Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,263
- 17,139
Hujui kitu. Kuzindua mradi hadi mwenge? Ina maana mwenge ukizimwa huwa hakuna miradi? Hivi wajua mwenge ukiwashwa hadi kuzimwa unatumia sh. ngapi ukimbizwa mikoa yote au ni wachache kupata posho.?
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.
Hivi nani huwa anakagua mapato na matumizi ya shughuli za mwenge? Ni huyu huyu CAG tuliyenaye au masuala ya Mwenge ni off limit kwake?
mkuu Ofisi yetu haina mipaka ya kukagua,lakini kwny ili eneo huwa tunakagua level ya local gvt,we do very partial.ni wakati wa cag kufanya special audit ya mwenge.huu ni mgodi wa ccm.btw miradi ya mwenge huweka vizuri sna kwa hofu ya kuumbuka.ikikosekana tunazindua gest
Hujajibu swali kwa nini chadema wanaupinga mwenge wa uhuru hata sababu wanazotoa hazina maana.
Mkuu umepinga nini na umekubari nini,sioni kama kuna gharama zozote za kuendesha mwenge ukilinganisha na faida zinazopatikana.
Bongo lala mwenge unaleta maendeleo gani?
chadema kama waliweza kumsapoti kagame watashindwa kupinga mwenge wa maendeleo na uhuru ambao umekuwa ni chachu ya maendeleo katika maeneo mengi.
Mwenge ni mzigo kwa Taifa. Gharama ya kukumbiza mwenge ni kubwa sana kama itakavyokuwa kwa serikali 3!
haya ni madhara ya viroba na bangi eti nawe unakichwa au umebeba nazi tu.
Jibu limejibiwa na Kabila01 japo hutaki kusikia na kasema hivi "Mie sio mwanachama wa chama chochote lakini napinga sana suala la mbio za mwenge. Wananchi wanajichanga wanajenga kadarasa kamoja, harafu unakuja kuzindua mwenge ambao ndani yake watu wamejilipa posho za 80,000 per day times 50 people. Bado wametumia magari waliyojaza mafuta pamoja na gharama za uchakavu. tunatumia milion 10 kwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa choo cha shule? Kwa kweli tubadilike"
Na mimi naongezea, mbali na kuzindua mradi labda wa Zahanati iliyojengwa kwa michango ya wananchi na si serikali lakini mwenge unakuja unachangisha hao watu tena ili wazidue mradi wao, tuseme kwa uchache kila mtu kachanga 500, mfanya biashara 5000 zimepatikana katika kijiji hicho laki tano. Kwa hiyo wamekaribisha mwenge kuzindua zahanati yao kwa gharama za sh. 500000, sasa hao watu wazinduzi au wakimbiza mwenge nao wamelipwa posho ya kila siku 80000 watu 50 yaani (80000x50)+500000(michango ya kijiji)=4,5000,000, je wangemuita mkuu wa wilaya au mganga mkuu wa wilaya angekula hiyo milioni nne na nusu kwa siku moja? Sasa piga hesabu kuukimbiza nchi nzima ni mabilioni mangapi yameteketea. Ndio Chadema wanapinga ufisadi huo.
Nyongeza nyingine mwenge ni source ya ufusika na usambazaji wa ukimwi. Ukiangalia pale mwenge umelala yanayofanyika hapo Mungu tuhurumie, ni ulevi na kusambaza ukimwi tu.
Ningeendelea kukupa hasara za mwenge ila naona uchungu acha tu niishie hapo
Ni upotezaji wa muda na nguvu kazi maana badala ya watu kufanya kazi wako wanakimbiza mwenge tu
chadema kama waliweza kumsapoti kagame watashindwa kupinga mwenge wa maendeleo na uhuru ambao umekuwa ni chachu ya maendeleo katika maeneo mengi.
Nyie maccm vichwa vimejaa maji mnafikiri kwa kutumia matumbo, Mwenge unamsaidia nini mwananchi watoto wake wanaketi sakafuni darasa la vumbi?
Maneno mengi lakini ya maana ni mawili tu,
kunahaja ya chadema kuacha kuropoka kwa kupinga kila kitu badala yake ijikite kuendeleza jamii zaidi kuliko kupinga.
njaaa hizi zinawafanya watu kujitoa ufahamu
Baada ya kusoma comments zako nyingi nimegundua yafuatayo.
Hayto ni kwa uchache tu mengine nitarudi kuongezea ukipenda.
- Wewe unahusika moja kwa moja na kunufaika na hizi Mbio za mwenge ndio maana hukubaliani na hoja za msingi za wachangiaji wengine wanaopinga
- Umetumwa au kwa maksudi unatetea hizi mbio za mwenge ili uendelee kunufaika pasipokujali kama kuna gharama nyingi zinapotea ukilinganisha na Miradi inayozinduliwa.
- Menge umepoteza maana yake halisi na hivyo ungekuwa sehemu ya utalii kwani hauleti TUMAINI, AMANI, HAUANGAZI NJE YA MIPAKA WALA KULETA HESHIMA tena badala yake unatumiwa tofauti na maazimio yake.
wanaotumia tumbo ni warafi kama wewe ulivyo mrafi unawaza tumbo tu.