Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Huyu kumfuga labda awe kwenye kundi ambapo nadhani ni gharama sana na ukisema umfuge peke yake ni hatari maana nyati anapokuwa peke yake anahisi kuwa kwenye hatari so anakinukisha mda wowote. Ni hatari sana kukumbana na nyati akiwa mwenyewe kachengana na kundi lake ndo maana akiwa mmoja anaitwa mbogo. Labda mumfuge ila kila siku awe anapigwa tranquilizer
 
chui ni hatari, huyu sio wa kumfanyia masihara kabisa kabisa.. ukitaka kujua kwamba hanaga muda wa mazoea
1. hawaishi kwa makundi, labda mama akiwa analea watoto
2. mating yao ni for the purpose ( yaani jike na dume wanakutana kwa ajili ya uzalishaji tu) so kunamfanya awe ni kiumbe ambacho muda wote awe mawindoni
3. hali chini ( hula juu ya mti, anapanda na kitoweo juu ya mti), ni nadra sana kumkuta anakula chini
hana mazoea ya hovyo
Ni mchoyo na anajua msosi ukikaa chini fisi au simba watampora tu
 
Nyati ukimkuta kajitenga peke yake porini usimkaribie ni hatari zaidi ya hatari tofauti akiwa katika kundi pamoja na wenzake.

Wanayama wawili porini ambao muda wote wao wana hasira ni Kifaru (faru) na Nyati.

Hatari yao kubwa ni pembe zao zilizochongoka ila mbaya zaidi ni kifaru na wanakimbia balaa
Kuna siku niliona ugomvi wa nyati na faru ni hatari, hebu fikiria lile pembe la faru lilivochongoka ila nyati ni chizi anaenda kujigongesha pale mwisho wa siku nyati alikimbizwa baada ya kuchotwa na lile la faru akangua chini faru akataka kwenda kummalizia chini pale nyati akasepa
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Umeshasema Tembo na Nyati wa India,sasa wadanganye waje wajichanganye kutaka kufuga hawa wa huku kwetu...
 
Watu wamekariri simba simba simba.

Kipori pori simba ni paka mkubwa tu,kula yake ni ya shida na shuruba nyingi,tofauti na anvyoonekana ni mnyama asiyejiamini kabisa,ndio maana unaweza mkimbiza na akakimbia,usijefanya hii kwa chui ama nyati usijaribu kabisa wala kuwaza.

Ujasiri wa chui angekuwa na umbo kubwa kama la simba,hakuna mnyama angemsumbua.
Chui anachoka haraka. Niliona jana kwenye documentary, kuwa ana kasi ila inabidi awahi kukamata kwasababu anachoka haraka
 
Huyu mungu alijua kumkomesha hizo pembe zingikuwa zimechongeka kuangalia mbele yaani simba wangekuwa wanakufa sana.
Acha kabisa, hujakuta kakojea mkia wake akauvuruga chini akakurushia tope lenye mkojo hata kama umekumbatia tawi utashuka tu huyu hana adabu kabisa
 
Acha kabisa, hujakuta kakojea mkia wake akauvuruga chini akakurushia tope lenye mkojo hata kama umekumbatia tawi utashuka tu huyu hana adabu kabisa
ni kisarani kwelikweli huo mkojo hamna cha baunsa wanamwelewa ndo maana.
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Ni kweli kabisa
 
yule mwamba hata simba huwa wanajipanga haswa sio mmoja na wakija kundi simba anachezwa danadana kaa mpira.
Yule hua hanogi mpaka wamuangushe chini, mmoja adande na koromeo, mwngine adande na uti wa mgongo, mwengine wadhibiti miguu ndio akae
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Tatizo lipo kwenye majani wanayo kula nyati wa india wakila majani magumu saaaana ni ukoka ila hawa wa Tz wanaotega mpaka bhangi zilizopandwa porini kinyemwela
 
Yule hua hanogi mpaka wamuangushe chini, mmoja adande na koromeo, mwngine adande na uti wa mgongo, mwengine wadhibiti miguu ndio akae
kabisa mkuu na wakiwa simba wawili nanaweza tembea nao haaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom