Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

Binafsi sioni ata umuhimu wa chadema kuwapokea hao ma ccm kwasababu waweza kuja kuwa ndo wasaliti wao wazuri. Na pia kama ccm ndo mafisadi, wanapohama ufisadi wanamwachia nan??. Chadema kuweni makini coz hao wahamiaji naamini wanakuja baada ya kupoteza tumaini lao😀

Cdm ni taasisi kubwa na makini,yeyote anaye kwenda ndani ya cdm,atafundishwa miiko ya cdm na kama hayupo tayari kuifuata milango ipo wazi kama ilivyotokea kwa zzk na wenzake.
 
Huwezi kwenda sehemu ambayo hata atakayekupigia kampeni kutoka ngazi za juu hafahamiki. Ukiwa CHADEMA huna sababu ya kujitambulisha sana maana ukisema vyama vya upinzani usipotaja CHADEMA bado hujakamilisha upinzani.

Kweli kabisa mkuu
 
Tumeshazoea kauli za viongozi wetu pindi wanapotafuta ridhaa kuongoza wananchi.Hayo ni maneno tu mdomoni,mbona alishindwa kukemea akiwa kwenye baraza la mawaziri miaka 20?

Ccm imetudanganya sana na sasa tunasema basi
 
wanatafuta nafasi za kugombea ubunge na udiwani, ila Urais ni wa slaa, na kwa cuf urais ni kwa lipumba
 
Mkuu, unataka kusema wote wanaohama ccm kwenda CHADEMA ni mamluki wanakwenda kwa kazi maalum ya kuchinja, kuiba na kuharibu mabadiliko?

Kwamba watakapogombea kupitia CHADEMa watafanya makusudi ama kuharibu form ili wawekewe pingamaizi? Kwamba watajichelewesha kurudisha forms ili wajifanye kushituka muda umepita ili ccm wapite bila kpingwa? Au watajitoa dakiks za mwisho kwa sababu mbali mbali ili chadema isiwe na mgombea?

Kwamba watakuwa wakipiga kampeni za hapana kwa CHADEMA kisirisiri?

Kwamba watakuwa wanatafuta taarifa na mikakati ya CHADema na kuipeleka Ccm ili ccm wawe na taarifa kamili kusudi wakamilishe uhaini na ugaidi wao?

Kwamba watakuwa makada kwenye kura halafu wauze number kwa ccm?

Au shida kubwa unayoiona ni nini? Kama ni haya CHADEMA wanafahamu katika msafara wa mamba na kenge wamo. Hili wamejiandaa. Ila kama unatahadhari nyingine, naomba uweke bayana!.

Or else ccm bye bye!

Tumeshatunga nyimbo.

CCm ilizaliwa visiwani Zanzibar, Sherehe za kwanza mkoani Dodoma.

Kilikufa kule Magogoni, mazishi yake yakafanyika kule CHATO mkoani geita.

Kitakumbukwa kwa kudidimiza maisha ya Watanzania, kuimarisha rushwa na ufisadi.

Zaidi sana kitakumbukwa kwa uvunjaji wa katiba ya nchi, mauaji ya raia wasio na hatia,

Matumizi mabaya ya raslimali za uma na madaraka.

Upendeleo na ubaguzi.

Ccm ulikuwa nasi katika raha, na katiba tabu ulitupeleka na kutelekeza.

Mafisadi walikupenda, lakini shetani amekupenda zaidi.

Kwa heri ccm. Ulale kwa pasipo amani.

Alale kwa shetani kila kukicha ni moto tu
 
Fahari amebakia mmoja baada ya ccm kusambaratika

Mmawia mtakuwa mmewaumiza sana Watanzania pale mtakapokubaliana na wajinga wachache kumkaribisha Edo.Kamwe hatutawaelewa.Mtabaki na Edo na makabrasha tu.
 
Mmawia mtakuwa mmewaumiza sana Watanzania pale mtakapokubaliana na wajinga wachache kumkaribisha Edo.Kamwe hatutawaelewa.Mtabaki na Edo na makabrasha tu.

Huo ni mtazamo wako kamwe hauwezi kukatazwa kutoa mawazo yako,na cdm kama taasisi haipo tayari kufuatisha ccm inataka nini
 
Cdm ni taasisi kubwa na makini,yeyote anaye kwenda ndani ya cdm,atafundishwa miiko ya cdm na kama hayupo tayari kuifuata milango ipo wazi kama ilivyotokea kwa zzk na wenzake.

Uwiii ha ha ha ha akina Shibuda ndo wabunge wenu hiyo ndo sampuli inayoingia sasa hivi this time mnalo na wamejipanga mpaka wameingilia nafasi ya mgombea wenu wa urais !Teh teh teh CDMCCM !!
 
Ta
yari naona umetishika wakati ulisema chadema imeshakufa

Kwani ikiwa tayari kambi ya wahamiaji haramu inamtisha nani? Inasubiriwa kuvamiwa na kuvunjwa tu tena waliohamia ndo wataivunja vizuri maana ni waroho wa madaraka kama Shibuda!!!
 
Mbowe aliwahi sema milango ya chadema imefungwa sasa hawa wanapitia madirishani? au alisahau kutoa funguo au maharamia yametumia "funguo Malaya" Slaa na Lisu watapata wapi ujasiri wa kukemea ufisadi wakati ndo yamejazana huko baada ya kukata ccm?

Hivi kuna fisadi yoyote aliyehamia cdm?
 
Binafsi sioni ata umuhimu wa chadema kuwapokea hao ma ccm kwasababu waweza kuja kuwa ndo wasaliti wao wazuri. Na pia kama ccm ndo mafisadi, wanapohama ufisadi wanamwachia nan??. Chadema kuweni makini coz hao wahamiaji naamini wanakuja baada ya kupoteza tumaini lao😀
Mradi tu wataipigia UKAWA kura ya ndio, katika hatua hii tunawakaribisha bila kujali ni mafisadi au sio. Kwa kitendo chao cha kuja kushiriki kuiuwa CCM tumetanguliza kuwasamehe! Karibuni nyote!!
 
Huenda yameshaanza kutimia. Mungu hunena katika vinywa vya binadamu na kanena kupitia kwa mtumishi wake
 
Back
Top Bottom