Nani wa kumfunga paka kengele au tuendelee kuyageuza mawe kuwa mkate?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kumekuwa na tuhuma kuwa wapinzani hawana hoja zaidi ya kutegemea kuteleza kwa serikali ndiyo wapate hoja za kuongea. Huenda hili ni kweli lakini nikumbushe kuwa siasa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu, jinsi unavyo tengeneza makosa ndiyo unatengeneza nafasi za kufungwa zaidi na kupoteza mchezo.

#UPINZANI upo kimkakati kuhakikisha serikali inapoteza mchezo kutokana na makosa yake, hii ni credit kubwa sana kwa wapinzani kuonyesha udhaifu wa serikali, kuwa imeshindwa kuiongoza nchi kwa kufuata misingi ya utawala bora. Ndiyo maana haitajika nguvu kubwa kuonyesha madhaifu ya serikali.

MAKOSA MAKUBWA YA SERIKALI:

Ni kukubali kuendelea kufanya makosa ya wazi wakiamini watalindwa na vyombo vya dola kwa kuwa viko chini yake, bunge ambalo kwa wingi wa wabunge wake toka chama kinacho tawala na mahakama.

VYOMBO:

Vyombo vya dola hususani jeshi letu la POLISI limekuwa jeshi la kulinda usalama wa serikali na CCM kwa misingi ya kuhakikisha serikali ya CCM pamoja na udhaifu ya serikali haidondoki , hii imekuwa kinga kubwa na kuijengea CCM na serikali yake kuwa serikali jeuri kuliko serikali zote za chama hicho zilizopita.

BUNGE:

Limekubali kuacha majukumu yake na kuwa mhuri(rubber stamp) kwa lengo kuu moja, kubariki madhaifu ya serikali na kulinda chama chao kisipoteze serikali.

Udhaifu huu wa bunge ndiyo unaoibua hoja kwa wananchi kuwa bunge letu ni dhaifu. Udhaifu wa bunge ni kukubali kuwa idara ya serikali inayopokea madaraka na majukumu yake kwa mujibu wa serikali na siyo katiba.

Tumeona maazimio mengi ya bunge yakipuuzwa kwa njia moja au nyingine ili kuzuia uovu wa serikali. Mathalani kiti cha spika kuitisha ofisi ya CAG kutofanya nayo kazi ili tu ripoti yake kuhusu matumizi ya hovyo ya fedha za serikali isijadiliwe bungeni.

Tumeona bunge likikataa kuunda kamati za uchunguzi wa usalama wa raia hususani vitendo viovu vya vitisho kwa wabunge wanaoibana serikali bungeni, matokeo yake ni kushambiliwa kwa Mbunge mh. Lissu akitokea bungeni lakini bunge likiwa kimya.

Tumeona sheria ya bajeti ikikanyagwa kwa makusudi na serikali kutumia udhaifu huo wa bunge kufanya maamuzi ya kibajeti bila idhini ya bunge. Kwa hali kama hii serikali imekuwa kinara na isiyo ambilika kwa kuwa mihimili mingine imekubali Kuwa idara za serikali.

MAHAKAMA ;

Imekuwa eneo lisilo salama likipokea maelekezo ya maamuzi yatokanayo na jukwaa la siasa. Si ajabu Leo ukasikia rais akiagiza mahakama na kutoa hukumu ilihali kesi hizo zipo mahakamani.

Mhimili huu mkubwa ambao ndiyo nguzo ya utetezi wa haki wenye kulinda haki za wananchi ikipoteza kuaminika tusitegemee nchi kuwa salama. Tumeona nchi nyingi duniani zikiingia kwenye migogoro mikubwa kutokana na mwingiliano na mgongano wa kimaslahi kwa mihimili hii mitatu.

Leo hii baadhi ya mahakimu katili kwa makusudi wameamua kupokea maelekezo toka juu ili kuharibu mwenendo wa mashitaka ili kudhibiti mashinikizo toka kwa wakosoaji wa mwenendo wa serikali.

Leo hii ukitumia nguvu zako kimamlaka kuzuia sauti za malalamiko ya wanyonge dhidi ya udhalimu wa serikali una pandishwa cheo. Hii ni hatari kwa mustakabali wa amani yetu. Ikumbukwe uvumilivu una kikomo, tusiuchezee uvumilivu walio nao wananchi, uvumilivu huu ndiyo tunda la amani hii mnayojivunia sasa, ukipotea nchi hatakalika.

#Bahati mbaya sana ni kuwa wanaharakati waliopaza sauti zao kuzuia maovu ya serikali wameungana kwa kukubali vyeo na kuwasaliti wengi wanaopigana haki za uhuru.

Walionekana wana kiburi cha kiharakati wamegeuzwa maadui wa taifa kwa kupigwa risasi, kutekwa na kupotezewa kusikojulikana, na wengine kuwekwa gerezani kwa makosa ya kutengenezwa.

#Nguzo kubwa iliyokuwa inategemewa ni taasisi ya maadili ambayo ni DINI,. Tumeona rais akikutana na viongozi wa Taasisi hii, lakini ajabu walicho kiwakilisha kwa rais ni kinyume na WARAKA WA PASAKA, ni kinyume na BARAZA LA MAASKOFU. Wameshauri mambo madogo madogo yale yanayo ipasua nchi na kuuwa mshikamano wa kitaifa wamerudi nayo kwenye kanzu zao na majoho yao, lakini wamegeuka kuwa tishio kwa wakosoaji wa serikali.

Ikiwa hata viongozi wa dini wanamuogopa mtawala nani atamvika paka kengele!!!!!!

Wenye uwezo wa kumwambia ukweli ndiyo hataki kukutana nao kwa kuwa si wanafiki na kwa kuwa hapendi kukosolewa hawa atawashughulikia kwa uwezo wa mamlaka aliyonayo.

Kwa hali hii nchi imejawa na hofu kama iko vitani, kila mmoja amegeuka msaka tonge akilinda ugali wake ili asije upoteza kabisa. Nabii Issa (AS) alipojaribiwa na shetani aliambiwa ageuze mawe yawe mkate ili aondokane na njaa aliyokuwa nayo, lakini alisema hatuishi kwa kula mkate tu, aliendelea kupinga batili na kuisimamia imani yake bila kujali mateso ya mwili wake, je sisi tunajivunia nini kutoka kwake, tumekubali kugeuza mawe kuwa mkate ili kulinda dhamana zetu na kuwaacha wengine wateketee!!!!??
 
Umetoa sana shutuma mkuu, m nilitegemea ungekuja na critical analyisis badala yake umekuja kulaum tu, kipengele namba 2 kimekosa hoja tetezi kabisa, it mostly based on what you heard
 
Umetoa sana shutuma mkuu, m nilitegemea ungekuja na critical analyisis badala yake umekuja kulaum tu, kipengele namba kimekosa hoja tetezi kabisa, it mostly based on what you heard
Haya uzi mpyaaa LUMUMBA KASHADANDIA!!

YAANI YOTE ALIYOELEZA HUJAONA YANA UKWELI!!!

HALAFU UNAKUJA NA HITIMISHO LA KITOTO KABISA

'' it mostly based on what you heard "
 
Sawa mkuu, ila mbona hoja yangu haijajibiwa hapo
HOJA ZA MTOA MADA NI :-
KUKAMATA MIHIMILI MINGINE ILI IIUNGE MKONO SERIKALI MIFANO KATOA.
WABUNGE KUTISHIWA MAISHA (ZZK),
KUDHURIWA (TAML),
SPIKA KUTISHIA KUTOFANYA KAZI ZA CAG.
SIWEZI KURUDIA POST NZIMA.

WE HOJA YAKO NI NINI KWA MFANO??
***UWEZO WAKU WA KUFIKIRI KUJENGA HOJA NA KUZITETEA UNAFANANA NA ULUMUMBA WAKO***
 
HOJA ZA MTOA MADA NI :-
KUKAMATA MIHIMILI MINGINE ILI IIUNGE MKONO SERIKALI MIFANO KATOA.
WABUNGE KUTISHIWA MAISHA (ZZK),
KUDHURIWA (TAML),
SPIKA KUTISHIA KUTOFANYA KAZI ZA CAG.
SIWEZI KURUDIA POST NZIMA.

WE HOJA YAKO NI NINI KWA MFANO??
***UWEZO WAKU WA KUFIKIRI KUJENGA HOJA NA KUZITETEA UNAFANANA NA ULUMUMBA WAKO***
unatumia nguvu kubwa sana mkuu, msomi hafananii hivyo, badala ya kujenga hoja unapandikiza chuki. ni makosa sana kwa aliyekupa kadi kwenye tawi lenu
 
Umetoa sana shutuma mkuu, m nilitegemea ungekuja na critical analyisis badala yake umekuja kulaum tu, kipengele namba 2 kimekosa hoja tetezi kabisa, it mostly based on what you heard
Makosa ya serikali yanalindwa na vyombo vya dola, bunge na mahakama. Kila anayeionyooshea kidole serikali huyo ni adui wa taifa ana shughulikiwa kuliko wahujumu uchumi, bunge limekuwa la kimkakati kuhakikisha maovu ya serikali yanalindwa kwa gharama yeyote ile, ndiyo maana mambo makubwa yanaitafuna nchi yanabaki kwenye meza ya spika. Wabunge wanatishwa ndani ya bunge mpaka nje ya bunge.
 
soma kipengele kinachozungumzia makosa ya seriakali hoja zingine atleast zimetolewa utetezi ila hio imeelezwa juujuu
Makosa ya serikali nime categories jinsi vyombo vya dola, bunge na mahakama vinavyo shindwa kusimamia majukumu yake na kukubali kuwa idara ya serikali
 
Back
Top Bottom