Kwanini kanisa linaadhimisha misa siku ya mwaka mpya?

Kwanini kanisa linaadhimisha misa siku ya mwaka mpya?

Pamoja na hayo....leo ni siku kuu ya bikira Maria mama wa Mungu
 
Kifupi ni kwamba kwenye muongozo hakuna misa ya mwaka mpya ni uamuzi wa paroko kuamua kufanya kama misa ya shukrani kumaliza mwaka kikawaida ila sio mwaka wa kanisa ( kiliturujia)

So inaweza kufanyika tu ibada ya shukrani na misa unayoshiriki asubuhi ni sio misa kwa ajili ya mwaka mpya bali ni sherehe kubwa ya UMAMA WA BIKIRA MARIA ambapo sherehe hii huangukia tarehe 1/jan


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwenye kuelewa aelewe hii.
 
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji120][emoji120][emoji120]
Nafikiri ushawahi sikia BC (before christ) yaani kabla kuzaliwa kristo na AD (anno domino) kilatini hicho yaani mwaka wa kuzaliwa kristo, kuna mengi yalitokea miaka hiyo lakini miaka michache baada ya kuzaliwa kristo tarehe zilianza upya na mwaka namba 1, kwa hiyo kama wafuatilia vizuri historia sikukuu ya mwaka mpya ni sikukuu ya kuzaliwa mkombozi yesu kristo japo imetengwa kidogo na christmass ambayo ni tar 25 ni siku moja, ndio maana basi lazima tarehe moja kuwe na misa sababu bado ni mwendelezo wa sikukuu ya kuzaliwa mwokozi

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
Mwaka Wa kanisa unatofautiana na mzunguko Wa siku 365¼ za kalenda unaohitimisha mwaka. So tarehe 31 December tunafanya ibada mwishoni mwa mwaka kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mungu kwa yote alotujaalia pamoja na kutufanya tuwe hai kwa mwaka mzima. Tarehe 1 Jan tunafanya ibada kuashiria tunaanza mwaka kwa kuendelea kumtumainia mungu ktk maisha yetu kwa mwaka mwingine tena
 
Huo mwaka wako wa kanisa sio wa kila kanisa .Sema wa wakatoliki.
Sisi Wengine mwaka wa kanisa letu Ni tatehe moja january

Basi mchague na siku ya kushereke pasaka 2020 maana bila kuufata mwaka wa kanisa katoliki hamtajua pasaka mfanye lini

Kifupi ni kwamba huwezi kulikwepa kanisa Katoliki ndugu yangu hili ni kama maji usipo yanywa utayaoga

NB fanyeni hivi unganeni waprotestant woote na wasabato kisha mchagua tarehe ya pasaka mkama mtaweza na mkishindwa mjue mnasubiri kanisa katoliki lifanye ndipo na nyie muige


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwaka Wa kanisa unatofautiana na mzunguko Wa siku 365¼ za kalenda unaohitimisha mwaka. So tarehe 31 December tunafanya ibada mwishoni mwa mwaka kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mungu kwa yote alotujaalia pamoja na kutufanya tuwe hai kwa mwaka mzima. Tarehe 1 Jan tunafanya ibada kuashiria tunaanza mwaka kwa kuendelea kumtumainia mungu ktk maisha yetu kwa mwaka mwingine tena
Sasa hujajibu swali, kwanini mwaka mpya? Ilianzia wapi? Huu ni mwaka mpya wa kikristo, na ulianza baada ya kristo kuzaliwa ndio maana unaitwa Anno domino

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom