Kwanini hupigi kura licha ya kuwa una sifa zinazokuruhusu kufanya hivyo?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Wapo watu wengi wenye sifa za kupiga kura, lakini wamekuwa wakijiandikisha na baada ya hapo hawaendi kupiga kura kuwachagua viongozi wa kuwaongoza, na wengine hawajiandikishi kabisa licha ya kuwa na sifa stahiki na ni haki yao ya msingi ya kikatiba.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa haki kila raia wa Tanzania kupitia Ibara ya 5 (1), kila raia aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura. Lakini Watu wamekuwa wakishindwa kutumia haki hiyo kwa sababu mbalimbali wanazozijua wenyewe.

Kupitia sanduku la kura raia anapata fursa ya kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi anayeona ana sifa za kumuongoza.

Je, ni sababu zipi zimekuvunja moyo au kukufanya uache kupiga kura licha ya kuwa na sifa na unafahamu umuhimu wa zoezi hili?
 
Tume ya uchaguzi inaundwa ma Rais, ambae kama sio anatetea kiti chake basi chama chake kimesimamisha mgombea, halafu matokeo ya Urais yakitangazwa hayapingiki popote, sasa ya nini nikapoteze muda wangu kituoni?
 
Nimeapa kutokupiga kura kwa sababu kuu tatu;

1. Nimegundua pasipo na shaka kura yangu haiheshimiwi, maana mshindi anaamuliwa na mamlaka badala ya mimi mpiga kura!

2. Tume ya uchaguzi siyo huru! Wateule karibia wote wanateuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala.

3. Matokeo ya Rais hayawezi kupingwa na chombo chochote kile cha kisheria, hata kama ni batili/yamepikwa.
 
Siwezi kupiga kura kwa sababu napoteza muda tu kuanzia kujiandikisha mpaka siku ya kupiga kura ilihali mimi 'kula' yangu mpaka nitoke niangaike ndio nipate!

Kwahiyo siwezi acha familia yangu iteseke niende kupiga kura.
 
Nasoma comment mbaka sasa wasiotaka kupiga kula 3 wanaopiga kura 0

Kwa mimi naungana nao wasio piga kula.
 
Back
Top Bottom