Ndikwega
R I P
- Feb 1, 2012
- 5,979
- 5,524
Moja ya jambo ambalo linanisikitisha kwa Mh ni hili la kujihami. Amekuwa mtu aliyetengeneza mazingira ya kutokosolewa, akikosolewa tu basi ujue umejitakia matatizo lolote linaweza kukuta.
Ili kudhihirisha hili moja kuonesha hofu hiyo aliagiza Bunge lisioneshwe mubashara kuhofia kuwa wananchi watashuhudia mijadala mbali mbali ya kukosoa utawala wake na kuibua madudu kitu ambacho inaonekana hafurahishwi nacho. Walikuja na kisingizio cha gharama, lakini walipojitokeza wadhamini was vipindi vya Bunge wakaja na sababu ya kupoteza muda badala ya kufanya kazi. Hizi ni sababu dhaifu mno.
Jambo lingine ni kamata kamata ya watu walioonekana kuhoji mambo anuai kwa yeye ama utawala wake, mathalani Godbless Lema na sasa Ben Saanane kapotea na haijulikani kapotelewa wapi na Serikali imekaa kimya. Japokuwa inafahamika kuwa naye alihoji PhD ya Mkuu.
Vyombo vya Habari pia vimetungiwa sheria ambayo inavikandamiza. Hii ikiwa na maana kwamba habari za kuandika ni zile za kusifia Utawala tu.
Je, ni kweli Mungu anaruhusu haya yanayotekea maana tumeambiwa tumuombee kwa Mungu?
Kwanini hataki Kukosolewa na hali ni Binadamu?
NB: Mh Ungewaacha Waongee mwisho wake watatulia wenyewe, wapuuze tu na hawana madhara kwako maaana wewe ndiwe Boss.