Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

Kwanini iwe CHADEMA tu? Kuna mkono wa mtu, Si bure!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tangu lianze vuguvugu la kuhama chamani-kutoka CCM kwenda kwingineko,wahamaji wamekuwa wakihamia CHADEMA. Kuanzia Simiyu hadi Monduli;Shinyanga hadi Muleba mambo ni hayo hayo.

Wamehama madiwani wa kutosha (wa mwisho ni wa jana wa kule Kamachumu Muleba). Wabunge wawili nao wameshagoma kuchukua fomu za CCM: Lembeli na Bulaya.

Pamoja na kwamba hawajataja vyama watakavyoibukia, I bet, wataibukia CHADEMA. Watakapoamua kugombea nje ya CCM. Labda wasigombee kabisa. Vuguvugu hili,kwetu wachambuzi wa kisiasa,lilitarajiwa. Majeraha ya Dodoma yatapuuzwa lakini chama kitaumizwa. Hilo lipo wazi kama nazi. Tutaficha kucha lakini upele utatuumbua.

Kuhama chama hakunishtui. Hakunioneshi tukio la kustaajabisha kisiasa. Wapo wazito kabisa chamani,kama Wasira,Tambwe na Makongoro,waliohama wakimwaga lawama lakini wakarejea wakifurahia. Na hata kuponda walipopapenda wakati wanakwenda.

Swali langu,hasa wakati huu wa uchaguzi,ni kwanini iwe CHADEMA tu? Kwanini kila mhamaji anahamia CHADEMA tu na si kwingineko? Tanzania haina vyama viwili. Waende na kwingine.

Kutakuwa na tatizo au tuzo ima wanakotoka au wanakowenda. Si bure! Viongozi wa CCM na CHADEMA wamulike vyema kabla ya kufungwa kwa dirisha hili la usajili ambao kwasasa halihitaji akili. Kutakuwa na jambo,na kuna mkono mtu nawaambia!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
.
 
Mbowe aliwahi sema milango ya chadema imefungwa sasa hawa wanapitia madirishani? au alisahau kutoa funguo au maharamia yametumia "funguo Malaya" Slaa na Lisu watapata wapi ujasiri wa kukemea ufisadi wakati ndo yamejazana huko baada ya kukata ccm?
 
Huwezi kuwa mkimbizi kutoka Burundi ukaenda Sudani,Somalia, Rwanda au Congo......lazima uende mahali palipo salama na uhakika wa maisha tofauti na ulipotoka......tukirudi kwenye siasa zetu Tanzania kwa sasa CHADEMA pekee ndio mahali salama na kimbilio la wanyonge.
Kuwe na mkono wa mtu au mguu wa mtu ula ukweli ni kuwa ukiwa ndani ya CDM upo mahali salama.
Tunakusubiri na ww Mzee wa Lumumba.
 
Kwa nini CDM? kwa sababu hakuna mtu atakayeruka maji akakanyage kinyesi! Unataka waende kwingine wanaweza shinda!!! nina wasiwasi, ila CDM kuna matumaini yasiyoishia njiani
 
Binafsi sioni ata umuhimu wa chadema kuwapokea hao ma ccm kwasababu waweza kuja kuwa ndo wasaliti wao wazuri. Na pia kama ccm ndo mafisadi, wanapohama ufisadi wanamwachia nan??. Chadema kuweni makini coz hao wahamiaji naamini wanakuja baada ya kupoteza tumaini lao😀
 
Mbowe aliwahi sema milango ya chadema imefungwa sasa hawa wanapitia madirishani? au alisahau kutoa funguo au maharamia yametumia "funguo Malaya" Slaa na Lisu watapata wapi ujasiri wa kukemea ufisadi wakati ndo yamejazana huko baada ya kukata ccm?

imefunguliwa kwa sasa special case .... lowassa kwani pesa kesha pewa
 
Jibu mbona liko wazi sana Mzee Tupatupa?

Ni kwamba Chadema ndiyo chama kikuu cha upinzani kwa nyakati hizi tulizo nazo, vivyo hivyo Chadema imejidhihirisha bila mashaka yoyote kuwa ndiyo tumaini pekee la wananchi wanyonge wa nchi hii.

Ingawa miaka ya nyuma napo kuliwahi kujitokeza baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo navyo kwa kiasi chake viliitingisha CCM, lakini tofauti kubwa ya vyama 'hivyo' na CDM ni kwamba baadhi ya vyama hivyo vya siasa vimebobea kwenye fani ya usanii, wakati CDM haijabobea kwenye taaluma ya usanii, badala yake wao ni 'specialists' wa FACTS and REALITY.
 
VUTA-NKUVUTE

"SITAKUWA NA HAYA NA MTU AMBAYE HATATEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA UMAKINI PINDI NITAKAPOPATA RIDHAA YA KUIONGOZA NCHI HII"

Nadhani kauli hiyo unafahamu imetolewa na nani....hivi kwa kauli hiyo unadhani wale wanaojifanya viongozi bila kuwa na impact lazma waondoke, sishangai kuona wanaondoka,,,watoto wa mjini wanasema TINGATINGA linakuja lazma watu watafute pa kwenda,,,ila wenye kujielewa watabak huko waliko
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom