Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Kwanini hakuna Zoo ya kufuga Nyati?

Nadhani kutunza jamaa yako ni kazi kweli kweli kiasi cha kuweza kutumia kuliko anachoweza kuzalisha. Si huyo tu. Iko wapi zoo ya twiga, tembo au fisi?
Fisi wanatunzwa. Shinyanga Wasukuma wanacheza nao ngoma. Tembo kuna ZOO Arusha wanafunga na kucheza nao kuna Mhindi mmoja anafuga Tembo. Sijaona Nyati.
 
India Nyati wanafugwa kama ng'ombe tu na wafugaji wa kawaida tu vijijiji na huwatumia kulima mashambani na kukokota mikokoteni ya mizigo

Waweza pishana nao kibao wakichungwa na kijana mdogo tu kupelekwa malishoni

India hata tembo wanafugwa majumbani vijijini na hutumika kwa kazi mbalimbali za kilimo na kubeba mizigo na hata kuwatumia kama punda .mtu anapanda tembo anaenda aendako
Nyati maji wale,nyati mnyama umfunge jembe alime majaluba!?..acha dharau bro!!
 
Ukiwa Tabora kuna ZOO kama unaenda National kuna kila aina ya wanyama lakini huyu mwamba hayupo.

Kule sijui Arusha kuna shamba la kufuga wanyama na watu wanacheza mpaka na Simba, lakini hili dume Nyati halipo.

Nini shida mpaka huyu mtemi anaogopwa kufugwa.View attachment 2584899
Hivi zoo ya tabora Ina WANYAMA siku hizi!!?..Mara ya mwisho nilienda 94-97,hapakua na kitu zaidi ya kichwa Cha nyati langoni,palikua na Simba zamani pale,Kuna siku akatoka,walevi vilabuni walijificha nyuma ya tairi la baiskeli,ilikua patashika
 
Nyati ( mbogo) , Huyu wenyewe maofisa wanyama pori wanamuita FIELD FORCE, wanyama wengine wote , wakichachamaa na kuvamia maeneo ya WANANCHI kuwaswaga kuwarudisha porini ni rahisi tu.

Lkn miamba hii NYATI (MBOGO) msamiati wa kurudi nyuma wao HAWANA. ni mapambano kwenda mbele, jamaa alinisimulia kuwa waliwakamata MAJANGILI wakiwa wametega mtego na tayari NYATI kanasa!!.

Wale maofisa wa wanyamapori wakawapa MAJANGILI sharti la kuwaachia ni wao MAJANGILI waende wakautegue ule mtego ili NYATI anasuke.

MAJANGILI wakagoma katakata wakasema sharti hilo ni bora tu , wawapeleke kwenye mkono wa sheria. Lkn kwenda kumnasua NYATI akiwa HAI hawawezi kuthubutu.
 
Black Death(African Buffalo),
Hata ukienda mbuga za wanyama, Warning ya kwanza ni ukiona nyati hakuna cha kumuangalia usoni wala kujivimbisha, option ni mbioo,
Screenshot_20230412_101709_WhatsApp.jpg
ukichoka lala japo kulala ndio option ya mwisho lakini ni hatari pia, lazima akutest na pembe, huwezi vumilia, kosa ambalo litakupeleka pluto.
 
Fisi wanatunzwa. Shinyanga Wasukuma wanacheza nao ngoma. Tembo kuna ZOO Arusha wanafunga na kucheza nao kuna Mhindi mmoja anafuga Tembo. Sijaona Nyati.
Nyaji sio kivutio mzee unamfananishaje mnyama Kama Tembo na nyati kwenye utalii...wewe ukiambiwa balabalani anaoitishwa Tembo na uambiwe anapitishwa nyati wapi moyo wako utapasuka kjwa na shauku ya kwenda kjmuona

Nyati ni ng'ombe tu analiwa na Simba daily
 
Kati yamnyama anaeongoza kupeleka matanga kwenye koo zasimba bhas nihuyu mwehu hua wanakufa sana kwenye harakat zakuwawinda hasa ukute mbogo alokomaa halafu kavurugwa
 
Nyati ( mbogo) , Huyu wenyewe maofisa wanyama pori wanamuita FIELD FORCE, wanyama wengine wote , wakichachamaa na kuvamia maeneo ya WANANCHI kuwaswaga kuwarudisha porini ni rahisi tu.

Lkn miamba hii NYATI (MBOGO) msamiati wa kurudi nyuma wao HAWANA. ni mapambano kwenda mbele, jamaa alinisimulia kuwa waliwakamata MAJANGILI wakiwa wametega mtego na tayari NYATI kanasa!!.

Wale maofisa wa wanyamapori wakawapa MAJANGILI sharti la kuwaachia ni wao MAJANGILI waende wakautegue ule mtego ili NYATI anasuke.

MAJANGILI wakagoma katakata wakasema sharti hilo ni bora tu , wawapeleke kwenye mkono wa sheria. Lkn kwenda kumnasua NYATI akiwa HAI hawawezi kuthubutu.
tena ni heri ukutane na kundi la nyati wengi porini, lakini usiombe ukutane na nyati akiwa peke yake... na pia anatabia ya kuvamia kwa kushtukiza
 
Mkisema nyati hafugiki ni jeuri, mbona simba na ubabe wake anafugwa na maliasili huwa tunamuona pale kwenye maaonyesho ya sabasaba dar? Vipi kuhusu chui naye anafugika?
Simba si hatari sana, huyu unaweza kutana nae porini na asikufanye kitu
Chui ni hatari kuliko kawaida, akili yake huwa inawaza kuua tu na si vinginevyo, yaani kwanza lazima akuue mambo mengine yafuate... unaweza bahatika ukapambana nae akakujeruhi.. lakini ni m'baya sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom