Kwanini Lowassa atashinda Uchaguzi Mkuu wa Oct 25

Kwanini Lowassa atashinda Uchaguzi Mkuu wa Oct 25

mchemsho

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
3,230
Reaction score
935
Kilichotokea na kushuhudiwa kwenye kampeni ya leo viwanja vya Gymkhana Bukoba, naamini CCM leo hawalali usingizi..lazima wamechanganyikiwa. Kama ilivyotarajiwa umati ulojitokeza kupindukia ulikuwa gumzo..hakukuwa na malori, ma bus wala hakuna aliyeletwa kwa shuruti kuhudhuria mkutano.

Kilichoshangaza zaidi ni pale Lowassa aliposimama ili aanze kuhutubia...haikuwa hali ya kawaida, umati huo kwa maelfu walipiga makelele ya kushangilia kwa takribani dakika 3, huku Lowasa mwenyewe akijitahidi kuwashusha munkari umati huo. Wengine walisikika wakisema hata usijichoshe kuongea...kwa kweli hamasa ilikuwa kubwa sana. Ni kweli nimeamini maelfu ya watu wana"Mahaba" na Lowassa.

USHAURI WA BURE KWA CCM:

Jumatatu kwenye mkutano wenu, ambao na nyie kama kawaida yenu kuiga mmeuhamishia kwenye viwanja vilvyibatizwa leo "Lowasa Grounds" msitaje jina la Lowassa, wala msitaje neno mabadiliko, MTAUMBUKA.

Kasombeni watu na malori kama kawaida yenu kutoka Kemondo, Katerero, Maruku,hata kutoka Kyaka ili nanyie mjaze UMATI.
Pia msisahau kuleta wasanii wale wakali zaidi ili angalau wakazi wa bukoba waje kushuhudia burudani ya bure.
Mwisho..chonde chonde msizungumzie meli kwasababu mkapa aliahidi mwaka 2000, Kikwete 2005,Kikwete 2010..na mpaka leo bila bila.

Nilikuwa nayasikia tu ila kwa leo nimeamini,

LOWASA IS UNSTOPABLE.
 
💩💩💩💩💩💩💩💩💩💩
 
Wameipata kwenye taarifa ya habari najua hawana hamu lazima wajilaumu kwanini Rais mpendwa walimkata kichwa

sasa amekuwa lulu kwa watanzania kwa kuwa ndiye atakayetukomboa na kutuletea maendeleo kwa kasi.Viva BK, :A S 41:
 
Post picha. Tumuone. Babu mwenye nyota ya kupendwa na kuaminiwa.na umati ws watz.
 
Rais anayesubiria kuapishwa October mwishoni sasa hv anapita kila mkoa kuelezea mabadiliko ya Elimu bure,

matibabu bora, utawala bora, katiba mpya, makazi bora, uchumi imara, maji safi na salama kwa kila mtu,kufuta nafsi

ya wakuu wa wilaya,kilimo cha biashara, michezo juu, maendeleo ya kasi na kenya wajiandae kukosa ya watalii wote

wanaokuja tz wataanza kutua direct KIA na Air Bus ya Tanzania mpya mapema mwakani:A S 41:

lowasa ni nani?
 
jaman msimsababishie preasure baba riz, nape na kinana wasije kufa hata kabla hawajakabizi nchi kwa EL na yule babu bingwa wa matusi anawezajinyonga kabisa mda wowote kuamzia leo maan nilichokiona bk ni ushindi tu kwa Ngoyai asubuhi tuuuu magufuli atakuwa analia tuuuuuu kwa kuukosa upresident
 
Back
Top Bottom