Kwanini haya yanafanyika Zanzibar?

Kwanini haya yanafanyika Zanzibar?

...kwa sababu yeye si mwanachama wa chama Fulani, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?
If you can't fight them, join them..
Kwa kuwa huo mfumo wa chama wa kibaguzi huwezi kuuondoa kwa sasa, nunua kadi yao upate kazi bro
 
If you can't fight them, join them..
Kwa kuwa huo mfumo wa chama wa kibaguzi huwezi kuuondoa kwa sasa, nunua kadi yao upate kazi bro
Ushauri mzuri, ila mimi sina mpango wa kuajiliwa kwenye taasisi zao wala serikalini,
Niko na mishe zangu.

Ila tu utaratibu wao kwa kizazi cha sasa na kijacho ni mbovu wa kibaguzi kwa makundi fulani fulani ya raia wake na hamna hatima njema ndani yake kama hawatabadilika.
 
kumbe inshu ipo serious, kuna mtu aliniambia ameenda azam marine kutuma kadi ya chama iende zanzibar.
ila mtoa mada usijeeneza uvumi kama hauna taarifa za kweli, chonde chonde.

anachoongea ni ukweli mtupu, Zanzibar huwezi pata ajira yoyote ya Serikali bila ya kuwa na kadi ya CCM na cheti cha kuhitimu somo la Itikadi la CCM.
 
Wana Jf bila shaka mpo salama,
Hongereni kwa majukumu ya kutwa zima ya ujenzi wa uchumi mtu mmoja mmoja, Familia na Taifa,

Bila kuwachosha nijielekeze kwenye hoja yangu,

Kwa Zanzibar unakuta kuna malalamiko sana chini kwa chini hasa linapokuja swala la kuajiliwa kwenye taasisi za serikali na hata kwenye vikosi mbali mbali za majeshi, Jku, Kmkm, Valatia nk.

1. Unakuta vijana wana sifa zote za kuajiliwa, elimu wako vizuri.

2. Ni raia halali wa nchi.

3. Vipimo vya afya vinaonyesha wako fit.

4. Vitambulisho vyote wanavyo nk.

Lakini tu kwa sababu yeye si mwanachama wa chama Fulani, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?

Hawa mnaowaweka kando kisa tu si wanachama mnakuwa mpo sahihi kwa kiasi gani?

Hawa vijana ni raia wa nchi yenu wanazo haki zote za kikatiba juu ya nchi yao ikiwemo kulitumikia taifa lao kwenye nyanja mbali mbali.

Leo hii kwenye baadhi ya taasisi mfano Hospital ya Mnazi Mmoja, baadhi yao wameajiliwa hawana vigenzo lakini tu kwa sababu ni wanachama wa chama chenu wametumika kupiga kura 2015 au 2020 wanapata upendeleo wa kuajiliwa, mwisho wa siku ukienda Mnazi Mmoja hospital unakutana na baadhi ya watoa huduma wenye kauli mbovu kwa wateja, wavivu wa kazi, watoro wachelewaji hawana weledi na kazi zao, hawana ubunifu, wenye sifa wengi wao mnawatupa nje ya mfumo.

Je, mnajenga taifa la namna gani?

Je, Tanzania bara nako haya hayapo maana chama ni hicho hicho?

Watanzania wengi tunajinasibu wacha Mungu kupitia dini zetu, Uislamu, Ukristo nk je dini zetu zinaruhusu ubaguzi?

Kubangua watu kwa sababu ya chama kwenye ucha Mungu ruksa?

Ikifika Kwaresima, Ramadhani full kufunga, swala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
"Kubangua" hawa vijana "kuajiliwa" ni sahihi kabisa kwa sababu hawajui kuandika.
 
anachoongea ni ukweli mtupu, Zanzibar huwezi pata ajira yoyote ya Serikali bila ya kuwa na kadi ya CCM na cheti cha kuhitimu somo la Itikadi la CCM.
Daaaah, na wazee wanaona sawa kabisa kuendeleza ubanguzi
 
Ukichunguza ki undani wengi wanaofunga Kwaresma au Ramadhani, wanafunga ni kama wanajishindisha njaa tu, maana matendo yao hayaendani na wanachokifanya., Ubaguzi, unafiki, u chawa, uzinzi, ufirauni n.k yote haya huwa wanasitisha kwa muda tu baada ya mwezi kuisha wanarudia yale yale.
Wengi kuna jambo wa ajifichamo jamii isiwajue ila ni watu wa hovyo sana
 
Si Bora Zanzibar wanaangalia chama,huku bara ukiwa na sijda usoni kupata kazi labda ukatambike,ubaguzi wa ajira Kwa kuangalia Iman ya mtu,kabila,rangi na chama chake na kadhalika ni jambo la kulaaniwa kabisa.
 
Si Bora Zanzibar wanaangalia chama,huku bara ukiwa na sijda usoni kupata kazi labda ukatambike,ubaguzi wa ajira Kwa kuangalia Iman ya mtu,kabila,rangi na chama chake na kadhalika ni jambo la kulaaniwa kabisa.
Mkuu THE BIG SHOW hakika kwa ustawi na kwa maslahi mapana ya taifa kubagua baadhi ya jamii si jambo njema.
 
Back
Top Bottom