbona yanapangwa mengine? Unajua maana ya maandamano kwanza?Maandamano hayajafeli na yamefanikiwa. Uchaguzi haukupigwa kama ulivyotarajiwa na vituo vingi vilichomwa na vingi vyao watu hawakujitokeza kupiga kura.
Sasa leteni propaganda nyengine uchwara wananchi wako imara. Haya kama umeshinda kwa kishindo kilichokufanya mfanye uapisho kwenye kambi ya jeshi ni nini?
Unafurahia haramu ambayo dunia mzima imejua kama hakukua na uchaguzi.
Hatutaacha mpaka Tanzania isiwe na mgeni hata mmojaMkuu kama yalifaulu mbona yanapangwa mengine? Unajua maana ya maandamano kwanza?
Haya sawa, Keyboard warrior nawaelewa vyema kwanza unakuta wakati huo ulikuwa chini ya uvungu wa kitanda hutaki shida na mtu, Ungekuwa front wewe si ungekuwa kwenye kesi ya uhaini mbona uko gheto sahivi mguu juu na mkono ndani ya boksa uanajisabahi ngogweHatutaacha mpaka Tanzania isiwe na mgeni hata mmoja
Natoa madini mnakaza shingo, Kama unahisi ulishinda haya sawa? Ungefiwa na ndugu zako ungenielewa ila kwa kuwa ukoo wenu wote waoga ndo maana mpo salama.Bibi yako alikimbia kuapishiwa vichakani. Mpaka Sasa anaishi kimachale machale. Haonekani. Ni kama digidigi 😆😆.
Sasa yalifeli vipi?
😀 😀 😀 Sema wadau mmepanic sanaHaya sawa, Keyboard warrior nawaelewa vyema kwanza unakuta wakati huo ulikuwa chini ya uvungu wa kitanda hutaki shida na mtu, Ungekuwa front wewe si ungekuwa kwenye kesi ya uhaini mbona uko gheto sahivi mguu juu na mkono ndani ya boksa uanajisabahi ngogwe
Kurudia maandamano wala sio shida ni miongoni mwa kulazimisha waliojitangaza kwa wizi kujulishwa kama haupo kwenye kiti kwa uhalali wa kuchaguliwa.Mkuu kama yalifaulu mbona yanapangwa mengine? Unajua maana ya maandamano kwanza?
Me nimetoa somo kama yakienenda kwa uzembe uleule nakuambia tunarudia kuzika.
Cc min -meNone sense
Tunaomba feedback kiongoziMAANDAMANAO YA 29OCT YATAFELI VIBAYA MAPEMA SANA KUTOKANA NA SABABU KUU ZIFUATAZO;
Anaandika, Robert Ng'apos Heriel
Mtibeli
1️⃣ Ukosefu wa Miundombinu ya Kiufanisi.
Maandamano makubwa yenye lengo la mabadiliko ya utawala yanahitaji:
a) Kamati za mipango (planning committees)
Hizi kamati naona hazipo. Ukimfuatilia Mange Kimambi na Maria Sarungi ambao ndio vinara wa maandamano haya unagundua hawana kamati zozote zaidi ya vikao vyote vinafanyika mitandaoni na inakuwa live.
Kamati ndio msingi mkuu wa goo organization na mobilization ya maandamano haya. Kama hazipo atafanikiwa vipi? Embu msaidieni Mtibeli aelewe.
b) Mfumo wa mawasiliano ulio salama,
Udukuzi, kufuatiliwa kuliko kupitiliza, usaliti wa mawasiliano ndani ya wenye nia ya kuandamana. Hayo yote yatakwamisha maandamano.
c) Mpangilio wa uongozi wa ngazi mbalimbali (national → regional → district → ward).
Unaweza kujiuliza kama wewe ni muandamanaji. Kwenye kata au mtaa wako kuna mfumo wowote wa kuyaratibu ili yatokee. Au ndio upo pekeako kwenye actual ground lakini mtandaoni ndio upo na na wenzako?
Tumia hiyo kama scale yako.
Mazingira ya Tanzania ya sasa, upinzani au wanaharakati wengi hawana mtandao thabiti wa ndani (grassroot network).
Hii inamaanisha hawana uwezo wa kuunganisha watu hata Laki moja kwa wakati mmoja bila kutambulika mapema.
Serikali inamiliki taasisi zote za mawasiliano, usalama, na inafanya doria usiku na mchana katika mitandao ya kijamii, hivyo hufahamu mipango kabla haijatekelezwa.
Kwa mantiki ya kiintelijensia, maandamano hayo yatakufa kabla hayajaanza, kwa sababu mpangilio wake utavujishwa na kusambaratishwa mapema.
2️⃣ Ukosefu wa Uratibu wa Malengo.
Maandamano yenye mafanikio lazima yawe na lengo moja linaloeleweka na kukubalika kitaifa.
Lakini maandamano haya yana malengo zaidivya moja yanayokinzana, mfano;
a). Kupinga uchaguzi,
b). Kuiondoa serikali iliyoko madarakani kumaanisha kuindoa CCM
c) Kupinga utekaji na mauaji. Wasiojulikana. Na sababu zingine.
Lengo la kwanza ni la kisiasa (kupinga uchaguzi)
lakini la pili ni la mapinduzi (kuiondoa serikali ya Samia madarakani) ambalo kisheria na kiusalama linachukuliwa kama uhaini au uasi.
Lengo la tatu ni la kijamii na haki za binadamu za msingi yaani haki ya kuishi. (Hili lingeunganisha watu wengi zaidi).
Hivyo, wapo wanaoamini wanapigania haki za uchaguzi, na wapo wanaoamini ni vita dhidi ya serikali. Na wapo wanaoamini wanatetea haki za binadamu za kuishi kwa waliotekwa na kuuawa na kutojulikana walipo.
Kukosekana kwa umoja wa tafsiri ya malengo kunafanya maandamano hayo yasifanane kihoja, kimkakati, wala kiitikadi, hivyo yatakosa mwelekeo mapema.
3️⃣ Udhaifu wa Uongozi wa Harakati.
Harakati yoyote ya kisiasa inahitaji:
a) Kiongozi mwenye karisma,
Najaribu kuangalia nani ni kiongozi aliyenyuma ya haya maandamano mwenye ushawishi. Kama ni Tundu Lisu yupo zake gerezani anapambana na kesi yake ya mchongo.
b) Mtu anayeaminika na umma,
Mwenye uwezo wa kujenga hadithi ya matumaini, hadithi zenye kuchochea chuki ya wananchi kwa serikali. Humphrey Polepole naye alitoa matumaini lakini amekamatwa dakika ya sabini ya mchezo kipindi cha pili.
Tanzania kwa sasa, licha ya kuwa na wanasiasa wa upinzani, hakuna kiongozi mmoja anayekubalika kitaifa kama sauti ya mabadiliko ya kweli.
Wengi wamechoka, wamegawanyika au wamo katika mikakati ya kisiasa ya muda mfupi. Na serikali inajaribu kila njia kuwavunja vunja na kuwagawanya kadiri inavyowezekana. Jana mumemwona Ezekiel Wenje. Ni kwamba wanawakatisha tamaa na kuwavunja moyo watanzania.
Bila kiongozi thabiti mwenye command structure, watu wanakuwa kama kundi lisilo na kichwa. Yaani kundi linajiendea endea bila mwelekeo. Hayatakuwa na tofauti na vuguvugu la Luddism kwa wale mliosoma Advance History 2.
Ndiyo maana kwa kitaalamu, maandamano kama haya huanza kwa makelele mitandaoni na kufa siku ya tukio. Haitakuwa mara ya kwanza.
4️⃣ Udhibiti Mkali wa Vyombo vya Usalama.
Kitaalamu, Tanzania ni nchi yenye mfumo wa ulinzi na usalama ulio wa kiintelijensia zaidi kuliko wa nguvu.
Taasisi kama:
I). TISS (Usalama wa Taifa),
ii) Jeshi la Polisi,
Iii) JWTZ (Jeshi la Wananchi)
Na vitengo vya cyber intelligence
vina uwezo mkubwa wa kutambua, kuvuruga, au kuzuia matukio kabla hayajafanyika.
Kwa mfano:
a) Mawasiliano ya Wapanga maandamano hufikiwa kupitia “surveillance”,
b) Viongozi wa maandamano hufuatiliwa kimyakimya,
c) Wengine huchukuliwa “preventive custody” kabla ya siku ya tukio.
Ndio hao unasikia kila siku wanakamatwa mara leo huyu kesho yule.
Wahamasisha maandamano mtandaoni au watu wenye mrengo huo nao huchukuliwa mapema kabisa kabla ya siku husika.
Mtu kama John Heche, John Mnyika, na wenzake hawawezi kuwa uraiani kufikia tarehe 29.
Watahifadhiwa kwa muda huku wakipewa usumbufu kidola mpaka upepo utakapotulia wataachiwa.
Hii inaondoa uwezekano wa maandamano kuanza kwa wingi au kwa ufanisi.
Kitaalamu, tunaita hii “preemptive disruption model” njia ambayo huzima uasi kabla haujaanza.
5️⃣ Hofu ya Kijamii.
Wengi wetu Watanzania ni watu wa amani tusiopenda vurugu, na tumelelewa kwenye misingi ya “amani ni bora kuliko vurugu, au funika kombe mwanaharamu. Apite".
Kisaikolojia, jamii imejengwa kuwa risk-averse (uepukaji wa hatari).
Hivyo, hata kama wanakubaliana kimoyomoyo na hoja za maandamano, wengi hawatashiriki hadharani.
a) Mfumo wa kiutamaduni, kiimani (dini), na kijamii unahimiza utii kwa mamlaka.
Wengi wataishia kusema “Mungu ataingilia” "Mungu atajibu", "tumuachie Mungu" au “Tusubiri uchaguzi mwingine”, hivyo kuua nguvu ya umoja wa kuandamana.
Kwa hivyo, uungwaji mkono utakuwa wa moyoni na mitandaoni lakini si wa miguu kwa mguu sako kwa bako. Watu wanakubaliana mtandaoni, lakini hawatokei barabarani.
6️⃣ Udhibiti wa Habari na Mitandao.
Serikali ina uwezo wa:
a) Kufunga mitandao ya kijamii.
Ikifunga mitandao wananchi wangapi wanauelewa wa kutumia VPN na mambo ya kidijitali. Wangapi?
b) Kudhibiti vyombo vya habari,
Media zote, redio zote, na wenye followers wengi watadhibitiwa iwe kinguvu au kwa kupewa pesa kuwatuliza
Si ndio yale mtaishia kumlaumu Millard Ayo wa watu. Atafanya nini?
c) Kuendesha kampeni za kupotosha
Vitengo vya propaganda kwa sasa vipo kazini: hakuna wakati vinatakiwa kufanya kazi kama wakati huu. Propaganda za kupotosha jamii mfano
“Maandamano yamehairishwa,”
“Viongozi wamekamatwa,”
“Maeneo fulani ni hatari.”
" Wanataka kuchafua nchi"
"Wanavuruga amani"
" Wanatumiwa na mabeberu"
" Watanzania ni waoga sana" hii pia ni. Propaganda iliyofanikiwa sana na ambayo kwa sasa watawala huipigia msumari ili iwe ni kama culture ya watanzania
Hii hufanya hata waliokuwa tayari kushiriki wakose maelekezo sahihi na motisha ya pamoja. Kwa mtazamo wa psychological operations (PSYOPS), hii ni silaha ya kisaikolojia inayotawanya umoja wa wanaharakati. Niliwaambia Saikolojia na soshiolojia ni msingi mkuu wa serikali kutawala watu.
Matokeo yake, maandamano hufa kabla ya saa sita mchana, na wale wachache waliotoka hukamatwa bila upinzani. Kisha baadaye watu huanza kulaumiana. Hoo hamjatoka. Nyie waoga n.k.
Kufikia hapa TaikonMaster sina la ziada. Nimejaribu kujadili. Kwa uhalisia na kwa kuzingatia siasa za nchi yetu, Saikolojia ambayo ninaifahamu kwa sehemu, intelijensia ambayo naifahamu kidunchu, na kwa kutumia falsafa (mantiki na hoja).
So kama utakuja kichwa kichwa na kutoa matusi yako sitaingilia uhuru wako na jinsi unavyoelewa mambo.
Nawatakia sikukuu njema ya Nyerere day.
Acha nipumzike sasa.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ninyi mnaojipachika utaalam wa mambo msiyoyajua, usipofanya research usituletee hii takataka. Kwenye maandamano ya Amani siku zote kuna baadhi wanakuja na malengo yao ama kwa kutumiwa na wasioyataka maandamano ama wahalifu rejea maandamano Makubwa ya North London ya mwaka 2011, na maandamano ya mauaji ya Gearge Floyd na Polisi Marekani mwaka 2020.Mdomo mwingi, Mdomo wa mtandaoni ulifanya wasiotaka hiyo kitu wajiandae vyema, Huku ninyi mmebweteka na kuongozwa na hasira ya visasi.
Ukosefu wa mbinu/Plans, mtu hajui aanzie wapi akamalizie wapi jambo ambalo linaondoa uzito wa maana halisi ya maandamano.
Unafiki, Mtu saa moja kaenda kupiga kura, saa nne kaja kijiweni kuponda Watanzania waoga na kwamba hawawezi kuandamana, Saa nane na yeye yupo anakoleza moto kuunguza kituo cha police.
Kutokuweka wazi sababu ya maandamano, No motto, No mabango yenye ujumbe husika, No guidence (Pale mbele wangekuwa watu ambao wana ushawishi wa kuutaka mabadiliko waki-push kwa kuongoza kwa nyimbo na sauti mbalimbali za nini kifanyike)
Kuharibu miundombinu, hapa ndo dhahiri kulifuta meaning nzima na kufanya adui kutumia kama sababu ya kukushughulikia kwamba hayakuwa maandamano bali fujo, Wenzenu mabomu (mashambulizi ya askari) yakizidi kama ni barabarani wanakaa chini. Emagine Watu buku tano mmekaa chini barabarani wanapiga mabomu hamuondoki ni mwendo wa kunawa uso wanamwaga majinya kuwasha mnakaza, Inafika sehemu mnabaki mnaangaliana tu na hakuna anetaka kurudi nyumbani (Mabango yanabaki yanaongea) Na ikitokea wanakaza mnakaa nao hapo hata siku mbili alafu muone kama haki isingepatikana.
Hakuna mtu angepata sababu ya kuua mtu maana lolote lingefanyika kwa sehemu moja yenye watu wengi walikusanyana ingesababisha umoja huo kulidhibiti jeshi na silaha zao sehemu hiyo.
Ni hayo tu niliyoyaona mimi.