Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,414
- 64,649
Maskini ni kama Inspiration Speaker anashauri vitu ambavyo yeye mwenyewe hafanyi.Katika ukuaji wangu huu sijawahi kuona mtu yeyote yule akienda kuomba ushauri kwa maiskini.
Sababu kuu itakuwa ni nini?
Tunawadharau, Hawana mawazo, Hawana dira, Ubongo wao haufanyi kazi au Sababu inaweza kuwa ipi?
FafanuaMule mule
Kwa hiyo sababu kuu ya kutotaka ushauri wao ni nini?Maskini ni kama Inspiration Speaker anashauri vitu ambavyo yeye mwenyewe hafanyi.
Au mganga anayekupa utajiri wakati Watoto wake ni maskini wa Kutupwa.
Kwa upande wako, ulishawahi kuomba ushauri kwao?Yote ni kwa sababu tunaishi kwenye jamii yenye fikra potovu, jamii inayochanganya ukubwa wa pochi na ukubwa wa akili, ikiamini kuwa maskini hawezi kuwa na hekima, jambo ambalo ni la kijinga na la aibu sana.
Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.Maskini ni kama Inspiration Speaker anashauri vitu ambavyo yeye mwenyewe hafanyi.
Au mganga anayekupa utajiri wakati Watoto wake ni maskini wa Kutupwa.
Siyo mara moja, ni watu ambao napenda kuwa nao karibu zaidi ili kujifunza zaidi.Kwa upande wako, ulishawahi kuomba ushauri kwao?
Labda ni huko ulikokulia. Mimi nimekulia kijijini na katika watu waliokuwa wanafuatwa kwa ushauri ni mama mmoja aliyekuwa anaishi kwenye kibanda cha nyasi. Ni kesi gani ingefanyika bila yeye kuombwa kwenda kusikiliza na kutoa ushauri? Ni mama mmoja alikuwa na busara mno. Kwa uapnde mwingine alikuwepo baba mmoja alikuwa tajiri lakini watu walikuwa wanamwita jina la utani wa''lijinga'' (kwa kilugha lakini). Napingana kabisa na hii dhana yako.Katika ukuaji wangu huu sijawahi kuona mtu yeyote yule akienda kuomba ushauri kwa maiskini.
Sababu kuu itakuwa ni nini?
Tunawadharau, Hawana mawazo, Hawana dira, Ubongo wao haufanyi kazi au Sababu inaweza kuwa ipi?
Sema wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi. Asante sana. Jamaa amepotosha kabisa na nadhani anaweza kuwa mtoto wa juzi juzi ambaye hajapambana na maisha. Kwa kiwango kikubwa kwenye jamii yetu watu wanaofutwa kuombwa ushauri ni watu wasio matajiri.Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.
Maskini anaweza kukupa ushauri mzito unaoweza kukuokoa, kwa sababu ameliishi janga hilo. Tajiri anaweza kukuangusha kwa ushauri wa mazoea yasiyoendana na uhalisia.
Fundi hatengenezi gari anarekebisa matobo na kufunga nati zilizolegea.Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.
Na bahati mbaya matajiri nao hawatwambii njia za utajiri hata akisema basi ni uongo.Huwezi kushauriwa kitu na mtu aliyeshindwa kufanya hicho kitu hata kama mawazo yake ni mazuri..in short unatakiwa kutajirika kwanza ndo utoe ushauri
HeheheMaskini atakushauri nini zaidi ya kukwambia nunua uwanja ujenge!
Hakika, hili nimeli- experience pia.Sema wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi. Asante sana. Jamaa amepotosha kabisa na nadhani anaweza kuwa mtoto wa juzi juzi ambaye hajapambana na maisha. Kwa kiwango kikubwa kwenye jamii yetu watu wanaofutwa kuombwa ushauri ni watu wasio matajiri.