mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,503
- 252
Katika habari yenye kichwa ''' CHADEMA YAASWA'' iliyotoka katika gazeti la habari leo. Dr Bana ameonekana kuishangaa CDM kwa maamuzi iliyofikia. Kwanza ameusifu waraka huo kwamba eti ni mzuri sana na unaonyesha demokrasia. Pili anadai eti kitendo cha wanachama kuaandaa waraka huo ni cha kawaida hata katika vyama vingi. Ajabu ni kuwa anatolea mfano wa baba wa taaifa alipoandika kitabu cha '' hatima ya nchi yetu''' hii ni ajabu sana!!! hivi kweli waraka huu wa kina kitila unaweza ufananisha na kitabu cha mwali chenye ujumbe wa hatima ya nchi yetu??? kweli Napata mashaka na ma dokta wa namna hii. Pia katika maoni yake Dr, Bana amedai CDM kimekuwa kikilaumiwa kwa ukabila na ubinafsi na ukanda kwa sababu hizo anaunga mkono waraka. Nina mashaka sana na huyu DR. kwa nini azungumze sana wakati huu? Na kwa nini aipone chadema? Mbona katika chama chake kuna migogoro mikubwa na makundi yanayohasimiana lakini hatumsikii akitoa maoni ya ama kuponda kundi moja au jingine? Wadau nisaidieni katika hili je DR Ni kweli anaipenda Chadema hata aseme hayo au nini kipo hapa?