Kwanini bei za mafuta zimepanda zaidi mwezi Mei 2022?

Monica Mgeni

Member
Oct 7, 2021
82
134
Taifa Digital Forum imefanya ufuatiliaji wa kina juu ya ongezeko la Bei ya Mafuta ya Nishati Nchini na kubaini kuwa katika kupindi cha Mwezi Machi 2022, bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia ilikuwa ni ya juu zaidi ikilinganishwa na bei za miaka 14 iliyopita.

Hali hiyo imesababishwa na dharura ya Vita kati ya Urusi na Ukraine iliyoanza tarehe 24 Februari 2022.

Kufuatia vita hii, bei ya Mafuta ghafi katika soko la Dunia ilipanda kutoka dola 96 kwa pipa hadi karibu dola 140 (ambalo ni ongezeko la 44%) ndani ya wiki mbili.

Kulingana na taratibu za mfumo wa ununuzi wa Mafuta wa pamoja (yaani Petroleum Bulk Procument System –BPS), kampuni za uuzaji wa mafuta huagiza/kununua ‘Stock’ (hisa) miezi miwili kabla.

Ambapo inamaanisha, mnamo Mwezi Machi 2022 kampuni za uuzaji wa mafuta ziliagiza stock za mwezi Mei 2022 katika kipindi hicho cha mwezi Machi. Na Kwa kuwa bei za Mwezi Machi 2022 zilikuwa za juu zaidi, ni lazima Bei za Kikomo za Mwezi Mei 2022 ziongezeke kwa kiasi kikubwa.

Tanzania ni mwagizaji mkuu wa bidhaa ya mafuta na hivyo tunategemea kwa asilimia 100 bidhaa za petroli zinazoagizwa kutoka Nje. Ndio maana, tunaguswa moja kwa moja na ongezeko la bei ya mafuta katika Soko la Dunia.

Kwa nchi zinazozalisha mafuta, wakati mwingine bei zake zinakuwa ni tofauti kwa sababu baadhi yao huweka vikwazo vya kuuza nje kwa kuweka ushuru wa mauzo ya nje kwa bidhaa za petroli. Ushuru kama huo hutumika kupunguza bei ya bidhaa za petroli zinazosambazwa katika soko la ndani.

Baadhi ya watu ambao ama kwa kukosa uelewa au kwa nia mbaya wanapotosha umma kwa makusudi kwa kuhusisha ongezeko la sasa la bei ya Mafuta na kile kinachoitwa mapungufu ya mfumo wa Taratibu za uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (yaani Petroleum Bulk Procument System -BPS). Jambo ambalo sio kweli.

TAIFA DIGITAL FORUM Reflects the Nation
 
Tanzania inaagiza nchi gani na vita viko nchi gani? Hebu jibu hilo kwa ufasaha kisha ndio uendelee na utetezi wako wa uhuni unaofanywa na mamlaka husika!
 
Usitudanganye!

stock ya mafuta waliyonayo bongo ni ya miezi sita nyuma na walinunua kwa bei ndogo, sasa waliposikia tu Russia karusha kombora moja Ukraine majizi hayo yakaja mbio kutumaliza kwa kupandisha bei ya wese maradufu!!

Lete documents utuoneshe hapa kama mafuta tunayouziwa sasa yameagizwa kabla au baada ya kuanza vita ya Urusi na Ukraine!

Binadamu ni kiumbe mjinga unawakomesha wenzako unawanyanyasa unawaibia unawapiga unawatukana halafu one day unadedi na hao hao wanakufukia na michanga na udongo hawa kina Makaaambakoo sifa zimezidi Mungu anawaona!!
 
Back
Top Bottom