Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,654
Naomba nianze na kudeclare interest. Mimi sio mshabiki wa CCm wala Magufuli. Ni mshabiki wa vyama vingi. Napenda utawala wenye viongozi wenye maono au challenge mbalimbali.
Tunavyoelekea uchaguzi mkuu mwaka huu. Naomba nitoe mapendekezo binafsi kwa watanzania wenzangu tunaojiandaa kushiriki uchaguzi wa viongozi wetu.
Utawala wa Rais Magufuli ni utawala wenye Mazuri mengi huku mabaya nayo yakiwa mengi. Maana yake anahitaji kukosolewa na kushauriwa sana.
Kitu nachoweza sifia utawala huu ni kuweza kusimamia rasilimali za nchi hii ili kukuza uchumi wa Tanzania. Kweli tumeona maendeleoa mengi yamefanyika.
Hii maana yake Watanzania Tunamuhitaji Magufuli sana aendelee kuwepo ili Tupate manufaa ya Utawala wake. ( Simaanishi aendelee kutawala zaidi ya miaka 10)
Ila tatizo linakuja kwenye Hawa wabunge wa CCM. Wengi ni Pasua kichwa. Sioni wanachomsaidia Rais Magufuli zaidi ya Kumsifia na kumtukuza ilimradi waendelee kukaa kwenye viti vyao vya ubunge au wapate teuzi mbali mbali.
Wabunge wa CCM sasa wamebadilisha Mbinu ya kuendelea kukaa madarakani. Badala ya kutetea wananchi na kupigania maendeleo katika majimbo yao. Wamebaki kuwa waimba mapambio tu bungeni na Kutukana wapinzani wakiongozwa na spika wao wa bunge ambye ninamashaka sana kama psychologically yupo vizuri
Mh Rais, Unahitaji wabunge wa Upinzani sana kuliko hawa wa chama chako. Hawakusaidii chochote zaidi ya kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili waendelee kula tena wengi wanatafuta mianya ya kukuibia tu.
Wananchi nao hatuoni utendaji wa hawa wabunge, nje na ndani ya Bunge. Kwa kifupi hawa wabunge wapo bungeni lakini hawajuu wajibu wao kama wabunge.
Kazi kuu za Bunge ni:
1) Kumhoji waziri yeyote kuhusu masuala ya umma yaliyo ndani ya dhamana yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2) Kujadili utendaji wa kila wizara wakati wa kikao cha mwaka cha Bunge la bajeti;
3)Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaotakiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
4)Kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji sheria na;
5) Kujadili na kuridhia mikataba na makubaliano ambayo Jamhuri ya Muungano ni mhusika na masharti yake yanahitaji idhini.
Wananchi wenzangu nawashauri Tukienda kwenye uchaguzi, tuhakikishe Rais Magufuli Tunampa kura zote ila wabunge mizigo wengi tuwakate mapema. Hatuhitaji Bunge lenye sauti moja ni bora lisiwepo kabisaa posho zao zikafanya maendeleo mengine.