joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 18,832
- 39,341
Ninacho wakubali wanaweza kuoa leo,kesho wakaacha na kesho kutwa wanavuta mwengine. Sasa Wakristo kuoa mchakato ,kuachana ndio usiseme ni mchakato wa mda mrefu mno.
Independent au dependants mkuu? Ulikua unamaanisha nini embu fafanua...Wanawake wengi wenye malezi ya kiislamu ni submissive Ila kwa upande wa pili ni independent zaidi..
Na kwa Tanzania, ni wachache wanaoweza kumchagua mwanamke independent dhidi ya mwanamke submissive Ila wote wana faida na hasara zake.
Wanawake wengi wakikristo wanatokea jamii zal bara ambapo wengi wana elimu kiasi lakini pia huwa wanafanya kazi. Iwe za shamba hadi corporates jobs kwa hiyo wao ndoa ni kitu muhimu ila sio kiini cha kuishi kwao sababu wana maisha pia nje ya ndoa yanayowawezesha, kujitegemea "independent".Independent au dependants mkuu? Ulikua unamaanisha nini embu fafanua...
Eti bara hakuna ujamaa acha vichekesho,bara ndiko kwenye maisha halisi ya mwafrika ukiachana na sehemu ambazo waarabu walipita kama ujiji,tabora,singida...huo ujamaa wa pwani labda kuwa firm kwenye udini.Kikawaida wakristu wengi pia huchelewa kuoa kwa sababu ya "ndoa ya mara moja pasipo talaka" Lakini pia gharama za harusi, send off plus kitchen party..
Halafu pia jamii za kiislamu nyingi ni za pwani ambazo bado zina ujamaa kiasi mtu akishindwa kuoa anaweza kutolewa mahari na wanandoa wakaishi ukweni kwa muda. Ila wakristo wengi wanatokea jamii za bara ambazo ujamaa ni mdogo hivyo ukiyavagaa majukumu. Watu kukutelekeza ni dakika
Sababu zipo nyingi Ila kwa uislamu ndoa ni nyepesi zaidi sio kwa kuingia ama kuachana. Kwa wakristu ni tofauti ndio maana wengi wanachelewa
Upo sahihi kwa mtazamo wako mkuu. Na sijapinga bara hakuna ujamaa ila katika masuala ya ndoa, kijana wa pwani anaweza kusaidiwa kutolewa mahari na wazazi wake. Akaoa na kuzalia nyumbani kwa wazazi wake.Eti bara hakuna ujamaa acha vichekesho,bara ndiko kwenye maisha halisi ya mwafrika ukiachana na sehemu ambazo waarabu walipita kama ujiji,tabora,singida...huo ujamaa wa pwani labda kuwa firm kwenye udini.
Hakuna ndoa isiyovunjika humu duniani, mkristo akitaka kuacha ndoa kuna taratibu zinafuatwa...Ndoa zao ni ndoano ukimeza umekwenda na maji. Mwanamke anaweza kuficha make changes yake akiolewa tu ndio kila rangi utaiona anajua hakuna kuachana milele wengi wanaishi kwenye mateso makubwa