Kwanini Elizabeth Michael "Lulu" ameamua Kuuza Nguo, Viatu Vyake?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Elizabeth-Michael-Lulu-1024x626.jpg




WAKATI Siku ya Wapendanao — February 14 mwaka huu — inakaribia, staa wa filamu, Elizabeth Michael Lulu, amekuja na jambo jipya; anauza nguo zake na viatu ambapo pesa atakayoipata itakwenda kusaidia wenye uhitaji katika jamii.



Lulu amethibitisha hayo katika akaunti yake ya Instagram ambapo amekuja na kitu hicho alichokipa jina la “Save My Valentine”.



Lulu.jpg




“Wakati Wengine Tumepata Fursa Ya Kuwa Na Furaha Kwa Vile Tulivyonavyo Kuna Baadhi Ya Wenzetu Wamekosa Nafasi Hiyo….. Na HUU NI MPANGO WA MUNGU, Kuelekea Siku Ya Wapendanao Februari 14,Nimeamua Kuuza Sehemu Ya Nguo Zangu Ambazo Yawezekana Umeshawahi Kuziona au Haujaziona.
Na Pesa Yote Itakayopatikana Kupitia Mauzo Haya Itaenda Kusaidia Vitu/Watu Wenye Uhitaji Katika Jamii.
Please Join me to Save My Valentine.
#Savemyvalentine”Ameandika Lulu



Post mbili za stori alizoweka kwenye mtandao wake wa instagram:



1-25-1024x448.jpg
2-17-1024x502.jpg
 
Huyo anauza nguo zake za zamani
Wanawake wa hivi huwa wanabadiri kila aina ya mitindo ya nguo,viatu na mikoba hufika sehemu makabati yote ndani yamejaa wakati bado kuna mitindo mipya inakuja hivyo wengine huwa wanachukua nguo zote za zamani na kuwagawia ndugu zao mikoani sasa yeye kaona bora auze kwa style hiyo ili apate chochote wala sio kwamba atawauzieni nguo mpya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chezeya vyuma na michango ya harusi doro imebidi tusingizie tutatoa misaada
 
Back
Top Bottom