Kwanini CHADEMA hawaandamani Moshi?

Kwanini CHADEMA hawaandamani Moshi?

Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Maendeleo yaliyoko moshi nimakubwa sana. Wamachinga wamejengewa mazingira mazuri.Mji umepangika vizuri lami kila mahali maji yapo. Mbunge tuliyenaye yuko imara. Tumesahau mdudu anayeitwa CCM kwa miaka mingi sasa iweje tuandamane.
 
moshi hawataki vurugu za maandamano! wanajua fika kabisa vurugu za maandamano zitaharibu biashara ya utalii ambayo vijana wengi ndo wanakoptata riziki zao, pia wao bize sana na biashara zao mbalimbali!

Wazo moja umeliremba bila sababu! Kutokuandamana kwa CHADEMA Moshi ni kwa sababu katika halmashauri nyingi zinazoongozwa na CHADEMA hakuna upuuzi upuuzi! Hata hivyo, mleta mada halengi kujua sababu kama uliyoitoa!Mleta mada anajiandaa KUKENUA akiona MJINGA yeyote amepost kwamba ni kwa sababu CHADEMA NI CHAMA CHA WACHAGA!
 
ahaa SIWEZI KUCHANGIA KWA SABABU THIS IS RE-POST.
 
Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema Moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema Moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Acha fikra mgando! Ulishawahi kusikia Kigoma, Sumbawanga, Dodoma, Singida , Tabora, Shinyanga, Ruvuma, na kadhalika wakiandamana? Hupangwa tu na kuamua sehemu ya kuandamana na kwa sababu maalum. Maandamano yaliyozuiwa yaliokuwa ya nchi nzima
 
Hai cdm
Rombo cdm
moshi mjini cdm
vunjo tlp.. Sasa si bado kidogo tuyamalize yote..
 
Moshi kwa wachaga bado majimbo ma wili 2 yani moshi vijijini linaloongozwa na crilli chami na na siha linaloongozwa na Agrey Mwanri.. Alafu tunahamia same ambapo bado ccm inawadanganya wapare..
 
Mosh wajanja wewe, waumizwe?
Mchaga mjanja sana, anawaandamishaje waarusha huko kwao?, wafe hana la kupoteza

we sema ccm hawakutumia nguvu kama arusha kulitaka lile jimbo ndo maana hakuna chokochoko
 
Mnama,

Kule Kibosho na Mwanga, nani anaongoza?

kama jambo hulijui vizuri uliza alafu muwe mnasoma kuanzia mwanzo sababu haya yalimalizika tangu jana. Kinachoongelewa hapa ni moshi manispaa{mjini} unapotaja mwanga ni wilaya nyingine kabisa na kibosho ni moshi (v) sasa unanipa wasiwasi wa kuamini kama unajua uacho post.
 
Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema Moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema Moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Hawataki kuharibu kwao wanalenga Miji mingine itakayoonekana Ina ulimbukweni ili Miji hiyo iharibike Na moshi izidi kusonga mbele ili liwe Jiji kubwa kuliko Miji yote tanzania
 
Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema Moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema Moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Wanataka Miji mingine wakalie maandamano na kusahau mambo ya Maendeleo wakati moshi kuko shwali ili Mji wao uzidi kukua Na baadaye uwe Mji Mkubwa kuliko Miji yote Tanzania
 
Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema Moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema Moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Hivi kweli unaifahamu Moshi ama unaisikia, Wakazi wa Moshi huwa wanafanyaga kitu kinachoitwa "COLD REVOLUTION". Historia inaonyrsha toka kuanzishwa kwa vyama vingi Jimbo la Moshi mjini halijawahi kuchukuliwa na wala halitowahi kuchukuliwa na CCM. Mosi wakaazi wa Mishi hawana muda wa kunuliwa kama njugu, una hele zako njoo nazo watazila kisha kwenye boksi lakura ndio usieme. Mwaka 1995 alikuja hayati baba wa TAIFA katika kampeni akimnadi Benjamini Wiliam Mkapa kwenye urais pamoja na mgombea wa ccm wakati huo jina kidogo limenitoka, kwa mara ya kwanza katika siasa Nyerere alionja challange ambayo hakuisahau mpaka alipoingia kaburini. Aliambiwa hapa Moshi CCM ni kofia ya Polisi haiuziki. Alikasirika sana ilikuwa ni uwanja wa mashujaa na alindoka kwa hasira kabla hata mkutani kumalizika. Kipindi hicho Lyatonga Mrema ndio anawika na NCCR-Mageuzi.
Wakazi wa Moshi hawana muda wa kupoteza muda walionao ni wakutafuta hela tu. Njoo na convoy yako ya magari ya kifahari na pesa zako kama wewe ni mdabwana hawana time na wewe.

Kwa Moshi wanaotakiwa kuandamana ni ccm na wala sio CHADEMA ukizingatia wao ndio wanashikilia Manispaa.Pili Moshi barabara za lami Mpaka vijijini, nyumba za kisasa (Block) mpaka vijijini, umeme mpaka vijijini, yaani kwa kifupi mahali kama Bukoba vijijini au Mtwara vjijini ukilinganisha na Moshi vijijini ni sawa na kulinganisha DUBAI na TANZANIA.
Sasa waandamane kwa lipi? Sijui kijijini ulikotoka wewe kukoje?
 
Moshi ni waelewa walishakubali chama mathubuti. Waliisha kombolewa kutoka magamba sasa ni sera bora zinaendelea moshi ndo maana hakuna cha kuandamana
 
Wakuu na maGT naomba mnisaidie, mbona sijawahi kusikia CHADEMA wakiandamana moshi au ndo kusema Moshi hapana matatizo kama ambayo huwasababisha wao kuandamana sehemu nyingine? Au ndo kusema Moshi hapana tatizo na wakishika dola nchi itakuwa kama Moshi?

Popo ana macho mangapi?
 
Mosh wajanja wewe, waumizwe?
Mchaga mjanja sana, anawaandamishaje waarusha huko kwao?, wafe hana la kupoteza

Kwa hiyo watu woote wanaoishi Arusha ni Waarusha tu sio? Na Dar Es Salaam wanaishi wazaramo peke yao sio? Sasa ninyi endeleeni tu na mawazo kama haya mkidhani kuwa taifa litabaki salama.
 
Back
Top Bottom