Kwanini kuna Njaa Tanzania kama wakati wa Nyerere?

Njaa ya wakati wa Mwalimu ilisababishwa zaidi na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wa Serikali (Ukame, Viwavi jeshi,teknolojia duni, uwekezaji duni nk.), Njaa ya zama hizi inasababishwa na UVIVU wa kufikiri miongoni mwa Viongozi wetu. Utafiti umekua sana zama hizi ingawa hautumiki ipasavyo, uwekezaji katika kilimo umeongezeka lakini bila malengo yanaoeleweka na bila umakini wa utekelezaji. Tumesikia kwamba Serikali ilipeleka vocha za mbegu za mahindi mkoani Singida katika msimu uliopita wa Kilimo, uongozi wa Mkoa ulizikataa vocha hizo na kuahidi kuzirudisha Wizarani kwa kuwa Mahindi si zao la kipaumbele kutokana na hali ya hewa ya Mkoa huo. Hii ina maana kuwa kuna watu Serikalini hawajui lolote kuhusu umuhimu wa tafiti katika kilimo au wanaendekeza mazoea. Hatuwezi kukwepa njaa katika hali kama hii.
 
MAJIBU:
Wakati wa Nyerere kulikuwa na msemo "KILIMO cha KUFA NA KUPONA!" watu wakafa njaa...
Wakati wa Kikwete kumekuwepo "KILIMO KWANZA" haitazuia watu kufa njaa...

SABABU:
Makosa ya WATANZANIA na SERIKALI ya TANZANIA ni kutojua nini maana ya UWEKEZAJI katika KILIMO. Na pia kutofahamu ama kufanya kusudi katika MIRADI YA KILIMO. Na kwa hili nadhani bado kuna mchango mkubwa wa kuendelea kuagiza chakula duni na kisichotosha kutoka nje ya nchi kwa sababu ambazo sijazielewa vema.

Ndio maana kukiwa na mvua WAKULIMA hupewa mbegu mbovu!
Kukiwa hakuna mvua wakulima hukopeshwa TILA!!
Katika hilo nadhani ni mtindo wa kuonesha dunia kuwa WATANZANIA hawawezi kulima...
Hivyo basi MAKABAILA waje WALIME ili tupate chakula cha kutosha!!

SERA:
Sera ya kilimo kote duniani kinakofanywa kilimo, kwanza ni kusogeza maji karibu na wanaofanya kilimo. Hili kwa Tanzania ni hadithi!!
watanzania kwanza wangeliangalia Libya iliwezaje kuwekeza maji jangwani na kilimo kikaanza. ama tuitazame Zimbabwe iliyokuwa ikilima kabla haijaiga sera ya kilimo ya Tanzania!

Kwa kifupi TANZANIA na NJAA, MARADHI, UJINGA na UISADI ni ndugu wa damu.
 
Uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu unaweza kuwa sababu ama kutopenda kuwajibika kwao. Pia kumbuka kuwa rushwa siku zote ni adui wa haki. Njaa ya Tanzania kwa miaka hii ni ya kujitakia tu. Kilimo kwanza ni nini? eti mapinduzi ya kijani? Mfano, chukua Bilioni 70 kama hizo za rada...nunua matrekta kisha sambaza katika mikoa yote ya kusini kwa kuunda vikundi, wakopeshe wakulima hao matrekta hayo kwa miaka 5 tu. Kuna njaa bado?
 
Nyumba mbovu hutokana na msingi wake. hivyo basi nyumba hiyo ivunjwe na kujengwa upya.
Hapa tuwekane sawa kwanza, na tutazame kwanini kilimo cha Tanzania hakina tija na njaa imepiga kambi ya kudumu!
WAKATI WA MJERUMANI, WATANZANIA WALILIMA KWELIKWELI! TENA WALILIMA MAZAO AINA ZOTE YA CHAKULA NA BIASHARA.
WALILIMA KWA NGUVU NA KWA HIYARI, HAKUKUWEPO SABABU ZA WATU KUFA NJAA. WAKATI WA MWINGEREZA ZILIANZA SIASA ZA BALAA LA NZIGE N.K. HIVYO BASI MISINGI MIBOVU ILIYOACHWA NA MKOLONI MWINGEREZA KUHUSU KILIMO ILIRITHIWA!! Hapa sihitajii kusema sana mengi yanaeleweka yaliyotokea na kutukia!!!
Tulipopata uhuru tulirithi utamaduni wa Mwingereza (KILIMO CHA MAKABAILA) na walikuwepo mamwinyi wenye viunga vya minazi huko pwani, kwingineko kote mazao yaliyozingatiwa yalikuwa ya kibiashara na si chakula. (Watanzania wakawa na utamaduni wa kutokuwa na ghala za vyakula vya kutosha bali chakula kichache na baadhi ya mifugo au mazao ya biashara ya kubadilishia ili wapate chakula) ndio maana mpaka leo wengi wetu tungali tukinunua kilo moja moja ama robokilo, badala ya kununua chakula cha kutosha walau wiki moja. (yaweza semwa sababu ni umaskini nasema la hasha kwa sababu hata wale wenye kipato cha kati NDIVYO TULIVYO!) NI UTAMADUNI.
Awali nimeelezea kwanini na kuna mada niliweka "FUMBO GUMU.." inahusisha kwanini "HATULIMI"
Na wala haishangazi kufika nyumbani kwa mtu mwenye eneo kubwa hana hata bustani ndogo ya mboga achilia mbali maua!
Hainishangazi kabisa, kuona mtu mwaka mzima ananunua mboga na matunda ambayo angalau angeliweza kupata nyumbani kwake angalau kwa msimu mmoja!
IKIWA NCHI HII KWELI INAHITAJI KILIMO KIWE UTI WA MGONGO, BASI KWANZA WATAFITIWE WATAALAMU WA KILIMO NA VIONGOZI WAO. ILI TATIZO LIBAINIKE NA KUPATIWA UFUMBUZI!! YAWEZEKANA KUNA MAMBO MAWILI:
1. KAMA WATAALAMU WENYEWE WA KILIMO SI TATIZO NA KIKWAZO CHA KILIMO..
2. BASI WATAWALA WANAWEZA KUWA NDILO GAMBA LENYEWE KATIKA KILIMO.. LIGANDULIWE!!

CHA MSINGI NI KUWA KILIMO KILISHATOKA DAMUNI KWA WATANZANIA SIKU NYINGI!
WALIJENGA VYAMA VYA USHIRIKA VIKAFISIDIWA..
WALILIMA HAKUKUWA NA TIJA!

WATANZANIA WAMESHAKUWA WACHUUZI SIKU HIZI NDIO MAANA KILA ANAEJENGA NYUMBA ANAWEKA sEHEMU YA DUKA!!!
 
Kanisa katolliki limeshidwa kuongoza tanzania sera zao zimeoza kazi kujisifu school zetu ni za kwanza sasa faida yake ni ipi ikiwa wameshidwa kuleta sera za shiba.
 
Tangu Slogan ya Kilimo kwanza ilipoanzishwa Tanzania imekuwa ikikumbwa na njaa kila mwaka hadi kuna wakati unasema labda hii slogan imekuja kuzidisha njaa badala ya kupunguza au kuondoa kabisa. Huwa najiuliza hivi mafanikio ya Kilimo kwanza yanapimwaje? Kama yangelikuwa yanapimwa hata kwa njaa kupungua ingekuwa afadhali lakini wapi hakuna hata mtu mmoja amewahi kutaja mafanikio yake!
 
Mwanakijiji unajua ni mchokozi sana! Unawaambia watu ukweli na watu wako busy kutuhakikishai kuwa Nyerere si lolote wala sio chochote. Jinsi ninavyoona leo hii kuna njaa kubwa sana kuliko enzi za Nyerere pamoja na kuruhusu mfumo huru wa uchumi. Hatuna visionary leaders....tuna wapiga midomo tu kama walima minazi wa kule kwetu Rufiji wakishakunywa ile pombe inaitwa mnazi.
 
Hii post imewekwa kwa CHUKI za UDINI.

Mimi sijui kama Kanisa Katoliki ndio linaendesha nchi hii, kwa kutokea wa kwanza; sio uongo; ila sioni kabisa connectivity. Let us be moderate and objective

Kanisa katolliki limeshidwa kuongoza tanzania sera zao zimeoza kazi kujisifu school zetu ni za kwanza sasa faida yake ni ipi ikiwa wameshidwa kuleta sera za shiba.
 
Mwanakijiji unajua ni mchokozi sana! Unawaambia watu ukweli na watu wako busy kutuhakikishai kuwa Nyerere si lolote wala sio chochote. Jinsi ninavyoona leo hii kuna njaa kubwa sana kuliko enzi za Nyerere pamoja na kuruhusu mfumo huru wa uchumi. Hatuna visionary leaders....tuna wapiga midomo tu kama walima minazi wa kule kwetu Rufiji wakishakunywa ile pombe inaitwa mnazi.

Ndugu Tangawizi

Mimi sipishani na wewe kwamba 'quality' ya uongozi ina suasua. Ila pia, sikubaliani na kusafishwa kwa failed Arusha Declaration and Nyerere's Economic Policies.

La msingi nitakalokuambia, tena unalijua na kila mwana forum analijua; ni kwamba viongozi wa leo ni products za Mwalimu na utawala wake. Awamu ya pili na ya tatu were largely his own. Na hii ya nne ni muendelezo.

Utendaji wa Serikali umekuwa mara nyingi unategemea mambo yazuke ndio yashughulikiwe. Serikali inafanya kazi kama zima moto. Mipango Mkakati imo kwenye MAKABRASHA, haifanyiwi kazi, hio ni sawa na kutokuwa na mpango. Watendaji wanatekeleza wanayoona yana maslahi nao. Hivyo mipango haitekelezwi. Ndio maana unamuona Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu ya Serikali anahoji; fedha inapelekwa kwenye Serikali za mitaa ili zitekeleze miradi ya maendeleo ya wananchi na mwaka unamalizika; zilizotumika ni chini ya asilimia ishirini. Kukosa kuwa na mipango madhubuti ni uzembe; wadhungu wanasema 'Fail to Plan is the same as Plan to Fail'; hatutoweza kufika kwa design hii. Kuna yale maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma. Pale, ili taasisi au Wizara iwe imetimiza masharti ya ushiriki; miongoni mwa yanayohitajika ni kuwa na Mpango wa Utekelezaji. Watu wanapeleka ma-document. Wakuu wa hizo taasisi [wakurugenzi watendaji, ma-kamishna na makatibu wakuu] wanajiita watendaji, ilhali hawasimamii mipango hiyo ya utendaji kwa umakini unaostahili. Na wanageuka Miungu Watu. Watumishi wa Kawaida, kama maafisa na maafisa wasaidizi wanawekwa katika hali za unyonge. Haki zao wananyimwa na kwa wale wanaobahatika kupewa; lazima ziwe zimechelewa.

Watumishi wenye uwezo, uzoefu na utaalamu wanajiondokea. Wanaobaki, inakuwa wengi wao hawana uwezo. Wanakuja kukabidhiwa nafasi za dhamana, wanakwenda kujadiliana mambo ya Kimataifa na Kikanda na wenzao Mahiri. Hawawezi kulingana nao. Alafu tunakaa na kuuliza kwa nini? Tena huu ududu umerithiwa tangu zama za Saint Julius Nyerere.

In short.

Serikali inapaswa kuweka utendaji wake wazi.
Inapaswa kusimamia mipango yake kwa ukamilifu, sio mipango iwepo tu.
Kanuni za utumishi wa Umma inastahili zifuatwe kwa umakini unaostahili, pasiwe na kubaguana kwa misingi yeyote ile iwe ya Dini, Ukabila wala jengine. Wanaoleta chokochoko washughulikiwe.
Viongozi wasitekeleza mipango yao wawajibishwe, sio waone ufahari kuwa na majina makubwa na kupata stahili ambazo wanapwaya. Ikumbukwe UONGOZI ni DHAMANA.
Utaratibu wa kuteua mawaziri waliochakachua VYETI vya ELIMU ukemewe na UKOME. Kama mtu amechakachua elimu yake atashindwa kuchakachua nchi?

Mie nakaribia kutoka machozi kwa kusikitikia tulipofikia.

Utasema Nchii ilikuwa haijakaliwa na Wakoloni.
 
Macho ya nje yanatudanganya!
mapenzi mara nyingi huuficha ukweli!
HATUTAKI KUAMBIANA UKWELI, LAKINI NJAA IKICHACHAMAA KABISA HAKUNA AMBAE ATASUBIRI AAMBIWE,
KILA MMOJA ATAACHANA NA SIASA NA KUUJUA WAJIBU WAKE!!

Waswahili waliposema MCHUMA JANGA HULA NA WAKWAO je hamkuwaelewa?
Je hakuna asiejua kwamba TULICHUMA JANGA MWAKA 1967? na ilipotimia mwaka 1971-72 tukaanza kuguguna mihogo?
Je tumesahau ilipofika mwaka 1974 nani hajui ilibidi HIMIZO la KILIMO litolewe "CHA KUFA NA KUPONA!" nani ambae hakumbuki miaka iliyofuata watu wakikimbizana kwenye maduka ya ushirika kugombea mkate wao wa siku? nani amesahau ilipofika miaka ya themanini watu walivyokimbizana ma magari ya ugawaji na kupanga foleni za mawe kwenye maduka ya kaya? Je nani hajui wakati wa Mzee Ruksa kilichotokea mikoa ya kusini? Watu mpaka wakafa kwa kula matunda mwitu? Je nani hajui wakati wa Mzee Ben yaliyotokea Same, Loliondo na kwingineko? NJAA NA TANZANIA... TANZANIA NA NJAA!!! UDUGU WA KUFA NA KUZIKANA!!
JE NI UBAYA WA TAWALA PEKEE ULIOCHANGIA NA KUCHAGIZA HALI ZILE?
UKITAZAMA UPANDE WA PILI WA SHILINGI, (Achana na sera mbovu za serikali na ubovu wa wanasiasa tulionao.)
WATANZANIA TU WAVIVU WA KAZI NA KUFIKIRI KUPINDUKIA. TUNATAKA KILA JAMBO TUFANYIWE. tunahitaji viboko ili tufanye kazi kama ilivokuwa kwa mkoloni wa kijerumani!
TUNAHITAJI UTAWALA MPYA USIOHITAJI KUCHEKEANA, KUBEBANA WALA KUBEMBELEZANA.
TUNAHITAJI SERA MPYA ZENYE MALENGO KWA TAIFA.
TUNAHITAJI TAFITI NZURI NA ZENYE KUTELELEZEKA NA SI ZILE ZA KUWEKWA MAKABATINI KWA AJILI YA KUOMBEA MISAADA KWA WAFADHILI.
HUU SI WAKATI WA KUSIFIANA KWA UPUUZI WETU WALA KUSHANGILIANA KWA SABABU YA KUFANANA WETU...
TUJITOLEE MIOYO YETU KWA AJILI YA TAIFA LETU.
 
WANASIASA WETU WAMESAHAU WAJIBU WAO, NASI TUMEJISAHAU NA KUWATEGEMEA WAO!
WANASIASA WETU WAMEJIKITA MIJINI, KAMA ILIVYO KWA WATAALAMU WETU WA KILIMO!
NA KWA MFUMO HUO WA KUJIHIMIZA KUFANYA KILIMO TUKIWA MAOFISINI TUTARAJIE KUSIWE NA NJAA!!
ALINACHA!

wacheni njaa itucharaze... utapiamlo ukomae katika bongo za watoto wetu!
ili tuendelee kutawaliwa na wao milele :-(

Wacheni tuendeleze ushabiki wa kisiasa kwa namna zote tujuazo na mbinu zetu nyinginezo...
mwisho wa siku litazama tutagawana mbao!
 
Huwezi kuwa na Madini Nchini, walaofaidi mirahaba ni Stewart Asseyyers.
Huwezi kuwa na Mikataba mibovu kila pahala, TICTS, RADA, RICHMOND; u name them; ukawa ni sawa;
Mbunge anaewawakilisha wa Tanzania kwa mwaka anakula Zahanati 6 za walipa kodi, wavuja jasho; anaowawakilisha;
Waziri anajiita Daktari wa falsafa, digrii ya kwanza kapenya kwa manati;
Waziri Mkuu anatoa kauli za ushabiki wa hisia bungeni; anapoambiwa ukweli analia;
Lakini yoote haya ni muendelezo, Awamu ya kwanza, Awamu ya Pili mpaka sasa.

Tumefanywa kuamini kwamba ukiwa mhudumu hotelini/mgahawani, akija mtu kutaka huduma; analeta ubwanyenye; ndio unaotupelekea kuchukia kuchukia kutoa huduma kwa ufanisi; maeneo yote yamekamatwa na watani zetu wa jadi.

Kinachohitajika, HAWA WAZEE WAISHIE ZAO. AKAMATE MTU kama atakua mkongwe sana awe na 50 years. Iundwe safu ya vijana, ambao wana uchungu, wazee wanasubiri kujifia tu.

Adabu hakuna siku hizi. Watu wanaiba kila pahali. Benki, mashule mpaka wahudu wa baa.
 
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUSAFIRISHA CHAKULA NJE!

From LEONARD MWAKALEBELA in Dodoma, 6th July 2011 @ 15:00, Total Comments: 0, Hits: 279

THE government has banned export of food crops for six months effective July 1, to prevent the spread of famine in many parts of the country.

The Minister for Agriculture, Food Security and Co-operatives, Prof Jumanne Maghembe told the National Assembly on Wednesday that "generally there is food surplus" in the country, but pockets of famine existed in 48 districts.

The minister said the government has revoked all permits for transportation of food crops outside the country.

"The objectives of these measures are to give the government ample time to assess availability of food to ensure food security in the country.

"The government invites neighbouring countries facing famine to negotiate directly with the government and buy food under international arrangements instead of informal cross-border trade," he said.

The minister said smuggling of food to neighbouring countries was now rampant and the pace of illegal exports, especially of cereals was a threat to food security.

Prof Maghembe said the latest report of the Food and Agriculture Organisation (FAO) shows food production globally has declined by 1.2 per cent and that 30 countries, mostly in sub-Saharan Africa, would face severe shortage.

He named neighbouring countries facing famine as Burundi, Somalia, Kenya, Uganda, the Democratic Republic of Congo (DRC), Sudan, Madagascar and Mozambique.

"Maize price in Nairobi has gone up from 215 US dollars per tonne (323/- per kg) in January to 465 US dollars per tonne (744/- per kg) in June 2011, reflecting a rise by 130 per cent.

"The Kenya has announced decline in food production by 1.3 million tonnes. This situation has fuelled smuggling of food crops, especially cereals to experiencing shortage," the minister explained.

Prof Maghembe said a preliminary assessment had revealed that there was food surplus in seven regions namely, Rukwa, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Kigoma, Mtwara and Kagera.

The assessment also indicates that eight regions of Morogoro, Lindi, Tanga, Dodoma, Singida, Tabora, Kilimanjaro and Manyara have sufficient food, while Mwanza, Shinyanga, Mara, Arusha, Coast and Dar es Salaam regions were facing deficit.

"During the 2010/11 season, production of cereals is projected to reach 6.78 million tonnes, against 7.2 million tonnes demand, thus a deficit of 413,740 tonnes.

"Production of non-cereal food during the same period is expected to reach 6.02 million tonnes, 4.3 million tonnes demand, thus a surplus of 1.7 million tonnes. So, generally, there's food surplus," he assured Tanzanians.

Non-cereal food include legumes, potatoes, cassava and banana. Prof Maghembe, however, said that due to the fact that most Tanzanians use cereals as their staple food, there was automatically food shortage.

He urged Tanzanians to use the available food sparingly. The preliminary assessment shows that there is food deficit in 48 districts in 16 regions.

The minister said that the government had distributed over 30,301 tonnes of relief food out 36,970 tonnes allocated for areas facing food shortage.

"The National Food Reserve Agency (NFRA) is offloading 115,000 tonnes from its centres in Makambako, Sumbawanga and Songea to its godowns closer to needy areas.

"The agency also continues to offload 50,000 tonnes to millers in 13 regions to reduce prices of maize," Prof Maghembe stated when announcing measures to address food shortage.

Up to last month, 35,334 tonnes was offloaded in such arrangement.
 
Back
Top Bottom