Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

ukimkana shetani na makandokando yake ni lazima umrejee Mungu .
 
Mzee Tupatupa, kwa huku Tanganyika wala haihitaji kupiga ramuli kujua ni kwa nini. Chadema kwa kipindi hiki wamejimarisha sana na kujionyesha kuwa ni chama organized, chama chenye nguvu, na tumaini pekee la watanzania katika kuleta mabadiliko tunayoyahitaji. Hakuna chama kingine chochote kilichojipambanua kihivyo.
 
swadakta .
 
Tangu lianze vuguvugu la kuhama chamani-kutoka CCM kwenda kwingineko,wahamaji wamekuwa wakihamia CHADEMA. Kuanzia Simiyu hadi Monduli;Shinyanga hadi Muleba mambo ni hayo hayo.

Wamehama madiwani wa kutosha (wa mwisho ni wa jana wa kule Kamachumu Muleba). Wabunge wawili nao wameshagoma kuchukua fomu za CCM: Lembeli na Bulaya.

Pamoja na kwamba hawajataja vyama watakavyoibukia, I bet, wataibukia CHADEMA. Watakapoamua kugombea nje ya CCM. Labda wasigombee kabisa. Vuguvugu hili,kwetu wachambuzi wa kisiasa,lilitarajiwa. Majeraha ya Dodoma yatapuuzwa lakini chama kitaumizwa. Hilo lipo wazi kama nazi. Tutaficha kucha lakini upele utatuumbua.

Kuhama chama hakunishtui. Hakunioneshi tukio la kustaajabisha kisiasa. Wapo wazito kabisa chamani,kama Wasira,Tambwe na Makongoro,waliohama wakimwaga lawama lakini wakarejea wakifurahia. Na hata kuponda walipopapenda wakati wanakwenda.

Swali langu,hasa wakati huu wa uchaguzi,ni kwanini iwe CHADEMA tu? Kwanini kila mhamaji anahamia CHADEMA tu na si kwingineko? Tanzania haina vyama viwili. Waende na kwingine.

Kutakuwa na tatizo au tuzo ima wanakotoka au wanakowenda. Si bure! Viongozi wa CCM na CHADEMA wamulike vyema kabla ya kufungwa kwa dirisha hili la usajili ambao kwasasa halihitaji akili. Kutakuwa na jambo,na kuna mkono mtu nawaambia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
.
Bulaya na Lembele hawaendi Chadema kwanza mchakato wa kuchukua fomu za ubunge bila shaka umekwisha huko chadema!
 
kupokewa wpokewe ila wasigombee ubunge wala udiwani wawe wanachama wakawaida hapo itafahamika mamluki na watakatifu
 
Huyo lowasa unaye muita mwizi hadi leo yupo mwanachama hai ndani ya chama chenu ccm,kwanini hamjamfukuza?au unataka kutwambia kuwa ccm ni chaka la kuwahifadhi wezi?naomba majibu yako

Mtu mzima akikufukuza hakwambii toka.nadhani umejionea hali ilivyokuwa pale Dodoma.ameshajipima na sasa yupo njiani kuelekea chagga saccos
 
Bulaya na Lembele hawaendi Chadema kwanza mchakato wa kuchukua fomu za ubunge bila shaka umekwisha huko chadema!

Wewe wacha ujinga wako,nani kakwambia hilo?tuliza tako sindano iingie na dawa upate kupona,wewe ndiye msemaji wa cdm?
 
Mkuu ulitaka wahamie TADEA, au Uprona, au UDPD, au... Chadema ni chama cha pekee kinachoonesha hadi sasa matumaini ya pekee kwa watanzania. Hata ambao hawajahama wanafahamu hilo.

Mkimchukua fisadi lowasa nahama ukawa naenda kwa magufuri
 
Huo ni mtazamo wako kamwe hauwezi kukatazwa kutoa mawazo yako,na cdm kama taasisi haipo tayari kufuatisha ccm inataka nini

Siyo suala la mtazamo au kufuata CCM wanataka nini!Bali ni suala la weledi?Siyo kila ukionacho ni almasi vingine ni vichupa vilivyopondwa vizuri mithili ya almasi.

Huyu ni kati ya wale wachache Dr.Slaa aliyewapigia kelele kudhoofisha uchumi wa nchi.Ndiyo huyi alileta lile sakata la Richmond leo tunamuona msafi.

Hata huyo Mungu mnayemtaja kila siku hatawaelew.Sidhani hata Dr.Slaa atakubaliana na hilo.

Kama tunatetea weledi wa viongozi basi tunatakiwa kusimamia yale tunayoyakataa wabunge wetu wakiwa BUNGENI.Sitamwelewa Lissu au Kululila hawa wakikubali wazo la kumuingiza yule aliyetuhumiwa.CDM inaweza kushinda viti vingi.vya ubunge bila hata kumpokea Lowassa.

Daima nitakuwa TAIFA KWANZA CHAMA BAADAYE.Pole kama nitakuwa nimekukwaza kaka yangu Mmawia.
 
watanzania bhana, wangezuiwa kuhamia ndan ya chadema tena ungesema chama cha wabinafsi, ccm hakuna haki ila wameiona ipo chadema, wamekaribishwa watabadirishwa tu. CHADEMA MAKINI, M4C PAMOJA SANA;
 
Chadema ni mafisadi maji hufuata mkondo baada ya mabingwa wa kununua watu ili kupata uungwaji mkono kushitukiwa na kufurushwa ccm,

Hawana sehemu nyingine ya kwenda zaidi cdm.
Huko ndiko kunakoendana na vitendo vyao.
 
Swali langu,hasa wakati huu wa uchaguzi,ni kwanini iwe CHADEMA tu? Kwanini kila mhamaji anahamia CHADEMA tu na si kwingineko? Tanzania haina vyama viwili. Waende na kwingine.

Kutakuwa na tatizo au tuzo ima wanakotoka au wanakowenda. Si bure! Viongozi wa CCM na CHADEMA wamulike vyema kabla ya kufungwa kwa dirisha hili la usajili ambao kwasasa halihitaji akili. Kutakuwa na jambo,na kuna mkono mtu nawaambia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
.

TUPATUPA unashangaza kweli utadhani umenyonfolewa macho mabwepande!!! hiviii kama ungekuwa ni wewe unaham tu ya kukikimbia chama chako unadhani kwa mtazamo japo nahisi kama huna macho basi tuchukulie na upofu wako je utaelekea upande upi katika upinzani??? :smokin:
 
Back
Top Bottom