Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,146
Mjadala wa uhalali na umuhimu wa kitambulisho cha Ujasiriamali umeibuka upya baada ya Lissu kukikosoa vikali na hapo hapo Magufuli kukitetea kwa nguvu zote.
Kuna maswali ya msingi ya kuhoji na kutafakari. Kwa mfano;
1. Kwanini kitambulisho kiuzwe elfu 20, badala ya kutolewa bure?
(Kama kitambulisho cha mpiga kura na NIDA kinatolewa bure, kwanini cha ujasiriamali kiuzwe?)
2. Kwanini malipo ya kukinunua hayana risiti, wakati sheria za serikali zinataka malipo yote halali yaendane na kutoa risiti?
3. Kwanini kitambulisho hakina jina, picha wala anwani ya mhusika anayekimiliki?
(Nini mantiki ya kumiliki kitambulisho ambacho hakikutambulishi wewe unayekimili?)