Kwanini kitambulisho cha taifa kina muda wa kuisha matumizi

Hiyo option haipo TRA Millenium Tower Kijitonyama? Mbona nimewaambia mara 2 lakini sikupigwa picha mpya?
Mkuu narudia tena pengine wewe ndio hufahamu.
Ukitaka kuhuisha leseni yako iliyoisha muda wake, wakati unaenda TRA kuna option ya kupiga picha upya.

Unawaambia tu nataka kubadili Picha, unaenda wanakupiga nyingine leseni yako mpya ikitoka inakuwa na picha yako currently.

Je, ulishajaribu kufanya hivyo ikashindikana?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ninafahamu hasa kwenye leseni.
Mfano mimi leseni yangu kwa mara ya kwanza niliipata 2004 (picha za kubandika ilikuwa kipindi hiki), nikiwa na miaka 20.
Nimeshaibadili mara kadhaa kwa kupiga picha upya, tena imekuwa rahisi kwasababu ya mfumo uliopo sasa hivi.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Asante sana kwa ushahidi
 
Vitambulisho vyote hivyo ni vile vyakirapeli vya mwanzo mudawake ukiisha utapewa Kama changu hakina expire date
 
Hiyo option haipo TRA Millenium Tower Kijitonyama? Mbona nimewaambia mara 2 lakini sikupigwa picha mpya?
Wameamua tu kukunyima.
Ila ni kitu kinachowezekana!!
Kwani huwa wanakupa sababu gani?

Japo ni rahisi zaidi kwa Makao makuu ya Mkoa.
Sijui kwa Dar uko Mkoa gani wa kiTRA

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Leseni za madereva wa eSwatini/Swaziland hazina muda wa kwisha matumizi kwa taarifa yako. Kwa hiyo usiseme haiwezekani.
Mbona unapuyanga!!!??? Tunazungumzia Tanzania, Eswatin inakujaje!!!?? Kwahiyo unatushauri tuhamie Eswatin?
 
Acha uji=ga na wewe. Mtu kasema haiwezekani. Mimi nikasema inawezekana. Ni suala la kuamua tu. Nikatoa mfano wa eSwatini. Wewe unaongelea kuhamia eSwatini!! Jihurumie ulivyonyimwa uwezo wa kufikiri.
Mbona unapuyanga!!!??? Tunazungumzia Tanzania, Eswatin inakujaje!!!?? Kwahiyo unatushauri tuhamie Eswatin?
 
Vitambulisho vyetu vya utaifa vimewekewa mda wa kuisha serikali imemaanisha nini kuweka ukomo wa kitambulisho au ni njia ya upigaji ambao umezoeleka.

Serikali ililenga nini kutupa vitambulisho vya aina hiyo kwa hiyo kikisha mda nitengenezewe kingine, mimi nachofahamu taarifa zangu hakuna mtu mwingine atakayezitumia hadi naondoka duniani iweje kuwepo ukomo wa kitambulisho hicho.

watanzania waliowengi hawajapata vitambulisho vya utaifa wengi wao wana namba za vitambulisho hivyo sasa hii naona kama haijakaa sawa hata kidogo!

Tunajuwa kuwa kunakufariki je hivi ni vigezo walivyoona vinafaa kuweka ukomo wa vitambulisho hivyo?

Mimi maswala ya vitambulisho hivi kuwa na mda wa kuisha bado sinauelewa wakutosheleza naomba wajuzi wanifafanulie kwani kuuliza siyo dhambi.
 
Back
Top Bottom