Kwanini kiatu kilinikimbiza?

Kwanini kiatu kilinikimbiza?

Joined
Apr 4, 2024
Posts
77
Reaction score
277
Habari wadau wa jukwaa hili
Bila shaka mko salama
Miaka 20 iliopita pale Tanga wilaya ya mkinga zamani
Muheza

Kata ya Maramba kijiji Cha Maramba kitongoji Cha msumbiji

Ilikua muda wa saa Saba usiku nikiwa natoka kuangalia mkanda wa video enzi hizo
Tulikua wengi lkn kadri tunavyokwenda ndo tunazidi kupungua mpk nafika njia panda ya kwenda nyumbani nilibaki mwenyewe

Picha lilianzia njia panda nikakutana na mtu mrefu sana akakimbiza akanipiga ngwala nikaanguka nikaburuzika Tumbo lilichubuka sana
Nilivyoamka sikuangalia nyuma nikaendelea na mbio

Lkn nafika mbele kidogo nikaona kiatu kikubwa kama buti la JEJE likiwa halina mguu lipo nyuma yangu linanikimbiza
Nilipokaribia nyumbani kiatu kikapotea.

Nafika nyumbani mzee anagoma kufungua mlango ananiambia Leo lala nje

Nikiwa mlangoni nimejibanza
Nikaona kundi kubwa la mapaka likiwa linaelekea mwisho wa mji ambako Kuna mashamba
Nilitulia tuliii

Nikalala pale pale mpk asbh
Mzee alipoamka akanikanya sana mambo ya kutembea usiku
Nikaomba msamaha yakaisha

Lkn muda wa saa moja asbh likaonekana lile buti na jembe kubwa vikiwa njia panda kilicho washangaza watu ni ukubwa wa lile buti likiwa na matope na lile jembe ni kubwa sana binadamu wa kawaida hawezi kutumia.
Na Yale matope ilikua wakati wa kiangazi.

Ikabidi mwenyekiti na wajumbe wakaita watu wao wanaowajua vikabebwa wakapeleka wanakojua wao

Sasa najiuliza lile buti kwann limenikimbiza? Na je lingenikamata ingekuaje?
Mpk Leo naogopa sana lile eneo
 
ni wazee wa hapo mtaani, waliamua tu kukutingisha, ukome kuwaharibia pozi wakuwa kwenye shughuli zao
 
Siku zote tunapata stories kwenye matukio kama hayo wahusika walikimbia tu au kuzimia. I wish siku initokee kama hivyo alafu nikaze ili nione matokeo yake itakuwaje😀
hayo mambo sio poa aise, unaweza kimbia speed ambayo hujawah + kuloa jasho na mkojo 🤓
 
Habari wadau wa jukwaa hili
Bila shaka mko salama
Miaka 20 iliopita pale Tanga wilaya ya mkinga zamani
Muheza

Kata ya Maramba kijiji Cha Maramba kitongoji Cha msumbiji

Ilikua muda wa saa Saba usiku nikiwa natoka kuangalia mkanda wa video enzi hizo
Tulikua wengi lkn kadri tunavyokwenda ndo tunazidi kupungua mpk nafika njia panda ya kwenda nyumbani nilibaki mwenyewe

Picha lilianzia njia panda nikakutana na mtu mrefu sana akakimbiza akanipiga ngwala nikaanguka nikaburuzika Tumbo lilichubuka sana
Nilivyoamka sikuangalia nyuma nikaendelea na mbio

Lkn nafika mbele kidogo nikaona kiatu kikubwa kama buti la JEJE likiwa halina mguu lipo nyuma yangu linanikimbiza
Nilipokaribia nyumbani kiatu kikapotea.

Nafika nyumbani mzee anagoma kufungua mlango ananiambia Leo lala nje

Nikiwa mlangoni nimejibanza
Nikaona kundi kubwa la mapaka likiwa linaelekea mwisho wa mji ambako Kuna mashamba
Nilitulia tuliii

Nikalala pale pale mpk asbh
Mzee alipoamka akanikanya sana mambo ya kutembea usiku
Nikaomba msamaha yakaisha

Lkn muda wa saa moja asbh likaonekana lile buti na jembe kubwa vikiwa njia panda kilicho washangaza watu ni ukubwa wa lile buti likiwa na matope na lile jembe ni kubwa sana binadamu wa kawaida hawezi kutumia.
Na Yale matope ilikua wakati wa kiangazi.

Ikabidi mwenyekiti na wajumbe wakaita watu wao wanaowajua vikabebwa wakapeleka wanakojua wao

Sasa najiuliza lile buti kwann limenikimbiza? Na je lingenikamata ingekuaje?
Mpk Leo naogopa sana lile eneo
hapo mzee wako ndo muhusika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom