Kwanini Kikwete hakusimama na Lowassa?

ndio maana Nyerere alibadili uteuzi wa, wa kiongozi moja wa juu, baada ya muhusika kumueleza Mke wake, ambaye nae alianza kusherekea kabla ya Taarifa rasimu kutolewa
 

Ha ha ha ha....Wewe ni lini ulichaguliwa kuwa msemaji wa Watanzania? Naona umewekwa hapa kuwakingia kifua mafisadi maana michango yako yote inaonyesha hivyo, kila la heri.
 
ndio maana Nyerere alibadili uteuzi wa, wa kiongozi moja wa juu, baada ya muhusika kumueleza Mke wake, ambaye nae alianza kusherekea kabla ya Taarifa rasimu kutolewa

Mkuu do you mean J.C Malecela?
 

Mkuu naamini huna uhakika wa hili. INASEMEKANA kwamba, Rais alikutana na PM wake na kuongelea mambo haya.

Kwa taratibu, katika hoja za nguvu kama zilivyotolewa na wabunge, Kamati Kuu ya NEC hukutana na kujadili nini cha kufanya. Inasemekana kuwa, CC-NEC ilimtaka PM ajiuzuru ili kulinda heshima ya Rais na Serikali. Hapo ndipo PM alipomuuliza Rais nae akasema sina pingamizi. Hivyo uamuzi wa PM ukawa ni kujiuzuru.

Wakati kikao cha Bunge kikizungumzia masuala ya Richmond, Makamu wa Rais alikuwa Arusha na Rais alikuwa Dar. Wote walikutana Dodoma kabla hata PM hajatangaza kujiuzuru. Rais alikutana na Kamati Kuu ya CCM Taifa kabla hata PM wake hajajiuzuru. Na kuna tetesi pia kuwa, Rais alishaamua kuwa atamteua MPP hata kabla EL hajajiuzuru.


Kweli kabisa


Rais hakushtushwa na kujiuzuru kwa EL hata kidogo. Ila naweza kusema alisikitishwa kwa uhakika.

Ni lazima tuzoee kuwa kujiuzuru katika dhamana ya umma ni jambo la lazima kama umevunja sheria za nchi au sheria za utumishi wa umma. Haiwezekani watu wakamezeana kwa kila jambo baya linalotendwa kwa kuogopa gharama ambazo zingeweza kukwepwa kwa kufanya uteuzi makini na kuwa na control kwa watu wanaoteuliwa.

Inavyoonekana ni kuwa EL alijiuzuru kwasababu asingefanya hivyo Bunge lingeweza kumtaka ajiuzuru kwa kupiga kura za kutokuwa na imani nae. Uwezekano huo ulikuwepo. Hivyo, aliona ni busara zaidi kujiuzuru kuliko kulazimishwa kwa njia ya kura za maoni za Wabunge.

Nakubaliana na wewe sana kuwa, kama Rais angeamua kuliomba Bunge kuelewa kilichotokea, kwa yeye kuwa na imani kwamba hakukuwa na makosa yaliyofanywa moja kwa moja na waziri wake Mkuu, Bunge lingeweza kutoa onyo kali kwa PM na mambo yangekwisha na EL angeweza kuwa PM hadi leo.

Hili pia linawezekana. Japokuwa kwa kufanya hivyo hakumuongezei/hakukumuongezea sifa yoyote ya maana kisiasa.

Je, ina maana kwa Kikwete kusimama na Lowassa kunamfanya Lowassa asiwe na makosa? Na kama alikuwa na makosa ni kweli yalimstahilisha ajiuzulu kwa namna ile ya utekaji nyara nchi?

Hapana, naamini kuwa kama Rais angesimama na EL katika yaliyomkuta, kusingefuta makosa yoyote ya EL, hata kidogo. Kwa kutegemea jinsi gani Rais angesimamia hoja, kungeweza kumuingiza Rais katika kashfa ile (angekuwa amenunua kesi) na angeweza kupoteza imani ya wananchi kwake, ama kungeweza kuisafisha serikali yake vizuri sana. Yote yanawezekana. Ila uangalifu mkubwa ulihitajika katika kuamua Rais awe upande gani. Nadhani pia alishauriwa aachie uhuru wa Bunge kufanya kazi yake.
 
- Rais alikuwepo Dodoma, Ikulu ya Chamwino siku waziri mkuu wake wa kwanza alipojiuzulu.

Nadhani uko sahihi; lakini Kikwete hakujua wala kamati yao haikujua Lowassa anajiuzulu siku ile. Hili nina uhakika nao.

- Suala zima la kujiuzulu kwa waziri mkuu Mh. E. Lowassa, lilikuwa handled na bunge kama katiba yetu inavyosema, rais wetu aliheshimu mgawanyo wa madaraka kati ya bunge, Mahakama na Ikulu.

Hapana, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Bunge halina usemi nao. Bunge lina uwezo wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani waziri mkuu na kumlazimisha kuondoka, lakini anapoamua kujiuzulu Bunge halina usemi hadi wasikie majibu ya Rais. Ndiyo sababu ya Spika kuahirisha Bunge kufuatia pendekezo la Masilingi ili awasiliane na Rais kwanza.
- Kwa kutoingilia kati maamuzi ya bunge, rais wetu aliheshimu katiba, na anahitaji heshima kubwa for that, kwa sababu aliweka msingi mzito wa kuheshimu katiba kwa kizazi kijacho

Hapana kwa kutokusimama na Waziri wake Mkuu au kushauriana naye kabla hajaleta hoja yake Bungeni, Rais wetu alionesha udhaifu mkubwa wa uongozi na kusababishia Taifa usumbufu mkubwa usio wa lazima.
 
Mwanakijiji,

..hoja yako hii inanifanya nirudi kwenye ripoti ya kamati ya uchunguzi ya Bunge iliyoongozwa na Dr.Mwakyembe.

..katika ripoti hiyo kuna taarifa za Waziri Mkuu Lowassa kukiuka maamuzi ya vikao vya baraza la mawaziri ktk mchakato wa mkataba wa Richmond.

..siamini kama Raisi hakuwa na habari kwamba Waziri Mkuu wake alikuwa akikiuka maamuzi ya vikao alivyoviongoza Raisi mwenyewe.

..mipaka ya kimadaraka ya Waziri Mkuu wa Tanzania haimruhusu kufanya jambo lolote lile la kuingilia maamuzi ya waziri mwingine, au kumshinikiza waziri huyo, bila baraka za Raisi.


..Waziri Mkuu Kawawa alipokwenda mbali na Azimio la Arusha mpaka kufunga maduka binafsi ya nyama, Mwalimu Nyerere alitamka waziwazi kwamba hakumtuma kufanya hivyo. sasa kwanini Raisi Kikwete amekosa ujasiri wa kutamka kwamba hakumtuma Waziri Mkuu Lowassa kuingilia na kuvuruga mchakato wa mkataba wa Richmond?

..kauli ya Raisi kwamba kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ni "ajali ya kisiasa" kunazidi kunishawishi kwamba madudu aliyokuwa akiyafanya yalikuwa na baraka za Raisi.

..swali langu ni hili: kama Raisi alisimama upande wa Lowassa wakati akivuruga na kuingilia mchakato wa mkataba wa Richmond, kwanini alishindwa kumtetea wakati alipopata matatizo?


NB:

..Lowassa alisema bungeni kitu kama shida yao ni waziri mkuu/uwaziri mkuu etc etc.

..hiyo nayo inaweza kumshawishi mtu aamini kwamba Lowassa alikuwa "bangusilo" tu.

..PAMOJA NA HAYO, NILIFURAHIA KUONDOLEWA KWA LOWASSA KUTOKANA NA KASHFA HII -- HATA KAMA HAKUWA "KILONGOLA."

..vilevile Dr.Mwakyembe alidai kuna mambo hakuyaweka ktk ripoti yake ambayo yangeweza kuiaibisha serikali.

..sasa ni aibu gani hiyo iliyofichwa inayozidi ile ya Waziri Mkuu wa Tanzania kuwa implicated kiasi kile?
 
Last edited:

Rais pia anatakiwa kuhakikisha kwamba ufujaji wa mali ya umma na rasilimali kwa wizi au ufisadi kama uliofanywa kwenye pesa za EPA, Rada, Kagoda, Gharama za ujenzi wa Twin Towers, Richmond/Dowans, Meremeta, Deep Greens, Kiwira, mikataba ya uchimbaji wa dhahabu.

Itakuwa ni kichekecho na uzembe wa hali ya juu kwa Rais wa chi kunyamaza kimya pale watendaji wake wengi aliowateua katika nyadhifa mbali mbali ambao wanaonyesha dhahiri kwamba utendaji wao katika nyadhifa mbali mbali walizopewa ni mdogo mno au umegubikwa na ufisadi.

Kutokana na tuhuma mbali mbali kuna viongozi ambao walitakiwa wawe wameondolewa madarakani siku nyingi sana.
Kwa mfano kamati ya Mwakyembe ilishauri kuondolewa kwa Mkuu wa TAKUKURU, na Mwanasheria Mkuu lakini hadi hii leo bado wapo madarakani na Rais hajasema lolote, yaliyosemwa na kamati ya Mwakyembe si maneno ya mtaani.

Baada ya aliyekuwa gavana wa BoT Ballali kukimbia nchi, Serikali ilikuwa na muda wa kutosha kuhakikisha anahojiwa ili kupata ushahidi toka kwake kutokana na wizi mkubwa wa shilingi 133 billioni lakini Rais hakuona umuhimu wa kufanya hivyo hata pale ambapo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini alipotamka hadharani kwamba nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania kumrudisha Ballali nchini ili ajibu tuhuma dhidi yake kama ikiombwa kufanya hivyo. Kikwete alinyamaza kimya badala ya kuichangamkia offer hiyo toka Marekani.

Swala la ununuzi wa Rada. Yule mhindi aliyekuwa kama wakala na kujipatia bilioni 12 za pesa za Watanzania alikuwa tayari ameshaanza kuhojiwa na vyombo vya habari. Kwa mshangao wa wengi hakuwekwa rumande ili kusaidia uchunguzi uliokuwa unaendelea na hatimaye akaweza kutoroka na hadi hii leo hakuna yeyote katika vyombo vya dola aliyechukuliwa hatua zozote kufuatia kutoroka kwa yule wakala. Na kushindwa kumchukulia hatua yeyote kunaonysha uzembe wa hali ya juu katika ngazi za juu kabisa za serikali.

Aliahidi kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa dhahabu. Sidhani kama inahitaji miaka minne kutoa agizo kwamba mikataba ya uchimbaji wa dhahabu ambayo haina maslahi kwa nchi ipitiwe ili kuhakikisha inakuwa modified kwa maslahi ya Watanzania. Huu pia ni uzembe mwingine.

Kiwira si maneno ya mtaani. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba Mkapa na Yona walijiuzia mgodi ule kwa njia za kifisadi, vinginevyo wangezungumza siku nyingi sana jinsi walivyojiuzia mgodi ule. Kunyamaza kwa Kikwete katika hili pia ni dalili za kwamba hawezi kusimamia haki ndani ya nchi yetu ili kuhakikisha kwamba maslahi ya Watanzania siku zote yanalindwa bila woga wowote ule

Kwa kifupi kunapokuwa na uzembe katika utendaji wa viongozi mbali mbali walioteuliwa na Ris na Rais akakaa kimya kuhusu uzembe huo, basi hii ni dalili ya kutosha kabisa kwamba Rais ameshindwa katika uongozi. Pia kuna ahadi Kikwete alizotoa wakati wa kampeni yake hadi hii leo hajazitimiza na wala hajatoa kauli yoyote kuhusu kikwazo cha kutimiza ahadi hizo. Kwa mfano ahadi ya kuipitia mikataba ya uchimbaji wa dhahabu, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na maisha bora kwa kila Mtanzania…(oops! Hili tunajua kwamba uchumi wa dunia umetetereka pamoja na hayo hatukuona sera zozote zile za kufanikisha ahadi hii maana tunajua mabilioni ya Kikwete yalikupotelea tena hakuna hata uwajibikaji wa kuonyesha pesa hizo zimewasaidia vipi Watanzania na mabilioni mangapi yametolewa. Huu ni ushahidi tosha kwamba Kikwete awamu moja inamtosha kabisa hana sifa yoyote ile ya kuongezewa awamu nyingine hapo 2010.

Wakati umefika wa Watanzania kuacha unafiki wa kuwasifia viongozi ambao hawana uwezo wa kuliongoza Taifa letu, kufanya hivyo kutalisaidia Taifa letu ambalo miaka nenda miaka rudi pamoja na misaada na mikopo chungu nzima toka kwa nchi za wafadhili na mashirika mbali mbali ya kimataifa na rasilimali chungu nzima tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu bado asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi maisha ya umaskini wa kutisha.
 
... lakini Kikwete hakujua wala kamati yao haikujua Lowassa anajiuzulu siku ile. Hili nina uhakika nao.

Uhakika wako si sahihi.

Kikwete alijua, tena alikuwa wa kwanza kujua, siku ile kwamba Lowassa atajiuzulu.

Edward Lowassa: Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.
 

Hapa swali ni je, Raisi anafungwa mikono asiweze kumwondoa Waziri Mkuu bila baraka za Bunge ?

- Kwenye kuheshimu maamuzi ya bunge, rais wa sasa amekuwa very consistent, na ni lazima ieleweke kuwa sometimes rais knows best on what is national interest na what is not ndio maana tukamchagua kuwa rais wetu.

Una hakika na unayosema ama ndiyo yale yale CCM knows best what's good for the country.

- Katika mkutano mmoja na waandishi wa habari pale Diamond wakati wa wahujumu uchumi, Mwalimu aliulizwa na Eda Sanga, kama kwa nini anawalinda viongozi kama Sir George Kahama, Mwalimu alijibu kuwa haendeshi taifa kwa kusikiliza maneno ya mtaani.

Yapi hayo maneno ya mitaani - EPA, Richmond, Meremeta, Tangold, Kiwira, Dowans, IPTL, List of Shame, Twin Towers, Kagoda ?

- Kwa kifupi rais wa jamhuri hawezi ku-respond on kila neno linaloanzishwa mtaani bila ya facts au ushahidi wa kutosha.

Ndiyo hawezi kwa sababu hana ubavu wala ujasiri wa ku'act'. Naamini Lowassa angekataa kujiuzulu, ingekuwa kasheshe.


Kazi kweli kweli !! Kwa mwendo huu mkate wa Salva uko hatarini.
 

Huo unaweza kuuita ushahidi ?
 
Ndio ni ushahidi.

Waziri Mkuu anapotamka hadharani, Bungeni, kwamba ameshamuandikia Rais barua hawezi kuwa anaongopa. Hawezi kusema tu halafu kutoka hapo ndio akakimbia kuandika na kutuma hiyo barua.

Tunaongelea barua kutoka ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ikulu, zinafika almost papo hapo na zina rekodi. Barua za kawaida za mitaani tu zina rekodiwa zimekuwa dispatched lini, sembuse ya kutoka Ikulu. Asingeweza kuja kuongopa "nilituma juzi, kwani hukuipata"? Kuna rekodi ya time line.

Na sidhani kama unaweza kutangaza umejiuzulu kabla ya kukubaliwa kujiuzulu.

Kikwete alijua, alikuwa wa kwanza kujua, kwamba Lowassa atajiuzulu.

Edward Lowassa: Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.
 

Umeamkia upande gani kaka! Kwa mara ya kwanza sipati maana ya maandiko yako kabisa - na taarifa zako zimekuwa za kufikirika! Ama unataka tufanye zoezi la kinadharia tu hapa! Naona unajaribu kutafuta sababu ya supu kuchacha wakati supu ilishamwaga - ama kunasupu nyingi inakaribia kuchacha?
 

Inawezekana nia ya MKJJ ni kuwapambanisha EL na JK maana keshaona zaidi ya hapo nothing else will happen,JK amecheza kama opportunist,na hivyo kuna wale wanaotaka kuona EL VS JK,Tusubiri if thats possible...It depends on who is willing to loose what and vice versa also the consequences of either or.
 
Ndio ni ushahidi.

Waziri Mkuu anapotamka hadharani, Bungeni, kwamba ameshamuandikia Rais barua hawezi kuwa anaongopa. Hawezi kusema tu halafu kutoka hapo ndio akakimbia kuandika na kutuma hiyo barua.

Ndiyo maana huwa nasema soma kilichoandikwa; Lowassa alisema hivi:

"nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi."

Sasa umesoma wapi kuwa amesema ameandika barua ya kuomba kujiuzulu?


Ni uamuzi tu tunauzungumzia. Unajuaje kama barua ilikuwa inaandikwa baada ya hotuba yake hiyo maana amesema tu "nimeamua" hajasema "Nimeandika barua kwa Rais".. ni vitu viwili tofauti. Yawezekana (na ndivyo ilivyokuwa) wakati anazungumza ndiyo barua inaenda kwa Rais. Vinginevyo tukiamini kuwa Rais alijua ina maana alimficha Spika kitu ambacho Spika anasema hakuwa na mawasiliano na aliyemteua (Rais).

Na sidhani kama unaweza kutangaza umejiuzulu kabla ya kukubaliwa kujiuzulu.

Ni wazi hukumbuki kilitokea nini Bungeni. Kaangalie rekodi zao.

Kikwete alijua, alikuwa wa kwanza kujua, kwamba Lowassa atajiuzulu.

Katika maneno ya Lowassa na katika mjadala wa Bunge hakuna ushahidi huo, pia zingatia hotuba ya Rais kwa wazee wa Jiji la Dar.
 

Ahsante,

Ndiyo maana niliuliza

Is this anything than an exercise in futile, and flawed at that, rhetoric ?

Mwanakijiji kama mtu uliyemsema sana Lowassa unashangaa nini kikwete alivyomtosa? Asingemtosa napo ungeandika makala ya kushangaa equally?
 

Hivi MKJJ anaweza akaandika barua kama hajaamua?
Nadhani hiyo ni past tense so na kwa maana hiyo aliposema "Ameamua" kwa wakati ule,ina maana kwamba ni jambo ambalo alishalifanyia maamuzi na kulitekeleza,unless kuna technicallities hapo mtueleze...Nilivyoelewa mimi hilo alilizungumzia kama past tense.
 
Ahsante,

Ndiyo maana niliuliza



Mwanakijiji kama mtu uliyemsema sana Lowassa unashangaa nini kikwete alivyomtosa? Asingemtosa napo ungeandika makala ya kushangaa equally?

Una maana gani "kumsema sana"? Hakuna ushahidi wa mimi "kumsema sana" Lowassa.
 
Duh,kweli hapa tutajuwa mengi,kwanza hapo kwenye kuamua kuandika barua,kwasababu atakuwa alilidanganya bunge kama akisema ameamua kuandika barua ya kujiuzulu kwa rais na wakati hakufanya hivyo,hilo pekee lina utata sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…