Kombo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,812
- 509
Njaa ya wakati wa Mwalimu ilisababishwa zaidi na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wa Serikali (Ukame, Viwavi jeshi,teknolojia duni, uwekezaji duni nk.), Njaa ya zama hizi inasababishwa na UVIVU wa kufikiri miongoni mwa Viongozi wetu. Utafiti umekua sana zama hizi ingawa hautumiki ipasavyo, uwekezaji katika kilimo umeongezeka lakini bila malengo yanaoeleweka na bila umakini wa utekelezaji. Tumesikia kwamba Serikali ilipeleka vocha za mbegu za mahindi mkoani Singida katika msimu uliopita wa Kilimo, uongozi wa Mkoa ulizikataa vocha hizo na kuahidi kuzirudisha Wizarani kwa kuwa Mahindi si zao la kipaumbele kutokana na hali ya hewa ya Mkoa huo. Hii ina maana kuwa kuna watu Serikalini hawajui lolote kuhusu umuhimu wa tafiti katika kilimo au wanaendekeza mazoea. Hatuwezi kukwepa njaa katika hali kama hii.