Kwanini kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe imekaa kibaguzi?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Nimetoka kutazama matangazo ya kampeni ya Tokomeza Zero iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo. Nikavutiwa nayo.

Hata hivyo, nimeshangaa kuona kampeni hii imeweka focus kwa wanafunzi wa kike pekee.. Hii imekaaje? Vipi kuhusu watoto wa kiume? Kwanini isiwe jumuishi?

Nampongeza sana DC Jokate kwa dhamira yake ya kutatua changamoto za elimu katika wilaya anayoiongoza.

Sote tunajua mikoa ya Pwani inakabiliwa na matatizo mengi na mara nyingi shule za huko zimekuwa zikishika mkia kwenye matokeo ya mitihani. Hivyo, uamuzi huu wa DC Mwegelo ni wa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Hivi karibuni kutakuwa na harambee ya uchangishaji fedha (fundraising) itakayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ambapo kiingilio kitaanzia laki 1 kwa MTU mmoja na Milioni 1 kwa VIP.

Kama kuna ufafanuzi wa hili suala ningeomba nipatiwe maana imekuwa kawaida mtoto wa kiume kuwekwa kando kwa kisingizio cha kumuinua mtoto wa kike.

Hongera tena DC Jojo kwa initiative nzuri!
 
Too much sasa. Mtoto wa kike hata umbebe aje bado habebeki bora sasa uwekwe usawa,msaada kwa wote wa kiume na wa kike
Sidhani kama kumbeba mtoto wa kike kunasaidia zaidi ya kuharibu tu saikolojia yake. Atakuwa akiamini yeye ili afanye jambo lazima asaidiwe..

Fursa sawa zitolewe kwa WATOTO wote kama kweli kuna nia ya kuwafanya wajione wako sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Jokate mpak sa hv hana mme hata hao wasichana wanaosaidiwa ujue na wao wengi wao hawataolewa waspokuwa makni, mwanamke anapoelimika sana huwa ana overconfidence na wengi wao wanaloose nature yao...na kujikuta wanapigwa eat and run method
 
Nimetoka kutazama matangazo ya kampeni ya Tokomeza Zero iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo. Nikavutiwa nayo.

Hata hivyo, nimeshangaa kuona kampeni hii imeweka focus kwa wanafunzi wa kike pekee.. Hii imekaaje? Vipi kuhusu watoto wa kiume? Kwanini isiwe jumuishi?

Nampongeza sana DC Jokate kwa dhamira yake ya kutatua changamoto za elimu katika wilaya anayoiongoza.

Sote tunajua mikoa ya Pwani inakabiliwa na matatizo mengi na mara nyingi shule za huko zimekuwa zikishika mkia kwenye matokeo ya mitihani. Hivyo, uamuzi huu wa DC Mwegelo ni wa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Hivi karibuni kutakuwa na harambee ya uchangishaji fedha (fundraising) itakayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ambapo kiingilio kitaanzia laki 1 kwa MTU mmoja na Milioni 1 kwa VIP.

Kama kuna ufafanuzi wa hili suala ningeomba nipatiwe maana imekuwa kawaida mtoto wa kiume kuwekwa kando kwa kisingizio cha kumuinua mtoto wa kike.

Hongera tena DC Jojo kwa initiative nzuri!
Ungeweka kapicha ingependeza kweli kweli
 
Tatizo wanawake tz wanaona wao ni watu wa kuonewa.....ila wakiwa na uwezo au akimzidi Mwanaume kifedha au nyadhifa wakiwa kwenye familia basi ni shida

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wanawake tz wanaona wao ni watu wa kuonewa.....ila wakiwa na uwezo au akimzidi Mwanaume kifedha au nyadhifa wakiwa kwenye familia basi ni shida

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Mentality ya kujikwamua sina shida nayo.. Tatizo ni pale inapofanywa at the expense of wanaume.. Kama bifu fulani hivi.. Fuatilia hata harakati za feminists utaona..

Kwanini isiwe tu fair play.. Hivi wanaume wakisema waanzishe na wao hizo mambo za kujipendelea wao na kuukomaza mfumo dume itakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom