Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Lowassa amesema:
1. Rais Dr. John Pombe Magufuli ndiye aliyemualika Lowassa Ikulu kwakuwa alikuwa na ujumbe wa kumpa.
2. Rais Magufuli alimpa ujumbe Lowassa wa 'kumuomba' arejee CCM na Lowassa alikataa.
3. Yeye Lowassa na Rais Magufuli walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali kama ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ukandamizwaji wa demokrasia na kadhalika.
Kimsingi, taarifa aliyoitoa Lowassa, ikisemwa kuwa ni maelezo aliyoyatoa mbele ya Kamati Kuu ya chama chake-CHADEMA inaleta sintofahamu kuhusu nini hasa kilijiri kabla, wakati na baada ya Lowassa kwenda na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.
Taarifa ya Lowassa inatofautiana waziwazi na hata video zilizooneshwa siku alipomtembelea Rais Ikulu na Rais Magufuli pamoja na Lowassa mwenyewe kutoa muktasari wa kilichojiri. Taarifa ya Lowassa ilipaswa kujibiwa kwakuwa ni yeye mwenyewe aliyeamua kuanika vya sirini.
Kwanini Kurugenzi ya Habari-Ikulu imekaa kimya badala ya kufafanua kuhusu kilichosemwa na Lowassa? Je, ni kweli Mhe. Rais ndiye aliyemualika Lowassa Ikulu? Je, ni kweli Mhe. Rais alimuomba Lowassa arejee CCM na Lowassa alikataa? Na kadhalika na kadhalika.
Kisheria, kukaa kimya (hata wakati wa kusomewa mashtaka mahakamani) ni kusema HAPANA/SI KWELI. Kijamii, kukaa kimya ni kusema NDIYO/NI KWELI. Tushike lipi hapo?