CHADEMA wa Mtandaoni watamwelewa lini Dr. Lwaitama?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,876
CHADEMA kama ilivyo Kwa vyama vingine imesheheni wajumbe hadi wa mitandaoni.

Ukweli mchungu Kuna Hawa wenzetu wa mitandaoni wenye kukaza bongo almaarufu kubadili bongo na kupania maembe:

Screenshot_20230806-232254.jpg

Kulikoni ndugu zetu ya Dr. Lwaitama kutambua umoja ni nguvu utengamano ni udhaifu yana kutokuwa yana maana yoyote kwenu?

Kwamba madini hayapo CDM tu bali kote kwenye vyama mbadala vilivyombebea bango kibaka wetu? Tatizo liko wapi?

Tusitoke kwenye reli kupopoana mawe sisi kwa sisi tukimwacha kibaka wetu kutokomea kusikojulikana:

Heshima kwake sana Dr. Azaveli Lwaitama.

======
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Dk Azaveli Lwaitama, amepanda katika jukwaa la ACT- Wazalendo na kuhutubia akisema anawapenda Zitto Kabwe na Juma Duni Haji kwa sababu wana madini.

Dk Lwaitama ambaye ni mwanazuoni amepanda katika jukwaa hilo leo Jumamosi Juni 3, 2023 wakati viongozi hao hao wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Plattform wilayani Bukoba mkoani hapa.

Msomi huyo aliyevalia kofia rangi ya nyekundu sambamba na fulani yenye rangi hiyo iliyoandikwa ' Katiba Mpya' amesema Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo na Duni Mwenyekiti wa chama hicho; ni jamaa zake.

"Nikiambiwa Zitto na Duni wanakwenda kuhutubia nakwenda kuwasikiliza hawa jamaa ni wenzangu hawa jamaa ni madini matupu nyie vijana wa mjini madini matupu," amesema Dk Lwaitama ambaye aliwahi kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwanazuoni huyo, ambaye pia amewahi kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine amesema Duni ni miongoni mwa watu waliomfundisha kuhusu mamlaka kamili ya Zanzibar.

Katika ujumbe wake, Dk Lwaitama amesema sio sahihi kwa vyama vya siasa vyenye lengo moja kurushiana vijembe wenyewe kwa wenyewe badala yake waunganishe nguvu na kupambana na adui yao.

"Watu wanabishana halafu wana lengo moja lakini tofauti ni sera, msiruhusu kuchochewa na kutumia nguvu nyingi dhidi ya mabishano yenu, balala yake elekezeni nguvu zenu kwa yule anayewachochea," amesema Dk Lwaitama.

Kwa upande wake, Zitto amemshukuru Dk Lwaitama kuhudhuria mkutano wake, akisema msomi huyo ni mzee wake tangu wakiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Dk Lwaitama yeye ni mtaalamu wa lugha lakini mimi nilikuwa nasoma uchumi, lakini nilikuwa nashinda ofisini kwake hadi watu wananishangaza,” amesema Zitto na kuongeza;

"Nakushukuru sana kwa kuungana nasi leo naunga mkono hoja yako kwamba hakuna sababu ya msingi pale ambapo vyama mnapiginia jambo moja mnaanza kurushiana mawe, badala ya kumrushia yule mnayepigana naye.”

Zitto ameongeza kuwa, hakuna sababu ya kutukana na kupigana badala yake wanasiasa wanapashwa kubadilisha taarifa za kufikia malengo yao, na kwamba ni kwa bahati mbaya wanasiasa wa Tanzania hawajafikia hatua hiyo.

“Inawezekana watu mkawa na lengo moja mkapita njia tofauti na sio vizuri kudhani njia ya mtu mmoja ndio sahihi," amesema.

Zitto amesema hivi sasa mjadala mkubwa ni Katiba Mpya na bahati nzuri katika jambo hilo hawatofautiani, isipokuwa namna ya kuuendea mchakato huo ili kuhakikisha mchakato unafanikiwa.
 
Kutoka June hadi sasa angalia matukio ya Zitto au ACT WAZALENDO , halafu toa maoni yako

Si kutokea Jun tu hadi leo. Zingatia clip hii ya Dr. Lwaitama. CDM wa mitandaoni waliokaza bongo zao ni mzigo kwa chama:

Kwa ujumla wanarudisha nyuma jitihada za ukombozi.

Lini watambue Umoja ni nguvu ndugu hao?
 
