Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Ndio angalia kuna familia ni baraka vizazi na vizazi na nyingine ni laana mwanzo mwisho
daahhh acha tu "" hapo kwenye " laana na baraqa " nimtihani mnoo"" na kumbuka nilipokuwaga mdogo " kuna familia ya mzee mmoja hivi kwa sasa ni marehemu "" karibia familia ya Watoto wake wote na wajukuu walikuwa ni majambazi na wezi "" kasoro Watoto wake wa kike tu "" yaani sijui alimkoseaga nini Mungu yule mzee ""familia yake ilikuwa inaogopeka mnooo"" na kumbuka mzee wangu aliwahi kunikataza hata kujenga urafiki na wajukuu wa familia ile
 
Aliye ona uchi ni Ham baba wa canaani

5 mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5
 
Kwa nini alilaaniwa Canaan ambaye hakujua kosa na si aliyemchungulia?
Aliye ona uchi ni Ham baba wa canaani

5 mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5
 
Hivi inakuwaje kosa afanye mtu mwingine then adhabu apewe mwingine? hii imekaaje? Sometimes Bible huwa siielewi yani
Hii inahitimisha

5 mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5
 
Hebu nami nitupie machache ktk huu mjadala, kadri ambavyo nimerudia rudia tena na tena kusoma hii incident ya Noah najiwa na maswali mengi baadhi ni kama hivi!
1.Je ni muda gani ulipita tangu family hii itoke ktk safina mpaka tukio hili lilipofanyika.?
2.Canaan alikua mtoto Wa NNE Wa Shem , je huyu mtoto alikuaje kuaje mpaka Noah hakuingiwa na huruma yoyote kumpa laana nzito vile?
3. Je Ham alifuata nini ktk Tent la baba yake mpaka akamkuta ktk hali ile ilihali alikua ni MTU mzima mwenye mke na watoto na makazi yake?
6.Na kama ilikua bahati mbaya kwanini akaenda kuwasimulia nduguze tukio hilo kama vile it was funny ?
7.Yawezekana hakuwa na nia mbaya(ovu) alikwenda kwa baba yake may be kuzungumza but akamkuta amelewa akakereka na hilo hivyo kwa hasira akawambie nduguze "Ah baba mlevi kweli nilienda kuongea nae nmekuta yuko uchi kalala huko ndani" ndipo nduguze wakaenda kumfunika, lkn waliwezaje kumfunika pasipo na wao kumwona utupu ???.
Mwisho kabisa Noah alitambuaje yote haya wakati alikua hana ufahamu kwa pombe ?? Na kwanini hakutoa hata muda kutaka kujua jambo hilo kabla hajatoa hukumu ?
 
Hapana hapa umechanyanga mambo.. Angalia msingi wa mada hebu soma tena kwa makini
Msingi wa mada nimeuelewa sana ila kuna kitu hapo kuhusu laana ya vizazi kwa vizazi mlijaribu kuzungumzia kama sehemu ya utetezi sasa ndio nataka maoni yako kuhusu hili jambo kutoa laana kwa vizazi ambavyo avijashiriki kwenye uovu uoni sio jambo jema maana mnawanyima fursa ya kutubu ni ilo mkuu
 
Mkuu lawama na laani ni vitu tofauti sana. Waziri hawezi kuua mtu huko Iringa then Magufuli ndo akamatwe Mmmh!! hapana.

Haya maandiko ya Bible me yananivuruga sana Ukisoma Mwanzo 3:17 Mungu anailaani ardhi sababu ya Adamu sasa ardhi ilifanya kosa gani pale Eden?

Yoshua 7:24+ Akani alifanya dhambi ya kuiba aliteketezwa yeye na uko wake mzima hadi ng'ombe, punda, na vitu vyake vyote. sasa wao viumbe wengine walikosa nini wahusike kwenye adhabu ya Akani?

Sikumbuki ni kitabu gani but utanisaidia kama unakijua. kuna mtumishi mmoja wa Elisha Nabii alifanya kosa kumuomba zawani Naamani alieponywa ukoma na Elisha nabii. Huyo mtumishi alipatwa na ukoma yeye na ukoo mzima. sasa wao ndugu zake wengine walifanya kosa gani mpk wahusishwe kwenye adhabu ya huyo mtumishi?

Najiuliza Mungu yukoje? na anatumia kanuni, sheria, utaratibu gani kuadhibu watu vitu ambavyo hata havijahusika kuadhibiwa pasipo kosa?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…