Kwanini haya yanatokea kwenye mapenzi?

Kwanini haya yanatokea kwenye mapenzi?

Ila mimi jamani niwe tu mkweli nikimtumia mwanaume wangu text moja tu hasa whatsapp akaiona na ikaweka kabisa blue ticks halafu hajanijibu huwa naanza kuwaza tu hivi kweli mimi ndo ninaiaibisha familia yangu kiasi hiki kwa kujipedekeza namna hii?

Why me Lord? Lord why me? Yaani huwa ninahisi kama vile mbingu na dunia vyote vinanicheka huwa ninaona kama vile nimevuliwa nguo zote nimeaibishwa nimedhalilishwa yaani huwa nawaza mambo mengi sana daah sijui shida ni nini
Aisee ...
 
Baada ya wiki mbili asiniambie tena! Akae nalo akufwe nalo!

Mfano sms za mleta mada hapo juu, wewe unajua mwenzio kapata shida kumbe anatafuta ushahidi wa kuleta JF!

Suala la mazungumzo huwa halikwepeki, ila mimi ni sms moa tuu, na missed call moja baaaasiiii.

Akizikuta hata baada ya mwezi atanitafuta!
Kwa hiyo mtu kama yuko mahabusu ametoka baada ya wiki mbili asikuambie?
 
Mtu na sio babe wangu!
Basi mimi mtu wa kwanza kumuwaza huwa ni babe!
Hata nivurugwe na mchepuko wangu Asprin mtu wa kwanza kumkimbilia ni yeye!
Kwa kweli tunatofautiana, mimi nikivurugwa sitaki kuongea na yeyote wakati mwingine kuepuka usumbufu nazima simu kabisa
 
Kwa kweli tunatofautiana, mimi nikivurugwa sitaki kuongea na yeyote wakati mwingine kuepuka usumbufu nazima simu kabisa
Kweli tuko tofauti!
Akizima simu akiiwasha aniambie vizuri kabisaaa, sababu ya kunizimia simu
 
Hata hivyo tulichokuwa tunaeleweshana sio hiki. Ninyi mnasema kama umemtumia meseji mtu ni LAZIMA atume yeye ndio utamtumia tena, ndio hicho mimi nasema siwezi....naweza nikakupigia simu leo usipokee, nikakupigia kesho usipopokea ntakupigia tena keshokutwa na usipopokea kama kuna means yoyote ya kukupata nitakutafuta nijue kulikoni, nikijua kwamba ulikuwa unafanya makusudi ndio nitaamua nafanyaje tofauti na wewe ambae ukipiga simu nisipopokea hupigi tena hadi nikupigie mimi...kitu ambacho mimi sikiwezi.
Sasa tunaongea lugha moja[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ananipenda sana, ila sina hisia nae hata kidogo...

Hana kasoro yoyote, ana sifa zote kuitwa mke, lakini mimi simpendi...

Hajawai nikosea, kila siku mimi ndio namkosea lakini haniachi..

Ananipenda sana, muda mwingi anazungumza kuhusu ndoa, anawapenda na wazazi wangu pia

Sijui kwanini mimi simpendi, yani namtamani tu pale napokuwa N.y,ege..

Kwa mambo makubwa alionifanyia naogopa kumwambia simpendi.. Nahis anaweza ata kuniua

DAH,
View attachment 1135849View attachment 1135850View attachment 1135851
Sio kosa lako demu ndio anazingua kuna mambo demu akifanya yanakukata mood kabisa mfano demu kutuma messages zaidi ya mbili wakati hajajibiwa inakera sana...
 
Kweli tuko tofauti!
Akizima simu akiiwasha aniambie vizuri kabisaaa, sababu ya kunizimia simu
Sio kwamba nakuwa nimemzimia mtu, simu ni ya kwangu nna uhuru wa kuzima na kuwasha kwa kadri ninavyojisikia as long as sina miadi na mtu
 
Yani adi nashangaa, yupo tayar kufanya chochote ili mradi tu mapenzi yetu yaendelee... Kila nikileta kisingizio cha kuachana..anatatua na wala hajali
Ngoja apate ujauzito ndiyo utaoa kabisa sahizi kazana kazana utaitungisha tu hapo upendo utakuja tu
 
Dada hebu kuwa serious aki!
Mahabusu two weeks na nisijue?! Anaishi na mie kama nani sasa!
Sasa utajuaje kama ukituma meseji mara moja usipojibiwa hutumi tena wala kupiga mpaka pale atakapojibu meseji yako? Kumbuka hapa hatuzungumzii mume tunazungumzia mpenzi/ mchumba ambae mnaishi makazi tofauti tofauti pengine hata miji ni tofauti.
 
Hata hivyo tulichokuwa tunaeleweshana sio hiki. Ninyi mnasema kama umemtumia meseji mtu ni LAZIMA atume yeye ndio utamtumia tena, ndio hicho mimi nasema siwezi....naweza nikakupigia simu leo usipokee, nikakupigia kesho usipopokea ntakupigia tena keshokutwa na usipopokea kama kuna means yoyote ya kukupata nitakutafuta nijue kulikoni, nikijua kwamba ulikuwa unafanya makusudi ndio nitaamua nafanyaje tofauti na wewe ambae ukipiga simu nisipopokea hupigi tena hadi nikupigie mimi...kitu ambacho mimi sikiwezi.
Huwa kama kuna tatizo kuna ndugu watanijulisha tuu!

Umeona sms za mdada lakini, zenyewe ni za muda tofauti na siku tofauti!

Matokeo yake ndo haya sasa, mwenzake anatafuta ushahidi wa kuleta JF!
 
Mimi ni mwanaume wapo kweli wenye kushow love for me but siwapendi lakini huo unaoufanya ni zaidi ya unyama moto wako unaandaliwa kuni za reli maana miti hutaungua vizuri yaani mtoto wa wa watu kajibebisha mpaka kawa baby kweli lakini unamkaushia hivyo hembu geuza shilingi Kwa upande mwingine ingekuwa wewe ndo unafanyiwa hivyo ungekuwa na hali gani? Mnyooshee mtu kama humtaki ili aangalie sehemu ya kweli,, ataumia sana ukimwambia ukweli ila atapona tofauti na kuwa kimya akija kujua na kuambini mwenyewe ataumia sana na kidonda chake hakiponagi Kwa muda sana
 
Sio kwamba nakuwa nimemzimia mtu, simu ni ya kwangu nna uhuru wa kuzima na kuwasha kwa kadri ninavyojisikia as long as sina miadi na mtu
Siku ya babe wangu ni yangu na yangu ni yake!
Amevurugwa ameamua kuzima simu, basi anijulishe! Siko na mood sakayo nazima simu!
 
Huwa kama kuna tatizo kuna ndugu watanijulisha tuu!

Umeona sms za mdada lakini, zenyewe ni za muda tofauti na siku tofauti!

Matokeo yake ndo haya sasa, mwenzake anatafuta ushahidi wa kuleta JF!
Hapo kwa ndugu si mpaka wawe na namba yako sasa na hata kama MNA mawasiliano pia wanaweza kuchelewa kukujulisha. Tufanye basi sio wiki mbili, ni siku tatu
 
Hapo kwa ndugu si mpaka wawe na namba yako sasa na hata kama MNA mawasiliano pia wanaweza kuchelewa kukujulisha. Tufanye basi sio wiki mbili, ni siku tatu
Mahabusu siku tatu zote hizo jamanii!
Nijuavyo pale unapewa nafasi ya kutoa taarifa kuwa uko polisi!

Akiwa kwenye shida anijulishe, na kwenye raha pia! Nini maana ya wapenzi sasa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom