Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 699
Hadi uhuru Waingereza walitazama Kenya kisheria kuwa na sehemu mbili:Kwa mujibu wa historia na post yako inaonyesha Pwani ya kenya na kisiwa cha Lamu sultan, wa zanzibar alizikodisha kwa muingereza. Je huo muda wa kukodi haujesha na kama umeisha ni nani aidai hii sehemu, smz au jamhuri ya muungano au MRC (mombasa republican council).
a) Protectorate of Kenya, yaani kanda la kilomita 16 (=maili 10) kwenye pwani la bahari, pamoja na visiwa vyote. Hili lilikuwa kanda ambalo waliwahi kukodi kutoka Sultani, wakiendelea kulipa kwenye makisio ya Zanzibar. Kisheria walitawala hapa kwa niaba ya Sultani.
b) Kenya colony, yaani maeneo yote mengine ya Kenya.
Hali halisi walitawala yote kama sehemu moja. Wakati wa uhuru wanasiasa wa Kenya bara hawakuwa tayari kutambua hali za Sultani, hivyo Waingereza walinyamaza tu na kukabidhi yote kwa serikali ya Nairobi. Hata hivyo, wenyeji wengine walipinga. Katika historia hii uko pia msingi wa mahakama za kadhi (mahakama za Kiislamu) zilizopo katika Kenya, maana Waingereza walitunza utaratibu waliokuta.