.CHADEMA kujitolea ni kosa kubwa.lakini sisi wa ccm tunajitolea kwani wenyeviti wa kata na matawi wa ccm wanalipwa wanajitolea kama mbowe anavyojitolea.wangwe si mwanasiasa ni mbishi nashangaa kwanini chadema walmempa madaraka yote haya.mwanzoni alikuwa akiitwa rasta.naamini hata kupata ubunge somply CCM waling'ang'ania chambili lakini wamgemuweka mtu mwingine wangwe asingeambua kitu.tarime ni wana ccmKuelekea ukombozi ni lazima wachache ama wengi wawe tayari kuumizwa kwa faida ya wengi.
Hii ni vita ya kuelekea ukombozi ,na ijulikane kuwa wafanayabiashara na wenye pesa hawakichangii CHADEMA kwani wanaogopa CCM.
vitu vingine tuwe tayari kusema ukweli mbona hata hapa JF inaendeshwa kwa kuchangiwa na wanachama wake wenye uwezo wa kuchangia?
Mbona hapa hamlalamiki kuwa waache kuchangia?
Nani anamlipa Invisible na JF Crew yote hapa ?mbona wao wanajitolea na kufanya bure?
Ama kujitolea CHADEMA ndio dhambi na kosa?
2008-07-02 09:46:16
My Take:
- Kwanini Chadema isiwalipe viongozi wake? Hicho chama siyo taasisi ya dini au NGO, huu mtindo wa kulipa fedha za wao wenyewe na wengine kutolipwa ni mtindo mbaya. Hata mtindo wa Mbowe kutoa fedha yake mfukoni kwa ajili ya Chadema siyo mtindo mzuri kwani unamfanya aonekane kama ana maslahi zaidi ya mtu mwingine. Chama kiendeshwe kama Chama. Hata kama chama hakiwezi kuwalipa inavyopaswa ni muhimu kuwa na token payment hata kama Shs. 10,000 kwa mwezi kwa viongozi lazima walipwe, wasifanye kazi za chama bure.
- Kama Bajeti ya Chama ni ndogo kuliko mahitaji yake, ni lazima wajifunze kufanya mambo ndani ya bajeti. Kama ni kuanzisha miradi n.k wafanye hivyo lakini wasifanye vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvigharimia. Katika hili wanaweza kuanzisha miradi ya Chama. Hili linawezekana kwa kuanzisha kampuni ya Chama (Holding Company) na wanaweza kuangalia ni jinsi gani chama kinaweza kumiliki kitega uchumi. Kama mnapata karibu milioni 66 kila mwezi na fedha zote zinaishia kwenye matumizi na hazizalishi basi kuna tatizo la kiuwekezaji.
- Uongozi mkuu wa chama ujitoe kwenye kusimamia fedha na badala yake waajiri watu ambao wana weledi wa mambo ya fedha. Mhasibu Mkuu, Mkaguzi wa ndani, watunza fedha n.k na wataalamu wa Boharia. Wanasiasa wabakie kufanya maamuzi ya kisiasa. Na watumishi hawa walipwe kwa kiwango cha fani zao, na wasiwe na uhusiano wowote ule wa karibu na kiongozi yeyote wa juu wa chama hicho. Kabila, mkoa, rangi, au dini na jinsia don't count.
- Ruzuku ya Chama isipokelewe na kiongozi wa kisiasa, period. Fedha za ruzuku au fedha nyingine yoyote inaenda moja kwa moja kwenye akaunti ya chama na hesabu zake zinaeleweka na zinasimamiwa ipasavyo. Lazima waweke mfumo mzuri wa usimamizi wa fedha ili saa ya yoyote ijulikane wana fedha kiasi gani, ziko wapi, na zimetumika vipi.
- Viongozi wa kisiasa warudi kwenye kuimarisha chama, kwa kupika makada wa kisiasa, kufungua matawi ya chama n.k. Sikumbuki mara ya mwisho kusikia Zitto, Slaa, au Mbowe amefungua tawi la Chadema mahali popote ilikuwa lini. Chama hakijengwi kwa hotuba za Bungeni, au maneno ya magazetini, bali kwa kushawishi watu kukikubali na kuzielewa sera zake. Na njia pekee ya kuonesha kuwa watu wanawakubali ni watu kujiunga na chama hicho.
Madai kuwa watu wanaelewa kuwa Chadema inapigia kelele ufisadi zaidi n.k ni madai tu lakini ushahidi wa watu kuelewa unaonekana kwa watu kujiunga. Je tangia mambo ya ufisadi yaanze na tangia sakata la Zitto Chadema imejipatia wanachama wangapi, na kiasi cha watu kujiunga kina tofauti gani na kabla ya hapo. Kama hakuna tofauti kubwa na inayoonekana basi kuna tatizo mahali fulani.
Mengine.. nitawaandikia in private katika kulinda "heshima ya chama" chenu.
unachoshindwa kujua ni kwamba JF sio chama cha siasa chenye malengo ya kuongoza nchi siku moja kama chadema, Hii ni forums ambayo watu wachache wamejitolea kwa moyo mmoja na hata wewe hujakatazwa kufanya hivyo, lakini Chadema ni chama cha siasa na kina katiba na dhumini la kuongoza nchi yetu kama ikibahatika,we unategeme siku Mbowe akisema anataka kulipwa pesa zake zote alizo jitolea wakati wako IKulu si watauza nchi yetu , kuwa makini ndugu yangu
Mkuu Slaa.
Sote tunatambua sana mchango wako wakupigana na mafisadi nchini.
Lakini tunasikitika sana kuona unatumia mtandao wa simu wa FISADI aliye kubuhu Rostam Aziz na hapa imewahi tolewa thread watu kususia huduma zote za mafisadi kama huyu.
Kwa hiyo mkuu kuendelea kutumia line ya simu ya VODA maanake unamuunga mkono RA anaye tuibia nchi yetu kwa kuwekeza kwenye hii kampuni ya VODA.
Tunaomba ubadilishe hii line ya VODA tupo tayari kukuchangia ununue TIGO au ZANTEL.
Ahsanteni.
MMK
Nakushukuru sana kwa ushauri kuhusu uendeshaji wa fedha kwenye vyama vya siasa. Hata hivyo, Chadema ni chama kinachofanya kazi yake kwa uwazi. Hatuna la kuficha napenda kueleza ifuatavyo:
i) Uamuzi wa viongozi wakuu, tena wanaotumia muda wao wote kwa shughuli za chama, za kisiasa na uendeshaji, ni uamuzi uliofanyika kwa hiari na kupitia vikao halali vya chama. Kwa bahati mbaya maamuzi mengine hayafiki hadharani. Chadema haioni cha ajabu katika hatua hii. Mwalimu Nyerere asingejitolea enzi za uhuru, na kuchangiwa na wapenzi wachache waliokuwa na uwezo leo tusingelikuwa na Uhuru. Nadhani wenye mapenzi mema na nchi hii wataelewa kuwa mapambano tuliyonayo ni mapambano yanayohitaji kujitolea kwa kiwango kikubwa. Viongozi wakuu wa Chadema kwa kutambua hili, waliamua kwa hiari yao, kujitolea ili ruzuku kidogo iliyoko itumike kwa shughuli za uenezi. Bendera, Kadi, nyaraka mbalimbali,ujenzi wa Ofisi stahiki Makao Makuu ya Chama kama sura ya Chama, kuwekeza kwenye miradi ya muda mrefu ya kuitegemeza chama( kazi hiyo imekwisha kufanyika siyo nadharia na kwa yeyote mwenye nia ya kutaka kujua tunaweza kumpa taarifa za kina), ziara za uenezi na kadhalika.
2) Viongozi wa juu wa Chadema ni Wabunge, ukimwacha Mwenyekiti. Mishahara wanayopata ikitumika kuendeleza Chama kuna dhara gani, Chama hujengwa na wenye moyo. Hili halina maana ya wenye kuchangia chama ndio waamuzi katika maamuzi ya chama. Chama kinaendeshwa kwa Katiba, Kanuni, Maadili, na Itifaki ya Chama. Maamuzi yanapofanywa kwa imla hofu hizo hutokea. Kwa Chadema, ambayo maamuzi yake hufanyika yote na vikao halali, mipango huenda kwa kadiri ya Strategic Plan, ambayo nayo si siri, ipo wazi kwenye Mtandao wa Chama, na kila mwenye nia njema anaweza kuipata bila tatizo. iwapo kuna mwenye kuhitaji maelezo ya ziada tuko tayari kuyatoa wakati wowote, vitabu vya Hesabu ya Chama ni mali ya Wanachama na wakati wowote Mwanachama anaweza kuomba taarifa atapewa, na au anaweza kufika Makao Makuu ya Chama akaona vitabu hivyo bila gharama yeyote. Taarifa zote za fedha hutolewa kwenye vikao vya Kamati Kuu, na sijawahi kuona Taarifa ya Fedha ikikataliwa kwa ubadhirifu au kwa sababu yeyote ile. Wajumbe wa Kamati Kuu ni mashahidi. Taarifa ya Fedha hutolewa pia kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuendana na Ratiba ya Kikatiba ya Vikao hivyo.
3: Fedha za Chadema hukaguliwa na Wakaguzi wanaotambulika kisheria, na huwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.
4: Ili kuepuka Wachache wenye uwezo kufanya chama kuwa mali yao, Chadema inaoutaratibu ambao sina hakika vyama vingapi unao, wa kutathmini na kutambu mchango wa kila mwanachama kwa maana ya fedha zake anazochangia kwenye chama, muda wake anaotumia kwa ajili ya shughuli za Chama ( hatua hii inafanyika kwa sasa Makao Makuu tu kwa vile Instruments za kufanya Tathmini hii kwenye mikoa na Wilaya bado inafanyiwa kazi na hata ya Makao Makuu bado inaendelea kufanyiwa kazi. Mathalan muda wa mtumishi wa Chama anayefanya kazi baada ya saa rasmi za kazi hutathminiwa na kupewa thamani ya fedha kama mchango wake kwa ujenzi wa chama. Inahitajiwa fikra mpya ili ukombozi tunaoendelea nao uweze kufanikiwa. Lakini kutegemea fedha tu hakutatufikisha mahali.
Hivyo, Tafsiri sahihi ya Kauli ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chadema, inaweza kuhojiwa katika misingi hii. Nimeona nieleze hili kwa misingi ya uwazi kwa vile Chadema hatuna cha kuficha, chama ni cha wote wenye nia njema, na hata wasiokitakia mema kama wapo ni vema wakajua Chadema inaendeshaje shughuli zake ili wasiohoji kwa nadharia na kwa hisia. Mwenye kuhitaji Taarifa zaidi, Dr. Slaa, anapatikana kwa Simu na +255 784 666995 au +255 754 366 995 au kupitia E mail zangu slaa@chadema.net, wslaa@hotmail.com. Nafurahi kwa wote waliochangia kwa angle yeyote ile kwani licha ya kuwa kila mmoja ana uhuru wa kutoa maoni yake, pia kila mwanademokrasia halisi hutambua mchango wa kila mmoja na pia anaweza kuokoteza mawazo mazuri katika michango hiyo. Hakuna mchango uko mbovu tu, hata uliombovu sana unajambo zuri, japo dogo la kuweza kujifunzia. Naomba radhi si nia yangu kutoa mhadhara, lakini kila inapohitajika katika mada yeyote ile nitafanya hivyo kwa maslahi ya nchi yetu, wanachama wetu na wote wenye mapenzi mema.
Dr Slaa
Naamini mwalimu anapomkemea mwanae/mwanafunzi si kwamba hua na nia mbaya naye bali ni kumtaka afanye yaliyo mema zaidi.
Kufananisha CHADEMA na TAA/TANU mimi nafikiri ni upotoshaji kwanini nasema hivi Mazingira yale ya ukoloni ya TANU si haya mazingira ya CHADEMA Na japo sikuwapo wakati huo bado siamini kama TAA/TANU ilikua inapokea ruzuku ya M.66 kwa mwezi kutoka serikali ya mkoloni.
Na bado siamini wale WATUMWA kwa thamani walikua na uwezo wa kuchangia M.66 kwa mwezi kwa TAA yao.
DR Slaa
Naomba nikuchoshe kwa maelezo yanayoambatana na maswali
Nia ya CHADEMA ni nini haswa??? CHADEMA imeanzishwa lini?? Kama hujayapata maswali yangu vizuri ngoja niongeze CHADEMA na CCM kimantiki tofauti yao nini?? My God!!
Kama CHADEMA inazaidi ya miaka 15,kama CHADEMA inapata ruzuku kutoka serikalini .Lakini bado mmshindwa kuweka miradi ya CHAMA kujisimamia chenyewe chama tu mmeshindwa je SERIKALI nzima mtaweza kubuni miradi jinsi ya kutukwamua ??
Serikali bajeti yake kwa 40% inategemea kuomba omba ninyi mnapiga kelele sasa basi mbona chama chunu kinategemea omba omba kwa 100% ,Hamuoni mkiingia madarakani ndio ombaomba itakua zaidi ya 100% maana hapo Mbowe vijisenti vyake havitasaidia kitu,hapo hakuna mfanyakazi atakeyefanya kazi bure.
au na ninyi mtafanya safari nyingi badala ya US mtaelekea kwa PuTIN.
NB: Kama mimi ndio ningekua msajiri wa VYAMA VYA SIASA kabla ya kusajiriwa chama ningepropose kikopeshwe na serikali kama BILION 20. harafu wakaanzisha mradi ambao ndani ya miaka 3 kiwe kimeajili watu zaidi ya 3000 kinawalipa mshahara std ,wakifeli wanatupwa jera kifungo cha maisha,Harafu vyama vyote vilivypo ndani ya Very limited Time wawe na miradi yao inayoendesha chama na wawe wameajiri zaidi ya watu 1000.Kufeli kwa hilo inamaana chama KINAFUTILIWA MBALI.
Maana watu wamekua wasanii tu ili kujinufaisha kumbe hata mpango wa kuwaendeleza watanzania hawanao.
Nasema kufeli kubuni miradi ya CHAMA lakini ukaendelea kuhubiri kubuni miradi ya KITAIFA ni USANII MKUBWA.mtu huwezi shindwa buni miradi ya familia ya kuwapatia kipato familia ikawa inalala njaa harafu ukawa unahubiri kubuni miradi ya wanakajiji wote. USANII HUU.
2) Viongozi wa juu wa Chadema ni Wabunge, ukimwacha Mwenyekiti. Mishahara wanayopata ikitumika kuendeleza Chama kuna dhara gani, Chama hujengwa na wenye moyo. Hili halina maana ya wenye kuchangia chama ndio waamuzi katika maamuzi ya chama. Chama kinaendeshwa kwa Katiba, Kanuni, Maadili, na Itifaki ya Chama. Maamuzi yanapofanywa kwa imla hofu hizo hutokea. Kwa Chadema, ambayo maamuzi yake hufanyika yote na vikao halali, mipango huenda kwa kadiri ya Strategic Plan, ambayo nayo si siri, ipo wazi kwenye Mtandao wa Chama, na kila mwenye nia njema anaweza kuipata bila tatizo. iwapo kuna mwenye kuhitaji maelezo ya ziada tuko tayari kuyatoa wakati wowote, vitabu vya Hesabu ya Chama ni mali ya Wanachama na wakati wowote Mwanachama anaweza kuomba taarifa atapewa, na au anaweza kufika Makao Makuu ya Chama akaona vitabu hivyo bila gharama yeyote. Taarifa zote za fedha hutolewa kwenye vikao vya Kamati Kuu, na sijawahi kuona Taarifa ya Fedha ikikataliwa kwa ubadhirifu au kwa sababu yeyote ile. Wajumbe wa Kamati Kuu ni mashahidi. Taarifa ya Fedha hutolewa pia kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuendana na Ratiba ya Kikatiba ya Vikao hivyo.
4: Ili kuepuka Wachache wenye uwezo kufanya chama kuwa mali yao, Chadema inaoutaratibu ambao sina hakika vyama vingapi unao, wa kutathmini na kutambu mchango wa kila mwanachama kwa maana ya fedha zake anazochangia kwenye chama, muda wake anaotumia kwa ajili ya shughuli za Chama ( hatua hii inafanyika kwa sasa Makao Makuu tu kwa vile Instruments za kufanya Tathmini hii kwenye mikoa na Wilaya bado inafanyiwa kazi na hata ya Makao Makuu bado inaendelea kufanyiwa kazi. Mathalan muda wa mtumishi wa Chama anayefanya kazi baada ya saa rasmi za kazi hutathminiwa na kupewa thamani ya fedha kama mchango wake kwa ujenzi wa chama. Inahitajiwa fikra mpya ili ukombozi tunaoendelea nao uweze kufanikiwa. Lakini kutegemea fedha tu hakutatufikisha mahali.
Gembe + MkamaP,
baada ya kuanzisha kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania, hivi CCM imeweza kuanzisha mradi gani haswa wenye kuweza kutuonyesha jinsi walivyomakini ama wabunifu?
Hivi SUKITA ilikufa mikononi kwa nani?

Kumbe lengo la Chama chako CHADEMA ni kuona wapi CCM imeteleza nyie ndipo mtokeo hapo?
huo ni kukosa ubunifu,na ndiyo tatizo kubwa amblo liko katika watendaji wetu serikalini.Kila siku wanapandisha Bei za BIA,SODA na SIGARA utazani hakuna jambo lingine amblo wanaweza kufanya kuongeza mapato ya Serikali,na kinanikera mimi ni kila mara nikiwa nje ya nchi naktana nao sana ila hawajifunzi chochote kutoka huko zaidi ya kwenda kula starehe..This is a shame.
MMK
Nakushukuru sana kwa ushauri kuhusu uendeshaji wa fedha kwenye vyama vya siasa. Hata hivyo, Chadema ni chama kinachofanya kazi yake kwa uwazi. Hatuna la kuficha napenda kueleza ifuatavyo:
i) Uamuzi wa viongozi wakuu, tena wanaotumia muda wao wote kwa shughuli za chama, za kisiasa na uendeshaji, ni uamuzi uliofanyika kwa hiari na kupitia vikao halali vya chama. Kwa bahati mbaya maamuzi mengine hayafiki hadharani. Chadema haioni cha ajabu katika hatua hii. Mwalimu Nyerere asingejitolea enzi za uhuru, na kuchangiwa na wapenzi wachache waliokuwa na uwezo leo tusingelikuwa na Uhuru. Nadhani wenye mapenzi mema na nchi hii wataelewa kuwa mapambano tuliyonayo ni mapambano yanayohitaji kujitolea kwa kiwango kikubwa. Viongozi wakuu wa Chadema kwa kutambua hili, waliamua kwa hiari yao, kujitolea ili ruzuku kidogo iliyoko itumike kwa shughuli za uenezi. Bendera, Kadi, nyaraka mbalimbali,ujenzi wa Ofisi stahiki Makao Makuu ya Chama kama sura ya Chama, kuwekeza kwenye miradi ya muda mrefu ya kuitegemeza chama( kazi hiyo imekwisha kufanyika siyo nadharia na kwa yeyote mwenye nia ya kutaka kujua tunaweza kumpa taarifa za kina), ziara za uenezi na kadhalika.
