Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Inaonyesha unajua vitu mkuu Kwann usivianzishie uzi humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleweka vyema mkuu endelea za izo injili mbili zilizobaki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kuulize kwenye Biblia kuna kitabu cha Eliya au Meshack/Mishael ? nimekutolea mfano tu, maneno/kauli za hawa watu zimenukuliwa kwenye Biblia na wako wengi wa aina yao ambao kauli zao ni sehemu ya Maandiko Matakatifu kwa kuwa Mungu aliwatumia kuwafikia wanadamu.

Wewe unaona nini cha ajabu kauli ya Enock/Henoko kunukuliwa katika Biblia? Au kinacho kusumbua ni kwa vile hii ya Henoko imenukuliwa kutoka katika hicho kitabu chake?

Hilo la kusema nimemchukulia Enock kirahisi ni lako. Tafuta posti zangu kwenye huu uzi, labda hukunielewa wala sishangai maana wako ambao wana malengo sawa na yule muovo. Kuna posti, na hapa nakurahisishia, Henoko, Melkizedeki, Eliya wana uniqueness zao kama walivyoelezewa na Biblia,hawa si wakawaida.


Na washawasha!


 
Biblia ni nini na ilitoka wapi?

Wakati wa mitume walikuwa wanawafundisha watu kwa kutumia nini?


Wewe naona unaendelea kushupaza shingo bado hujakubali tu kuwa huwezi kupotasha Neno la Mungu? Mungu ni mtaratibu sana katika kuchukua maamuzi/hatua, huwapa wanadamu muda wa kutosha kujitafakari ili wajisahihishe/watubu na kuacha njia zao za upotevu.


Na washawasha!
 
Kwanza,ni wapi Eliya amenukuliwa kwenye Biblia na amenukuliwa na nani?

Pili,nilichokifanya mimi ni kukuonesha kuwa kuna kitabu cha Enoch na kimenukuliwa na mitume wa Yesu na maneno hayo yapo ndani ya Biblia unayoamini wewe ni neno la Mungu 100% na jambo hili linayafanya maneno ya Enoch kuwa ni maneno ya Mungu,hili hulielewi kwasababu gani?

Hakuna kinachonisumbua mimi isipokuwa kipo kinachokusumbua wewe na unahamisha jambo hili liwe kwangu.Lakini nimeelewa pia hili linatokana na nini maana mara nyingi kisaikolojia huwa ipo hivi....

Kitabu cha Enoch ambacho wewe unakipuuza,binadamu unayeishi miaka zaidi ya 6000 baada ya kuishi Enoch,yupo mtu aliyeishi miaka zaidi ya 4000 baada ya Enoch na ni mwanafunzi wa Yesu ambaye anamfahamu Enoch kuliko hata Enoch mwenyewe alivyojifahamu na amenukuu maneno yake...

Ajabu kabisa ni kwamba wewe unayakubali aliyoandika Yuda lakini hutaki yale ambayo Yuda aliyanukuu na yapo miongoni mwa hayo unayoyaamini wewe....

Kituko cha karne hiki....
 
Nimekuuliza biblia ilitoka wapi,hujajibu na unaniambia nataka kupotosha neno la Mungu....

Nikakuuliza tena,wakati wa mitume,walikuwa wanakwenda kuwafundisha watukwa kutumia nini,jibu ni lile lile,napotosha au nataka kupotosha neno la Mungu....

Nataka kupotosha namna gani wakati ninataka nijue ujuacho juu ya namna biblia ilivyopatikana?

Napotosha namna ipi wakati nataka kujua Mtume Paulo kwa mfano,wakati anakwenda Rumi alikwenda na nini ili akawafundishe Warumi?

Unapoulizwa swali halafu ukaacha swali na kujitungia majibu yako ni dalili ya kushindwa hoja.....

Jikite kwenye swali kisha ulijibu siyo kujitungia mambo ambayo hata hayapo kwenye maelezo yangu....
 
Kwa kusema haya ndio umejibu swali uliloulizwa?maana hapa tunawafuatilia kwa makini tujue ukweli upi tuufate na sio kurukaruka na kupindisha uhalisia, kwa kifupi naomba ujibu swali uliloulizwa kama muungwana la sivyo utaonekana hujui unachodhani unajua.
 
Kwa nini unasema nimempuuza Henoko? Hujui kuhusu Eliya katika Biblia? Je kiko kitabu kinaitwa Eliya katika Biblia?

Sasa kwa nini kulazimisha kuwa kitabu kizima cha Henoko kuwa kati ya vitabu vya Biblia kwa vile kanukuliwa na Yuda mistari ambayo iko kwenye kitabu chake? Hayo mengine yaliyo katika kitabu cha Henoko ya faa kuwa katika maneno ya Mungu yaani Biblia?

Je kunukuliwa kwa mistari miwili na Yuda kutoka kitabu cha Henoko kwa halalisha vipi kitabu kizima cha Henoko kuwa sehemu ya vitabu vya Biblia?


Na washawasha!

 

Kwa mawazo yako unafikiri nimefanya nini? Au unapenda kusikia unachotaka kusikia?


Na washawasha!
 
Kwa nini unasema nimempuuza Henoko?
Kwasababu unadharau kitabu alichoandika...
Hujui kuhusu Eliya katika Biblia?
Nilikuuliza hivi "Ni wapi Eliya amenukuliwa kwenye biblia na kanukuliwa na nani"?,hili swali langu nilitarajia utalijibu kwa kunionesha mahali Eliya aliponukuliwa na unioneshe ni akina nani maana ulinipa mfano kwa kuniuliza kuhusu Eliya kwasababu mjadala wetu hapa ni Yuda kumnukuu Enoch na kwenye biblia sijawahi kuona mahali mwanafunzi wa Yesu au Yesu mwenyewe au mwingine yoyote akimnukuu Eliya ili ionekane aliwahi kuandika chochote....

Enoch na Eliya wameonekana kwenye Biblia kama character ambao walikuwa wakizungumziwa na waandishi wa Biblia lakini Enoch akaenda mbele zaidi kwa kuandika kitabu pia kama ilivyo kwa Musa.Musa ni character lakini pia ni mwandishi....

kinachotokea hapa ni sawa na vitabu vya Musa visingekuwepo kwenye biblia halafu akina Habakuki au Yohana wamnukuu,ni lazima watu wangezingatia maadniko ya Musa hata kama yasingekuwa kwenye biblia...

Enoch aliandika kitabu lakini Eliya hakuandika,unaponitolea mfano wa Eliya mfano wako unakuwa mfu.....
Je kiko kitabu kinaitwa Eliya katika Biblia?
Hakuna,so what?
Wewe hunielewi kabisa na hili ni tatizo kubwa.Ninakusaidia kuelewa kimantiki umuhimu wa kitabu cha Enoch kinyume na wewe na wengine mnavyokiona kitabu hiki kuwa hakifai kabisa....

Ninachotaka ukione hapa ni umuhimu wa sehemu ya maandiko yake kuwepo kwenye biblia ambayo wewe unaona ni neno la Mungu,ni kwanini mistari miwili tu ya Enoch iwe ni neno la Mungu na siyo maneno yake yote ya kwenye kitabu chake?

Bila ubishi ni kwamba wanafunzi wa Yesu walijua na walikisoma kitabu cha Enoch na ndiyo maana Yuda alisema "Kama vile Enock,mtu wa saba kutoka Adam alitoa unabii kuhusu.....",hii inaonesha kuwa alijua kuhusu maandiko ya Enoch na aliyasoma,ni kwanini wewe leo usikisome na kukizingatia?

Au wewe unaelewa zaidi ya Yuda mwanafunzi wa Yesu?

Kimsingi ni kwamba wanaokipinga hiki kitabu wanasumbuliwa na hofu tu za kimapokeo hakuna cha zaidi.....
 
1. Kutokudharau kitabu cha Henoko ni kutaka kitabu kizima kiwe sehemu ya Biblia?

2. Maandiko yaliyo katika Biblia kuhusu Eliya aliyandika Eliya mwenye? au kuna maana nyengine ya kunukuu?

3. Ni kweli sikuelewi katika hii agenda yako (yenu) ya Biblia kuchakachuliwa eti kuna vitabu kikiwemo cha Henoko vimeondolewa. Kwa nini husemi/hamsemi kwa undani sababu za kuondolewa hivi vitabu?

Hivi unajua kuwa si Mambo yote aliyo ya sema na kuyafanya Bwana Yesu (Mungu mwenyewe) hapa duniani yamo/kuandikwa katika Biblia/ Maandiko Matakatifu ya Mungu, sembuse kitabu cha Henoko? Mungu akusaidie.


Na washawasha!

 
1. Kutokudharau kitabu cha Henoko ni kutaka kitabu kizima kiwe sehemu ya Biblia?
Inaonekana hunuielewi na zaidi sana huelewi unachokiandika...

Hapa chini tu umeandika sisi tuna mpango wa kutaka biblia ichakachuliwe,hii unalenga kukosoa kwetu kwa kutokujumuishwa kwa kitabu cha Enoch kwenye vitabu vinavyounda biblia,kwa dhana yako hii ni kwamba unaona kitabu cha Enoch hakina sifa ya kuwemo na ndiyo maana unasema tunataka ichakachuliwe...

Wakati huo huo,Yuda ambaye ni mwanafunzi wa Yesu alimnukuu Enoch kwa kujua aliandika maneno ya Mungu,na maneno hayo hayo aliyoyanukuu Yuda unayaona ni maneno ya Mungu lakini mengine siyo...

Siyo dharau hiyo?

Au huelewi hata unaandika kitu gani?
2. Maandiko yaliyo katika Biblia kuhusu Eliya aliyandika Eliya mwenye? au kuna maana nyengine ya kunukuu?
Kwenye biblia kuna maelezo yaliyoandikwa na wengine yakielezea aliyotenda Eliya,hakuna mahali Eliya amenukuliwa kuwa ameandika chochote,hii ndiyo tofauti kati ya Eliya na Enoch...
3. Ni kweli sikuelewi katika hii agenda yako (yenu) ya Biblia kuchakachuliwa eti kuna vitabu kikiwemo cha Henoko vimeondolewa. Kwa nini husemi/hamsemi kwa undani sababu za kuondolewa hivi vitabu?
Hakuna aliyesema kitabu cha Enoch kimeondolewa kwenye biblia bali hakijajumuishwa kwenye mjumuiko wa vitabu vinavyounda biblia,elewa tofauti hii na itakusaidia...

Pia,nilikuuliza,unaelewa biblia ilitoka wapi na nani aliifanya iwe kama ilivyo? Nikakuuliza pia,akina Paulo walipokuwa wanafundisha walikuwa wanafundisha kwa kutumia nini? Au hawakutumia chochote?

Ukijibu maswali haya utapata mwanga wa kuanza kuelewa juu ya hiki ninachokueleza hapa....
Hivi unajua kuwa si Mambo yote aliyo ya sema na kuyafanya Bwana Yesu (Mungu mwenyewe) hapa duniani yamo/kuandikwa katika Biblia/ Maandiko Matakatifu ya Mungu, sembuse kitabu cha Henoko? Mungu akusaidie.


Na washawasha!
Unaelewa kuwa haya maelezo yako yanafanya uendelee kuonekana wa ajabu kwa kukataa kitabu cha Enoch?

Kwasababu,kama tu kuna mambo ambayo alitenda Yesu na hayakuandikwa,huwezi kufikiria tu kuwa kuna vitabu viliachwa na waliokusanya vitabu vinavyojumuisha biblia na viulitakiwa viwepo?

Halafu pia,akija mtu akikueleza kuwa jambo fulani Yesu aliagiza lakini halikuandikwa kwenye biblia,utakubali?

Kama ni hapana,ni kwanini hutakubali wakati umesema mwenyewe na kwenye biblia pameandikwa kuwa kuna mengine aliyatenda Yesu na hayajaandikwa?

Kama ni ndiyo,unatumia kipimo kipi kuyakubali hayo wakati sasa unakataa kitabu cha Enoch ambacho maneno yake ni sehemu ya mandiko unayoyaamini kuwa ni neno la Mungu?
 
Sio naonekana, ndio sikuelewi, si elewi ninachokiandika???!!! Huelewi ninacho kiandika. Yesu hapa Duniani alishi kama sie wanadamu ingawa yeye alishinda dhambi na hakutenda dhambi. Je ulishaona kwenye Biblia pameandikwa "Bwana Yesu alipokwenda msalani" ndio maana nilisema sio yote aliyo yafanya hapa duniani yako katika Biblia.

Mistari iliyotoka kitabu cha Henoko na kunukuliwa na Yuda katika Biblia jua ndio ilistahiri kuwepo katika Biblia hayo mengine yaliyo baki yalifaa kwa matumizi yako na wengine sio kwa Biblia. Kuondolewa au kuto kujumuishwa kwa kitabu hakuleti tofauti yeyote, bado mistari miwili ndio iliyopo.

Na kurahisishia sasa ili uelewe, kutokujumuishwa kwa maneno mengine ya kitabu cha Henoko katika Biblia ni sawa na kutokuandikwa katika Biblia Yesu alienda msalani.


Na washawasha!








 
Vitabu 73 mmevimaliza? Malizeni kwanza hivi ndio mtafute vingine. Ukisoma injili moja tu mfano Yohane inatosha kukufikisha Mbinguni. Hivyo mimi sioni shida viwepo au visiwepo.
 
Vitabu 73 mmevimaliza? Malizeni kwanza hivi ndio mtafute vingine. Ukisoma injili moja tu mfano Yohane inatosha kukufikisha Mbinguni. Hivyo mimi sioni shida viwepo au visiwepo.


Ajabu na kweli, hawa wanaoleta hizi stories hapa wana hidden agendas na mipango mikakati maalumu ya kuzitekeleza.

Kama mtu ana weza kuandika haya kuhusu kitabu cha Henoko lakini eti kashindwa kuona wakati ule Bwana Yesu anasulubiwa msalabani mmoja wa wale wawili waliosulibiwa naye alingia mbinguni kwa kumuomba Bwana Yesu palepale wakiwa wametundikwa, haikuhitaji nukuu ya Henoko wala Yashua ili ahakikishiwe huo wokovu wake.

Na Mungu kawapiga upofu na utahira wa kudhania kuwa kukosoa Biblia kutasaidia kuwarudisha nyuma wale ambao walishakata shauri kumpokea Yesu. Alishindwa Paulo wakati ule akitwa Sauli wataweza hawa wa kizazi cha makinikia?


Na washawasha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…