Wenye busara wana dhihaka hii..."never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable"!!!!

Hata kukosoa kuna adabu zake....

Wengi wetu vijana tumekuwa msambweni katika hili.....

Ni kama hatujui tunapigania nini katika "mvurugiko" wa dunia ya sasa na changamoto zake.....

Safari ni ndefu sana na tunaweza KUIPUNGUZA ikiwa tutataka na kubadilika......

#SiempreJMT
 
Si kutokea Jun tu hadi leo. Zingatia clip hii ya Dr. Lwaitama. CDM wa mitandaoni waliokaza bongo zao ni mzigo chama:

View attachment 2710472

Kwa ujumla wanarudisha nyuma jitihada za ukombozi.

Lini watambue Umoja ni nguvu ndugu hao?

"...yaani Lowassa mlikubali ila prof.Kitila Mkumbo hamumkubali"

Amenikumbusha "kubadili gia angani"....hatari sanaaaa
 
"...yaani Lowassa mlikubali ila prof.Kitila Mkumbo hamumkubali"

Amenikumbusha "kubadili gia angani"....hatari sanaaaa

Kubadili gia angani au ardhini kote ni sawa. Kubadili msimamo kutegemeana na mazingira na nyakati huo ndiyo uungwana.

Maana halisi ya kutokuwa na adui au rafiki wa kudumu bali agenda!
 
Wenye busara wana dhihaka hii..."never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable"!!!!

Hata kukosoa kuna adabu zake....

Wengi wetu vijana tumekuwa msambweni katika hili.....

Ni kama hatujui tunapigania nini katika "mvurugiko" wa dunia ya sasa na changamoto zake.....

Safari ni ndefu sana na tunaweza KUIPUNGUZA ikiwa tutataka na kubadilika......

#SiempreJMT

Si kutojua tunapigania nini tu. Bali hata tunasimamia Nini? Wapo huko uvccm pia. Hivi inajulikana wanasimamia Nini?
 
Kubadili gia angani au ardhini kote ni sawa. Kubadili msimamo kutegemeana na mazingira na nyakati huo ndiyo uungwana.

Maana halisi ya kutokuwa na adui au rafiki wa kudumu bali agenda!
Sawa....

Sisi "agenda" yetu ni kudumu kwa JMT yenye serikali mbili.....
 
Si kutojua tunapigania nini tu. Bali hara tunasimamia Nini? Wapo huko uvccm pia. Hivi inanulikana wanasimamia Nini?
Well ...

Huku UVCCM liko moja wanapatia sana....

Kusimamia KUDUMU kwa JMT yenye serikali mbili....

Hili huwa ninalala na kuamka nalo....yaani niko "obsessed" nalo kwa kweli.....
 
Siku zote kuna kukubaliana na kutofautiana, sio rahisi mtu kumkubali mwingine kwenye kila jambo.

Mfano. Dr. Lwaitama ameonekana kumkubali Zitto kwenye madini, lakini kama angeulizwa kwenye mambo mengine ikiwemo misimamo ya kisiasa kama anamkubali Zitto angeweza kujibu tofauti.

Zitto ni kigeugeu asiyeaminika. Hata hilo la Katiba Mpya unaweza kuungana na ukiamini mko pamoja, lakini ghafla mwenzenu akawaacha njia panda muda msiotarajia.

Kumuamini mwanasiasa anayeongozwa kwa kutazama sura ya aliyepo ikulu, badala ya kutazama interest za taifa kwanza ni ngumu sana, kufanya hivyo lazima ujigeuze mnafiki wa hali ya juu.

Wacha Katiba Mpya itafutwe na wenye nia ya dhati, wale wenye misimamo isiyoyumba, hao wengine wakiona umuhimu wa kujiunga na wenzao wanakaribishwa, lakini isitokee kupoteza muda kutafuta uungwaji mkomo wa mtu asiyeeleweka, huko ni sawa na kuzidi kujichelewesha?
 
Hayupo anayesema jitihada zozote kuwekwa kwenye kutafutwa uungwaji mkono na vyama vingine. Chama kisichojua watanzania wanataka nini hadi leo hakitufai.

Kinachosemwa panapo hoja mfanano, twende pamoja. Ila hii ya kupigana mihuri kuwa fulani msaliti au kigeugeu tumwachie Mungu.

Ikumbukwe kukubali kutofautiana ndiyo uungwana.

Ila hii ya kurushiana mawe na kuitana majina, hiyo siyo kabisa. Kwa hakika hiyo iko kwa manufaa ya CCM zaidi.

Tuzingatie:

1. Nini msimamo wa mtu au chama? Anapinga maonevu ya CCM au la?
2. Nini lengo? Tunataka Katiba mpya? Tunataka utawala mbadala?
3. Tunataka haki zipi?
4. Tuko tayari kwa Mapambano?
5. Nk.

Kwa kawaida mwanzo huwa ni kujikita kwenye vya msingi na kuona tofauti ziko wapi na kama zina himilika.

Zingatia madini anayoongelea Lwaitama kumhusu zitto si ya ardhini.

Madini = Hoja, kwa mujibu wa Lwaitama.

Hili ndilo CDM wa mitandaoni wasiloliona.

Cc: Zawadini
 
Sawa....

Sisi "agenda" yetu ni kudumu kwa JMT yenye serikali mbili.....

JMT yenye serikali mbili siyo msahafu toka Kwa Mola. Haya ya agenda yenu bila kutushawushi kwa hoja ndiko kukaza bongo na kupania maembe mahali pa bongo vichwani.

Kulikoni kutowashawishi watu Kwa hoja Ili wanaotaka serikali Moja au tatu wakaona mbili ni Bora?

Kulikoni kutaka watu wote kutaka kuburuzwa TU kwamba agenda yenu ni hiyo you basi?!

Kwamba mnasimamia serikali mbili bila sababu huoni haijulikani mnasimamia nini na mko kama mazuzu tu?
 
Well ...

Huku UVCCM liko moja wanapatia sana....

Kusimamia KUDUMU kwa JMT yenye serikali mbili....

Hili huwa ninalala na kuamka nalo....yaani niko "obsessed" nalo kwa kweli.....

Unaweza kuwa obsessed na suala la kijinga. Kwamba uko obsessed na suala la kijinga wewe peke yako au na wenzio kulikoni kudhani na wengine tudiokuwamo kuwa obsessed?

Ustaarabu ni kumshawishiana kwa hoja.

Wewe uko obsessed na JMT serikali 2. Wengine obsessed na JMT serikali 1, 3 au 0.

Kwani wakufuate wewe na wewe usiwafuate wao? Hapo ni hoja Sasa. Zaidi ya hapo kura. Wengi wape!

Nchi ni yetu sote. Hakuna mwenye haki zaidi.

Tudilazimishane. Wengi wape. Ndiyo ulio ustaarabu.
 
Hayupo anayesema jitihada zozote kuwekwa kwenye kutafutwa uungwaji mkono na vyama vingine. Chama kisichojua watanzania wanataka nini hadi leo hakitufai.

Kinachosemwa panapo hoja mfanano, twende pamoja. Ila hii ya kupigana mihuri kuwa fulani msaliti au kigeugeu tumwachie Mungu.

Ikumbukwe kukubali kutofautiana ndiyo uungwana.

Ila hii ya kurushiana mawe na kuitana majina siyo kabisa. Iko kwa manufaa ya CCM zaidi.

Tuzingatie:

1. Nini msimamo wa mtu au chana? Anapinga maonevu ya CCM au la?
2. Nini lengo? Tunataka Katiba mpya? Tunataka utawala mbadala?
3. Tunataka haki zipo?
4. Tuko tayari kwa Mapambano?
5. Nk.

Kwa kawaida mwanzo huwa ni kujikita kwenye vya msingi na kuona tofauti ziko wapi na kama zina himilika.

Zingatia madini anayoongelea Lwaitama kumhusu zitto si ya ardhini.

Madini = Hoja, kwa mujibu wa Lwaitama.

Hili ndili CDM wa mitandaoni wasiloliona.

Cc: Zawadini
Hayupo asiyependa hoja, wote tunapenda kusikiliza na kuchangia hoja, akiwemo Dr. Lwaitama, pamoja na mimi nawe.

Lakini wakati ambao bado unaikumbuka hoja ya mwenzio ya jana, ghafla leo unaona anageuka, anaanza kuzungumza vitu tofauti na jana, hapo lazima uwe makini..

Mfano, ACT msimamo wao ulikuwa Tume Huru kwanza, sijui ni lini walibadilika kwa pamoja wakaanza kusema Katiba Mpya kwanza, sasa unapoamua kumfuata mtu wa aina hii, umakini unahitajika, anaweza kukuacha solemba muda usiotarajia..
 
Back
Top Bottom