Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Nilikuwa na jamaa ila Sasa ni marehemu,alikiwa jangiri kubwa tu na kwenda porini kuuwa wanyama.

Wanasema Kuna siku walikutana na nyati porini Kwa bahati mbaya akiwa peke yake,ile kashkash ya pale porini iliwafanya Kila mtu arudi peke yake nyumbani.

Kiumbe hatari sana kama utajaa kwenye 18 zake
 
Ukiona tu pua ilivyo na pembeni zake hutatamani kumfuga. Akikufukuza ujifanye unapanda kwenye mtu, mwamba anakojolea mkia wake na anakurushia mkojo ukiwa juu ya mtu. Mkojo unavyowasha utadondoka nae atakumaliza. Ni WA kufuga??
Hii inatokana na uwezo wetu wa kupigania uhuru wetu, Unanifuga kwa nini? Kwa nini unipangie sehemu za kutembelea?
No way hapa FULL DEMOCRACY wakuu
 
Ukiona tu pua ilivyo na pembeni zake hutatamani kumfuga. Akikufukuza ujifanye unapanda kwenye mtu, mwamba anakojolea mkia wake na anakurushia mkojo ukiwa juu ya mtu. Mkojo unavyowasha utadondoka nae atakumaliza. Ni WA kufuga??
Uongo story za kitoto unatuletea watu wazima!! Ukipanda kwenye mti anakusubiri tu hizo hekaya za kurusha mkojo ni uongo
 
sawa, wanyamapori ni wa serikali, kwa nini kusiwepo mpango wa kukamua maziwa yao na yakauzwa kwa wananchi kama chakula bora ikiwa nyama zao ni nongwa wasije wakaisha kizembe? Wanyama kama hawa kina nyati, nyumbu, pundamilia, twiga, paa, tandala na swala ni wa kukamuliwa maziwa yao kwa ajili ya lishe kwa wananchi. Nyama, pembe na ngozi zao ni nongwa, hata maziwa yao nayo iwe nongwa, lini wananchi watafaidi maliasili zao?
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Water buffalo ni tofauti na hawa wa kwetu
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Wale wanaitwa Asian water buffaloes aka (mbogo maji) maana wanapenda kutumia muda mwingi katika mazingira ya maji maji tofauti na huyu African buffalo ambaye ni mbogo wa nchi kavu.

Asia water buffalo anatumiwa katila shughuli za kilimo kwasababu ana nguvu sana tofauti na ng'ombe wa kawaida ila huyu mbogo wa kiafrica ni ngumu kumfuga na kumtumia katika shughuli za kilimo kutokana na kuwa mkali sana (aggressive) anaweza kuua mara moja .
 
Nyati ukimkuta kajitenga peke yake porini usimkaribie ni hatari zaidi ya hatari tofauti akiwa katika kundi pamoja na wenzake.

Wanayama wawili porini ambao muda wote wao wana hasira ni Kifaru (faru) na Nyati.

Hatari yao kubwa ni pembe zao zilizochongoka ila mbaya zaidi ni kifaru na wanakimbia balaa
 
Simba si hatari sana, huyu unaweza kutana nae porini na asikufanye kitu
Chui ni hatari kuliko kawaida, akili yake huwa inawaza kuua tu na si vinginevyo, yaani kwanza lazima akuue mambo mengine yafuate... unaweza bahatika ukapambana nae akakujeruhi.. lakini ni m'baya sana

Watu wamekariri simba simba simba.

Kipori pori simba ni paka mkubwa tu,kula yake ni ya shida na shuruba nyingi,tofauti na anvyoonekana ni mnyama asiyejiamini kabisa,ndio maana unaweza mkimbiza na akakimbia,usijefanya hii kwa chui ama nyati usijaribu kabisa wala kuwaza.

Ujasiri wa chui angekuwa na umbo kubwa kama la simba,hakuna mnyama angemsumbua.
 
Ukiwa Tabora kuna ZOO kama unaenda National kuna kila aina ya wanyama lakini huyu mwamba hayupo.

Kule sijui Arusha kuna shamba la kufuga wanyama na watu wanacheza mpaka na Simba, lakini hili dume Nyati halipo.

Nini shida mpaka huyu mtemi anaogopwa kufugwa.View attachment 2584899
Huyu jamaa sio wa mchezo mchezo akikugeuzia kibao ndio utajua hujui
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom