Kwanini bei ya mafuta kwa Tanzania siyo rafiki?

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
504
953
Kila Jumatano ya mwanzo wa mwezi EWURA wanatangaza bei mpya ya nishati ya mafuta. Kwa asilimia kubwa kila wakitangaza ni ongezeko tu la bei na siyo punguzo.

Ukichukua mfano wa nchi zote za jirani zetu bei zao ni pungufu kuliko ya Tanzania. Hivi Tanzania tuna tatizo gani na tunawabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama ya mafuta. Leo hii Kenya wamepunguza bei ya mafuta lakini kwa Tanzania kila kukicha bei inapanda.

Kama nchi chukueni hatua mtafanya wananchi waichukie Serikali yao.
 
Kwa utawala wa huyu malikia wenu kuna nini kina nafuu?

Ukinunua luku unakatwa 1,500 eti kodi ya jengo?

Kaongeza elfu 1 kwenye kila mfuko wa sement

Katika hali kama hiyo kwanini mafuta yasipande?

Huyu yeye aliona njia alizokuwa anatumia Magu kudai kodi eti ni za zuruma, baada ya mambo kuanza kumchachia ndio akarundika makodi na matozo kwenye vitu vinavyomkamua mwananchi yakiwemo mafuta.
 
Sasa wanaopaswa kukemea upandaji wa bei ya vitu ndio wafanyabiashara wakuu wa vitu hivyo hivyo.

Unatarajia Shabiby au Nchemba akemee bei za mafuta kupanda ikiwa wanamiliki vituo vya mafuta.

Huyo Mama Abduli mwenyewe ana manufaa yake binafsi kila sehemu halafu mnategrmea atakemea.

Sasa hivi mkombozi wetu ni Mungu pekee.
 
Mie kinachoniuma na kuionea huruma Tanganyika ni eti Malkia ana mpango wa kugombea (na kushindishwa) kwenye nafasi ya urais!.
Mama hatoshi kabisaa, amewaamini wahuni na tayari wameshamdhibiti!.
 
Kila Jumatano ya mwanzo wa mwezi EWURA wanatangaza bei mpya ya nishati ya mafuta. Kwa asilimia kubwa kila wakitangaza ni ongezeko tu la bei na siyo punguzo.

Ukichukua mfano wa nchi zote za jirani zetu bei zao ni pungufu kuliko ya Tanzania. Hivi Tanzania tuna tatizo gani na tunawabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama ya mafuta. Leo hii Kenya wamepunguza bei ya mafuta lakini kwa Tanzania kila kukicha bei inapanda.

Kama nchi chukueni hatua mtafanya wananchi waichukie Serikali yao.
Kugharamia anasa na safari zao.kwenda ufaransa kutalii
 
Mkuu Mzimu wa Kolelo Salam kwako.
Naona hapa umetoa tuhuma nzito sana, naomba kama hutojali ututaji jina au majina ya hivyo vituo vya mafuta.
Ahsante
Mimi naona hakuna haja ya kumsumbua MTU asiyependa maendeleo, Sisi tunaohitaji maendeleo tusogezewe huduma zote kwenye maeneo yeti hasa hivyo vituo vya mafuta tutanunua hata mafuta ya taa kupunguza jam ya maduka ya mangi kujaziwa kila kitu mpaka usafi ukosekane, mambo mazuri yaje kila mtaa, Kwanza maendeleo yamechelewa Sana kwasababu ya tabia ya kupenda kuwa fungu la kukosa na maisha mazuri tunaachia watu weupe.
 
Hivi kwa nini wamiliki wa vituo vya mafuta hawaweki vituo vya gesi?? Naskia viko Dar tu..na ni viwili tu.
 
Back
Top Bottom