2) Viongozi wa juu wa Chadema ni Wabunge, ukimwacha Mwenyekiti. Mishahara wanayopata ikitumika kuendeleza Chama kuna dhara gani, Chama hujengwa na wenye moyo. Hili halina maana ya wenye kuchangia chama ndio waamuzi katika maamuzi ya chama. Chama kinaendeshwa kwa Katiba, Kanuni, Maadili, na Itifaki ya Chama. Maamuzi yanapofanywa kwa imla hofu hizo hutokea. Kwa Chadema, ambayo maamuzi yake hufanyika yote na vikao halali, mipango huenda kwa kadiri ya Strategic Plan, ambayo nayo si siri, ipo wazi kwenye Mtandao wa Chama, na kila mwenye nia njema anaweza kuipata bila tatizo. iwapo kuna mwenye kuhitaji maelezo ya ziada tuko tayari kuyatoa wakati wowote, vitabu vya Hesabu ya Chama ni mali ya Wanachama na wakati wowote Mwanachama anaweza kuomba taarifa atapewa, na au anaweza kufika Makao Makuu ya Chama akaona vitabu hivyo bila gharama yeyote. Taarifa zote za fedha hutolewa kwenye vikao vya Kamati Kuu, na sijawahi kuona Taarifa ya Fedha ikikataliwa kwa ubadhirifu au kwa sababu yeyote ile. Wajumbe wa Kamati Kuu ni mashahidi. Taarifa ya Fedha hutolewa pia kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuendana na Ratiba ya Kikatiba ya Vikao hivyo.
3: Fedha za Chadema hukaguliwa na Wakaguzi wanaotambulika kisheria, na huwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.
4: Ili kuepuka Wachache wenye uwezo kufanya chama kuwa mali yao, Chadema inaoutaratibu ambao sina hakika vyama vingapi unao, wa kutathmini na kutambu mchango wa kila mwanachama kwa maana ya fedha zake anazochangia kwenye chama, muda wake anaotumia kwa ajili ya shughuli za Chama ( hatua hii inafanyika kwa sasa Makao Makuu tu kwa vile Instruments za kufanya Tathmini hii kwenye mikoa na Wilaya bado inafanyiwa kazi na hata ya Makao Makuu bado inaendelea kufanyiwa kazi. Mathalan muda wa mtumishi wa Chama anayefanya kazi baada ya saa rasmi za kazi hutathminiwa na kupewa thamani ya fedha kama mchango wake kwa ujenzi wa chama. Inahitajiwa fikra mpya ili ukombozi tunaoendelea nao uweze kufanikiwa. Lakini kutegemea fedha tu hakutatufikisha mahali.
Hivyo, Tafsiri sahihi ya Kauli ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chadema, inaweza kuhojiwa katika misingi hii. Nimeona nieleze hili kwa misingi ya uwazi kwa vile Chadema hatuna cha kuficha, chama ni cha wote wenye nia njema, na hata wasiokitakia mema kama wapo ni vema wakajua Chadema inaendeshaje shughuli zake ili wasiohoji kwa nadharia na kwa hisia. Mwenye kuhitaji Taarifa zaidi, Dr. Slaa, anapatikana kwa Simu na +255 784 666995 au +255 754 366 995 au kupitia E mail zangu slaa@chadema.net, wslaa@hotmail.com. Nafurahi kwa wote waliochangia kwa angle yeyote ile kwani licha ya kuwa kila mmoja ana uhuru wa kutoa maoni yake, pia kila mwanademokrasia halisi hutambua mchango wa kila mmoja na pia anaweza kuokoteza mawazo mazuri katika michango hiyo. Hakuna mchango uko mbovu tu, hata uliombovu sana unajambo zuri, japo dogo la kuweza kujifunzia. Naomba radhi si nia yangu kutoa mhadhara, lakini kila inapohitajika katika mada yeyote ile nitafanya hivyo kwa maslahi ya nchi yetu, wanachama wetu na wote wenye mapenzi mema.
Kwa sasa ccm wamefeli na ni zamu ya chadema au cuf kuonesha mapungufu ya ccm na kuomba ridhaa ya watanzania kuongoza.
Suala la Pili ni kwamba CHADEMA kama wao wameshindwa kutafuta Wafadhili wa kuendesha chama sababu hakuna watu wabunifu ambao wanaweza kuandika Proposal nzuri labda waandikiwe na kina Baregu au Zitto ila wengi wao ni watu wanotawaliwa na Emotion.
The Truth is Upinzani wa kweli utapatikana mpaka pale CCM itakapogawanyika na kupatikana wapinzani wenye uwezo wa kuongozi siyo wanaotafuta Uongozi.
lengo la chama chochote cha siasa ni kushika hatamu za nchi. Kama chama cha siasa hakina lengo la kuongoza nchi basi hicho chama sio cha siasa.