Kwanini Jaji Mwanga asikilize kesi anayolalamikiwa? Iko wapi Natural Justice?

Kwanini Jaji Mwanga asikilize kesi anayolalamikiwa? Iko wapi Natural Justice?

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,908
Reaction score
3,231
Gw7y0O0WAAAD57o.jpg



Dhana ya kanuni za haki ya asili (natural justice) kimsingi imejengwa juu ya misingi mikuu mitatu.

Kwanza ni Nemo Judex in Causa Sua – "Hakuna mtu anayepaswa kuwa jaji katika kesi yake mwenyewe"

Pili ni ni Audi Alteram Partem – "Sikiliza upande wa pili"

Pia soma GE2025 - Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

Hii inahakikisha kuwa kuna usikilizaji wa haki. Kila upande katika mgogoro unapaswa kupewa fursa ya kusikilizwa na kutoa maoni au utetezi wake.

Tatu ni Uamuzi wenye sababu (Reasoned Decision) – "Haki haitakiwi tu itendeke, bali ionekane kuwa imetendeka"

Sasa katika hali ya kustaajabisha ni pale Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam anapokataa kujitoa kwenye kesi, ambayo walalamika wanasema hawana Imani naye.

Leo Julai 28, 2025, Jaji Mwanga amegoma kujitoa kusikiliza kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

‎‎Kesi hiyo ya madai ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Zanzibar na wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.‎

‎Walalamikiwa ni Bodi ya wadhamini waliosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama hicho.

‎‎Jaji Mwanga ameisikiliza kesi hiyo tangu Aprili 17, 2025 ilipotajwa kwa mara ya kwanza na kuendelea nayo katika hatua tofautitofauti.‎

‎Walalamikaji hao walimwandikia barua hiyo ya kumtaka ajitoe katika kesi hiyo Juni 23, 2025, huku wakimlalamikiwa kuwa na upendeleo kwa upande wa walalamikaji na mgongano wa masilahi na kuwa na mgogoro naye, malalamiko ambayo Jaji Mwanga aliyasikiliza Julai 14, 2025.‎

‎Katika uamuzi wake alioutoa leo Jumatatu, Julai 28, 2025 Jaji Mwanga amezikataa sababu zote zilizotolewa na walalamikiwa akieleza kuwa hazina mashiko.‎

‎Jaji Mwanga amesema sababu za walalamikiwa hao kumtaka ajitoe ziliegemea katika uamuzi wake alioutoa Juni 23, 2025 katika shauri la maombi madogo ya zuio la muda ya walalamikaji.‎

Katika misingi ya haki za asili, msingi wa kwanza unakataza mtu kuwa jaji wa kesi yake mwenyewe? Iweje Jaji Mwanga asikilize malalamiko ya watu wasiokuwa na Imani naye?
 
Bila shaka atakuwa ana maslahi binafsi na hiyo kesi, na ndiyo maana amegoma kujitoa.
 
Wewe unadhani hapendi kupanda cheo kama alivyohaidiwa, hilo Deal hawezi kumuachia yeyote.
 
Huwezi kujichagulia Jaji kama unachagua maembe, otherwise itasababisha abuse of court process, mtu anaamka kavimbewa viazi anamkataa Jaji, kuna judicial guidelines
 
Hivi ikitokea Issa Mohamed na Maulida Komu wakatangulia mbele ya haki, kesi itaendelea au itafutwa?
 
Hivi ikitokea Issa Mohamed na Maulida Komu wakatangulia mbele ya haki, kesi itaendelea au itafutwa?
kama vipi wantangulizwe kabisa ku balance equation, na jaji pia nayeye ilitakiwa awe six feet under
 
Back
Top Bottom